Karibuni Wachina na mikataba yenu ya ujenzi wa Bandari Bagamoyo

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,982
1,521
Huenda ikawa baada ya miaka 100 ijayo ngozi nyeusi ikapatikana kwa nadra hapa Tanzania kama ilivyo kwa Madagascar na Mauritius. Kupata mtu mweusi wa asili itabidi labda uende ndani kabisa mashambani huko vijijini. Majina ya asili yatachanganyikana na ya kichina kwa hiyo yatapotea kabisa.

Majina kama 'Mpango' utakuta limeshabadilika kutokana na uzalishwaji wa mbegu mpya wakati huo utakuta mtu anataitwa 'Mpanguang'. Kile kizazi cheusi kilichobaki wataonekana kama watumwa katika ardhi yao lakini baada ya muda mrefu watajikusanya na kuanza kudai nchi yao.

Kwa hiyo itakuwa ni vita ya ukombozi vya watwana kujikomboa kutoka kwa mabwana ambao ndiyo watakuwa wanafidi nchi.

Mungu apishilie mbali hili.
 
Hawa ni nyumbu a.k.a wazee wa legasi bado wanaweweseka.

Yule mtu alijua kushika watu masikio....eti mkataba unabana sasa kwanini wewe usiubanue.
 
... ya Karl Peters na Mangungo!

Kuna mikataba iliyofanywa zamani sana bado inatusumbua; mojawapo ikiwa ni matumiz ya maji kwenye ziwa victoria. Unapoingia mikataba ya muda muda mrefu ni lazima kuwa na viongozi wenye maono zaidi ya Mangungo.
 
........ ya Karl Peters na Mangungo!

Kuna mikataba iliyofanywa zamani sana bado inatusumbua; mojawapo ikiwa ni matumiz ya maji kwenye ziwa victoria. Unapoingia mikataba ya muda muda mrefu ni lazima kuwa na viongozi wenye maono zaidi ya Mangungo.
Hivi wa loliondo upoje kwa sasa na wa Kia aka KADcO
 
Hivi wa loliondo upoje kwa sasa na wa Kia aka KADcO
Mingine inaweza kuwa bado inatusumbua, wa Loliondo ulikuwa ni wakati wa Mwinyi, kama ulikuwa ni miaka 33, inawezekana unakaribia kuisha ila kama ulikuwa wa miaka 99, utatusumbua sana.
 
Back
Top Bottom