Karibuni Kwenye Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere-Jumapili 14 Oktoba-Nkrumah

Kwani sasa hivi Zanzibar haipo? Nikuhakikishie jambo moja: Hata Muungano ukivunjika leo, Tanzania itabaki. Hatuwezi kurudi kuitwa TANGANYIKA. Asilimia kubwa ya watu wetu ni WATANZANIA. Wamebaki akina Kingunge, Wassira, Jakaya, Lowasa,...., ndio waliozaliwa Watanganyika.


Mkuu vipi unaona aibu kuitwa Mtanganyika hata ung'ang'anie jina lenye elements za Zanzibar japo imeshajiondoa kwenye Muungano?

Waswahili wanasema "mkataa asili kafiri" .......
 
Tupende mabadiliko, tukiwasikiliza akina Dr Lwaitama kila siku hatutapata mawazo mapya. Mimi kwa mfano nilisoma na Ester Wasira ana hoja nzito sana. Nadhani tuwape nafasi na tuanze kulea kizazi kipya kitakachochukua nafasi za akina Prof Issa Shivji

Hebu tumwagie wasifu wa huyo Ester Wasira.

Ni nani, anafanya shughuli gani hivi sasa, na mengineyo kama hayo

Ahsante
 
Kuna Pro-Chadema kasema bora viongozi wa Bavicha wangekuwepo, Chadema bana.

Kwa taarifa yako hapo tuna kamanda Dk Vincesia Shule,huyu ni mbaya kuliko hata hao viongozi wa CHADEMA unaowafahamu,ni kamanda anayeshambulia kimyakimya.
 
UDASA & ITV

Wanawaletea


Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere


Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Tarehe: Jumapili 14 Oktoba 2012
Muda: Saa 8.00 mchana hadi Saa 11.30 jioni(2.00pm-5.30pm)
Ukumbi: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule


Wote Mnakaribishwa


Dr.Mkumbo naona litendee haki jukwaa hili kwa kuwaambia wana JF na labda utakuwa unaongea na umma wa Watanzania umetumia vigezo gani kuwaalika waliotajwa kama wasemaji wakuu kwenye kongamano hili. Wachache tunaowafahamu sidhani kama wana kitu (something tangible) kuwaambia Watanzania na walimwengu jukumu la vijana kihistoria katika kumwenzi Mwalimu Nyerere. Mwalimu alikuwa ni Mzalendo wa kweli aliyeipenda nchi na Watanzania. Hakuwa mbinafsi na yeye allichokihubiri ndicho alichokiishi. Alitetea wanyonge na siku zote alipigana ili wanyonge wanyanyuliwe na alionyesha kwa vitendo-kutaifisha shule ili wanyonge wasome na akawawekea viwango vidogo vya ufauru ili wasome na wao siku moja wapambane na maisha na wasijione ni wanyonge tena, hakukuwa na matumizi ya fedha kwenye kuupata uongozi, alizuia ubaguzi wa aina yoyote na mengine mengi. Sasa mwongeaji mkuu mmoja hapo anaitwa Jerry Silaa. Sijui huyu ana uhalali gani wa kutuambia Watazania vijana jukumu letu kihistoria kumwenzi Mwalimu wakati yeye kama mmoja wa viongozi wa UVCCM na kwa maana hiyo CCM wamewafanya Watanzania na hasa vijana kuchanganyikiwa maana umoja uliokuwepo wa vijana regardless of ideologies hivi leo umekwisha na kuna viongozi wa CCM ndio wanaopigana begabega kwa bega kuhakikisha vijana hawaungani tena. CCM kwa kutumia vijana na wazee wamepandikiza sumu ya udini, hitikadi, ukanda na kuonyesha kuwa these evils are the apex even where they are not. Everything is now judged in terms of religion, regionalism and political affiliation. Kuvuliwa mtandio wa DC Igunga na CCM walivyoutumia kama mradi, kuuawa kwa raia wasio na hatia na polisi kwa kisingizio cha kuzuia maandamano, hotuba za Makamba zenye ubaguzi wa kidini kuelekea uchaguz 2010 na mengine mengi. Sikumbuki kumsikia Jerry akiongea na kuonekana amejitofautisha na wenzake. Sikumsikia akimwambia Shigella kuwa katika majonzi usilete siasa. Polisi wameua unasema walioua ni CDM ati kwa sababu walikuwa na mkutano. Hivi kweli bunduki inamtoa mtu utumbo na imeshikwa na polisi na hili ni la kiongozi wa juu wa UVCCM kulikataa. Nilitegemea vijana tena wenye wadhifa UVCCM waje na wao wasema Shigella "causa proxima non remota spectatur"- immediate cause rather than remote cause.

Other vices that have shaken the country to its core ni wizi wa fedha ya umma-EPA, Richmond, Meremeta, Nyumba za serikali ziligawiwa kwa viongozi, mikataba mivovu ya madini na gesi. Litania ni ndefu. Wapo vijana wanaopiga kelele lakini sikumbuki kumsikia Jerry mbali na kuwa na wadhifa CCM/UVCCM. Na baadhi ya kashfa hizi pesa yake ilikwenda kuinufaisha CCM kwenye chaguzi ikiwemo na ile ya magari ya CCM ya uchaguzi. Mkubwa mmoja wa mamlaka ya Mapato alipojaribu kupinga kusamehewa kodi kwa magari hayo lilomkuta kila mtu anajua. Tulitegema vijana kama Jerry ndio waongoze mapambano ya kupinga haya. Lakini kama hili halitoshi yeye Jerry ni mwanamtandao akianzia pale UDSM miaka ya kuelekea uchaguzi wa 2005. Akiwa rafiki wa Riz1 wanajua walichokifanya ili waliyemtaka ashinde. The least I can say the set bad precedence na matatizo haya tunayoyaona na bado yanatutesa have got origin from wanamtandao. Sasa kijana wa aina hii atatwambia nini? Au alipokuwa diwani and then meya ameongoka? Kama ndivyo yetu macho na masikio lakini bado tujuavyo bado wale wale waswahili wa Pwani wajuanao kwa vilemba
 
UDASA & ITV

Wanawaletea


Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere


Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Tarehe: Jumapili 14 Oktoba 2012
Muda: Saa 8.00 mchana hadi Saa 11.30 jioni(2.00pm-5.30pm)
Ukumbi: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule


Wote Mnakaribishwa

Ningeshauri,ili kongamano linoge mngetafuta mzee mmoja mropokaji anayeweza amsha hasira za wachangiaji..nashauri mtu kama Wassira,au Sitta anafaa sana.
 
UDASA & ITV

Wanawaletea


Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere


Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Tarehe: Jumapili 14 Oktoba 2012
Muda: Saa 8.00 mchana hadi Saa 11.30 jioni(2.00pm-5.30pm)
Ukumbi: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule


Wote Mnakaribishwa

Hapo kwenye blue huyo gamba kilaza hafai kabisa! tafuteni mtu mwingine.
 
Dr. Mngeongeza na vijana wa Nyerere kama akina Generali Ulimwengu, Salum Salim yule mwandishi wa habari wa Zanzibar, akina Joseph Mihangwa, Paul Kimiti, Dr. Lwaitama, wapo wengi sana ambao walifanya kazi na Nyererere wakiwa vijana na mpaka sasa hawajajiunga na kundi la waabudu Fedha. Waongeze kiongozi ili tuje tupate raha. Maana watatoa changamoto zetu wanavyoziona wao na hawa uliowaweka watatoa kwa macho yetu sisi vijana wa leo.
 
Ametuachia umaskini usiokuwa na mwisho halafu leo tumuenzi si upuuzi mwingine huu pelekeni facebook huko.

Alitamani uondokane na umaskini wa akili ili ukusaidie kuyaona maisha katika taswira chanya na ukusaidie uondokane na umaskini wa mwili. Lakini bahati mbaya hukutaka ku-enjoy hiyo opportunity ndio maana umebaki ukiwa biased and prejudiced maana haingii mtu asiyekuwa na umaskini wa akili amlaumu marehemu aliyefariki miaka 13 iliyopita. Hivi umeshikwa mikono. Channgamsha akili, nenda shule na tumia fursa zilizopo tena nyingi alizitengeneza Mwalimu au alizilinda manyangau wasizipore ingawa sasa hivi wameamua kuzigawa na kujigawia
 
UDASA & ITV

Wanawaletea


Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere


Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Tarehe: Jumapili 14 Oktoba 2012
Muda: Saa 8.00 mchana hadi Saa 11.30 jioni(2.00pm-5.30pm)
Ukumbi: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule


Wote Mnakaribishwa

lakini hao wazungumzaji hawaendani na hadhi ya Kongamano! UDASA inaheshimika sana nchini hebu jaribuni kuwaleta watu ambao jamii itawakubali kwa kuzungumzia uhalisia wa kumbukumbu. Mfano wangekuwapo washiriki kama...

1.Prof.Issa Shivji
2.mzee Sitta.
3.Mzee Edwin Mtei
4.Mkapa
5.Mbowe
6.Lipumba na wengineo kongamano lingenoga sana na kubeba sura ya kitaifa.
 
Ningeshauri,ili kongamano linoge mngetafuta mzee mmoja mropokaji anayeweza amsha hasira za wachangiaji..nashauri mtu kama Wassira,au Sitta anafaa sana.
Wassira na Sitta hawamkumbuki vizuri Mwalimu ingawa ndie alieanza kuwatoa huko walikokuwa. Mwalimu aliwatupilia mbali wakati fulani wakabaki wabangaizaji mtaani.
 
Nilichogundua mie na wewe tupo tofauti kiumri, ninaposema wakongwe Mwl Kitila Mkumbo, kanielewa shughuli yeyote ya Mwl Nyerere pale Nkurumah lazima wakongwe kama Prof Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu, Salim A Salim wanakuwepo.
Ofcourse kwa maneno-"Shughuli" na "Lazima" tupo tofauti,

Mkuu, umeamua kujivua nguo jamvini, nimekwambia hii issue imekaa kitaaluma siyo kisiasa kama unavyopost vitu vyako vya hovyo hovyo, hujui unajifanya unajua, Cheki unavyoumbuka... UDASA ndio wameandaa Nkruma Hall, KIGODA CHA MWALIMU, ndio wapo hao wazee na watafanyia kongamano lao IRINGA, Tumain University.

Mpaka hapa nikuiteje?
 
Mkuu vipi unaona aibu kuitwa Mtanganyika hata ung'ang'anie jina lenye elements za Zanzibar japo imeshajiondoa kwenye Muungano?

Waswahili wanasema "mkataa asili kafiri" .......
Muhimu ni hawa wahuni wa Zanzibar kuondoka na Zanzibar yao. Hili la kubadili jina lina usumbufu na gharama zake nyingi tu kitaifa na kimataifa pia. Kuna vitu vingi tu tutabadili tukiendekeza hili ukiwemo wimbo wa Taifa, nembo za kitaifa, uraia,..., yote hayo ya nini.

Jina lenyewe Tanganyika limekaa kishamba sana. Teh Teh.
 
Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere

Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule

Mada ya Muungano wa Tanzania na muungano wa Afrika ni mada nzuri, muhimu kuitoa katika kongomano hilo. Mwalimu ni muumini wa Muungano,alipigania muungano wa Afrika.

Desa hili kwa atakaepata nafasi ya kufika Mlimani. "Changamoto ya Muungano wa Tanzania na umoja wa Afrika Mashariki katika kumuenzi Mwalimu Nyerere."

Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Shirikisho la Afrika mashariki.

Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki (uk. 90-92)

MmMiongoni mwa mambo mengine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:
a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007

b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009

c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009

d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo.


Michakato ya mashauriano ya kitaifa ilizinduliwa mwezi Oktoba nchini Tanzania, Kenya na Uganda na mwaka 2008 nchini Rwanda na Burundi.

Waafrika Mashariki walikubaliana kwa kauli moja juu ya shirikisho la kisiasa.

Yalitolewa pia mawazo ya kupinga uharakishwaji. Wasiwasi mmoja uliojitokeza kutokana na mchakato wa mashauriano nchini Tanzania ulikuwa ni suala la kuitenga Zanzibar kabisa, chini ya serikali ya Muungano katika serikali ya shirikisho.

Link shirikisho

 
Muhimu ni hawa wahuni wa Zanzibar kuondoka na Zanzibar yao. Hili la kubadili jina lina usumbufu na gharama zake nyingi tu kitaifa na kimataifa pia. Kuna vitu vingi tu tutabadili tukiendekeza hili ukiwemo wimbo wa Taifa, nembo za kitaifa, uraia,..., yote hayo ya nini.

Jina lenyewe Tanganyika limekaa kishamba sana. Teh Teh.

Nadhani hicho ndicho kinachokusumbua. Kasumba ya kuwa jina Tanganyika limekaa kishamba.

Huna tofauti na wale wanaokataa majina ya babu zao kisa hayaendani na image zao za "kimjini mjini"

Aibu kwako
 
Tupende mabadiliko, tukiwasikiliza akina Dr Lwaitama kila siku hatutapata mawazo mapya. Mimi kwa mfano nilisoma na Ester Wasira ana hoja nzito sana. Nadhani tuwape nafasi na tuanze kulea kizazi kipya kitakachochukua nafasi za akina Prof Issa Shivji

Kwani wangechanganywa na watu wenye umri mkubwa na ambao wanamfahamu vizuri mwalimu ingekuwa shida?

Ndo maana nikasema kama ni kongamano la vijana peke yao basi iwekwe wazi na hata title ibadilishwe.

Vinginevyo, tabia ya kutopenda kusiliza hoja zinazotofautiana na zetu inaanza kujengeka na huko mbele itatupa matatizo makubwa!!
 
Hakika tunapaswa kupata tafakuri ya ndani kuhusu mustakabari wa taifa letu hasa katika kipindi amabacho mwalimu hayupo na tukiweza tujifunze kuweza kusimamaia yale ambayo mwalimu aliyaamini na kutyaona yana manufaa kwa taifa letu.

Tunapaswa kumuenzi mwalimu kwa vitendo na sio kwa kufanya yale ambayo aliyakataa na kutya pinga waziwazi.
 
Mkuu
Naona mmekosa kabisa wazungumzaji ama? Kibamba na Mh J.Silaa, hawana credibility ya kuwa wazungumzaji, kwenye kongamano kubwa kama hilo la wanazuoni, tena ni UDASA!!.... huyo Kibamba ni mropokaji tu.. ni mtu wa ndimu mbili, hafai, Silaa nae ndio kabisaa, anaishi maisha gani? Kibamba usanii anajitengenezea jina ili apige pesa kwa wafadhili, Silaa.. uchaguzi UVCCM... hamna kitu hao.kwa vyovyote vile hao hawana connection nzuri ya maisha yao na mada tajwa!

Mkuu, kwenye familia ya Nyerere hakuna Kijana/mtu mzuri wa kuweza kuwa ni mzungumzaji mnatuwekea hao wasanii?
Ni kwanini magongamano ya Mwl. Nyerere huwa hamhusishi na familia yake?

Sijafahamu sifa walizotumia UDASA na ITV kuwaalika hao wawili kuwa wazungumzaji. ndio maana huwa nasema hakuna mtu hapo UD atakaeweza kuziba pengo la Prof. Chachage.RIP

Kongamano hilo ni kubwa ila limefanywa kuwa ni rahisi tu, Nitafika ama kuangalia ITV, kuwaona/ kuwasikiliza hao wawili (Blue) kwa kuwa siwafahamu, ila Prof. Chachage kafa na UDASA yake. full stop.

Mwisho! Kuna wana JF wangeweza kuliko hao wasanii hata Ritz TUMBIRI Mungi chama mikaelPAwenda benSaanane mwaJ na wengine kibao

Mkuu POMPO Kama kweli ulimaanisha Ritz , utakuwa uliteleza kidogo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom