Karibuni Kwenye Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere-Jumapili 14 Oktoba-Nkrumah

Hii siku inaigharimu sana serikali!...hebu wataalamu tufahamisheni ni kiasi gani cha pesa serikali inapoteza kwa siku moja hii "Nyerere Day" hasahasa inapoangukia siku ya kazi ambapo uzalishaji,utendaji husimami na serikali kukosa pato kama vile ukusanyaji wa kodi.
Wataalamu tuwekeeni kiasi cha pesa ambayo serikali inapoteza kwenye hii siku moja ili tuone kama kweli kuna faida kwa nchi changa kama Tanzania kujiongezea mzigo mzito namna hii kwa ajili tu ya Nyerere.
 
UDASA & ITV

Wanawaletea

Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere

Mada Kuu: 'Nini Jukumu la Kihistoria la Vijana Tanzania katika Kumuenzi Mwalimu Nyerere?

Tarehe: Jumapili 14 Oktoba 2012
Muda: Saa 8.00 mchana hadi Saa 11.30 jioni(2.00pm-5.30pm)
Ukumbi: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Wazungumzaji Wakuu

1. Ndugu Deus Kibamba
2. Mheshimiwa Jerry Silaa
3. Ndugu Esther Wasira
4. Dk Vincesia Shule

Wote Mnakaribishwa

Hii mada ingenoga angealikwa Mwenyekiti wangu wa BAVICHA Kamanda john Heche. Au kwakuwa amesoma St. Augustino ndo maana hajaalikwa?
 
Last edited by a moderator:
I will be there if God wishes,maana bado naweza kamata basi la kurudi morogoro baada ya Kongamano hilo,Asante my former president of daruso!
 
  • Thanks
Reactions: MC
Hii siku inaigharimu sana serikali!...hebu wataalamu tufahamisheni ni kiasi gani cha pesa serikali inapoteza kwa siku moja hii "Nyerere Day" hasahasa inapoangukia siku ya kazi ambapo uzalishaji,utendaji husimami na serikali kukosa pato kama vile ukusanyaji wa kodi.
Wataalamu tuwekeeni kiasi cha pesa ambayo serikali inapoteza kwenye hii siku moja ili tuone kama kweli kuna faida kwa nchi changa kama Tanzania kujiongezea mzigo mzito namna hii kwa ajili tu ya Nyerere.
Kwa kweli ni ghali sana siku hii moja kuliko Krismas na Boxing yake. Ghali zaidi kuliko zile Eid zote. Hata zile Ijumaa Kuu, Pasaka na Jumatatu ya Pasaka ni cha mtoto! Akina Mohamad( S.A.W) na Yesu wameifanyia makubwa sana nchi hii.
 
Mimi Siji Kwani nimuenzi kipi cha maana alichotufanyia na aende zake huko

sasa umeandika nini hapa? umepewa na umepata nafasi a kutoa maoni yako badala ya kuitumia vizuri unaandika upumbavu kua na hekima basi
 
Sideeq, ni watu wasioona mbali na wasioweza kuchambua mambo kama wewe wanaweza kusema hakuna sababu ya kumuenzi Mwl. Unataka tumwezi JK au nani.:)..
 
Hizi zilikuwapo na zikisherehekewa kabla ya Nyerere!zinaligharimu Taifa tayari kwa ridhaa ya wananchi wote, sasa kulikuwa na faida gani ya kuliongezea Taifa gharama nyingine tena kwa ajili ya Nyerere?
 
Hiyo ridhaa ya wananchi wote ilipatikanaje, kwa kura ya maoni? Mimi nisie Mkristo wala Mwislamu zinanigharimu kwa nini? Mwalimu kayagusa moja kwa moja maisha ya WATANZANIA wengi tangu mwaka 1954 hadi 1999. Tusimuenzi kweli?
 
Sideeq, ni watu wasioona mbali na wasioweza kuchambua mambo kama wewe wanaweza kusema hakuna sababu ya kumuenzi Mwl. Unataka tumwezi JK au nani.:)..
Mkuu hebu nichambulie hizo sababu na kama zinatosha kulifanya Taifa zima liingie gharama kubwa.
 
Hiyo ridhaa ya wananchi wote ilipatikanaje, kwa kura ya maoni? Mimi nisie Mkristo wala Mwislamu zinanigharimu kwa nini?
Mpaka sasa hakuna Muislamu,Mkristo wala Mpagani aliyelalamika kuhusu kuwepo kwa hizi sikukuu, hivyo hii inahesabika kuwa ni ridhaa.
WildCard said:
Mwalimu kayagusa moja kwa moja maisha ya WATANZANIA wengi tangu mwaka 1954 hadi 1999. Tusimuenzi kweli?
Hapa ndio tatizo linapoanzia! hao ambao maisha yao yameguswa moja kwa moja na Nyerere wakitaka kumuenzi basi wafanye kivyao, isiwe ni kulibebesha Taifa zima gharama.
 
Mpaka sasa hakuna Muislamu,Mkristo wala Mpagani aliyelalamika kuhusu kuwepo kwa hizi sikukuu, hivyo hii inahesabika kuwa ni ridhaa.Hapa ndio tatizo linapoanzia! hao ambao maisha yao yameguswa moja kwa moja na Nyerere wakitaka kumuenzi basi wafanye kivyao, isiwe ni kulibebesha Taifa zima gharama.
Kumbe kukaa kimya ni ridhaa! Hakuna ambaye hakuguswa au hataguswa na aliyoyafanya Mwalimu NCHI hii. Hata wewe unayemchukia kuna mahala kakugusa ati!

Hizi sikukuu za KIDINI tuwaachie wenye dini zao wahangaike nazo. Nitalipeleka wazo hili kwenye Tume ya Katiba Mpya. Serikali na vyama vyetu vya SIASA havina DINI. Wapo WATANZANIA kwa mamilioni sio Wakristo wala Waislaam.

Mungu mwenyewe dini hana!
 
Unaweza kuiandika HISTORIA ya Tanganyika/Tanzania bila kumtaja Mwalimu?
Hilo rahisi tu! kama vile wengine wanavyoiandika bila ya kumtaja Abushiri, Kinjeketile, Mkwawa na wengineo...kama hawa "wamesahauliwa" kwa nini iwe vigumu kwa Nyerere kusahauliwa?!
Huwezi kuindika pia bila ya kumtaja Mwarabu,Mjerumani,Mwingereza.......
 
bado unasadifu hilo jina ona unavyojigonga!!! waongeze wakongwe ama nguvu? ndio ukilaza wenyewe huo, umesahau kitu cha dakika60 tu, ndio huitwa umelaza yaani kilaza....soma nayoyaita maoni yako ya kwanza na unachosema sasa

Nilichogundua mie na wewe tupo tofauti kiumri, ninaposema wakongwe Mwl Kitila Mkumbo, kanielewa shughuli yeyote ya Mwl Nyerere pale Nkurumah lazima wakongwe kama Prof Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu, Salim A Salim wanakuwepo.
 
Last edited by a moderator:
Hii siku inaigharimu sana serikali!...hebu wataalamu tufahamisheni ni kiasi gani cha pesa serikali inapoteza kwa siku moja hii "Nyerere Day" hasahasa inapoangukia siku ya kazi ambapo uzalishaji,utendaji husimami na serikali kukosa pato kama vile ukusanyaji wa kodi.
Wataalamu tuwekeeni kiasi cha pesa ambayo serikali inapoteza kwenye hii siku moja ili tuone kama kweli kuna faida kwa nchi changa kama Tanzania kujiongezea mzigo mzito namna hii kwa ajili tu ya Nyerere.

ni kweli tunakosa kukusanya kodi ya kuwatajirisha mafisadi kama wewe!
 
I will be there if God wishes,maana bado naweza kamata basi la kurudi morogoro baada ya Kongamano hilo,Asante my former president of daruso!

Shembango, vipi ulikuwa kwenye Team ya kampeni ya Dr. Kitila for Daruso president nini? mi nilikuwa kitengo cha wabandika matangazo na picha kwi kwi kwi.......
 
Back
Top Bottom