Elections 2010 Kampeni ya CUF live on TBC1 Taarab kwa sana

Anazungumzia uhaba wa maji Dar, hii ahadi hata Jk aliizungumzia sana....Staili anayotumia Lipuma haitofautiani sana na ile ya JK, sina uhakika kama watu wanamwelewa vizuri
 
kazungumzia matatizo, ya maji na tatizo ya ajira, umeme na viwanda n.k....Lipumba anashindwa kutumia vizuri jukwaa hili kuwaconnvice watu hizi staili ya maelezo ni rahisi sana kwa Jk kupangua, Duni haji alianza vzr, huyu mwenyekiti anakosea direction aliyoianzisha duni haji
 
anazungumzia ile riport ya wanafunzi wetu kuwa vilaza, na matatizo ya elimu tz... anaongelea umuhimu wa kiingereza.. hii aliiongea Slaa vizuri
 
Sekondari za kata!! na matatizo ya elimu, hizi hoja ni nyepesi sana ni rahisi CCM kuandaa utetezi sbb watasema hizi ni challenge watakazokabiliana nalo watz wawape muda...attention ya wasikilizaji naona imeanza kupungua
 
Lipumba- Sekondari za kata zina lengo la kuwatenga vijana wa kitanzania ili vigogo waendelee kuwatawala,, hiizi tuhuma si sahihi sana anawapa credit CCm watazipangua kiurahisi
 
Ni prof kweli ndiyo maana nilimtwangia VEMA mwaka 2000 ila mwaka huu anisamehe chaguo langu ni Dr Slaa
 
Lipumba ansema amesoma bure shula za Mission tabora, A level Pugu enzi hizo ikiwa ni St. Fransis
jamaa alipata zawadi ya vice cancellor UD.. Yote hayo aliyapata bure.
 
jamaa anaeleza alivyofundisha uchumi mavyuo makubwa makubwa hapa duniani.....jamaa ni prof wa uchumi wa ukweli..
Alimshauri hadi kofi annan hadi uchumi!!! Du! jamaa kakata nyanga za shule si mchezo
 
anarudia anaomba kura sbb alisoma bure na anataka urais watu wasome bure....chichiM wana kazi ya kupangua hoja hizi maana za CHADEMA walisema hazitekelezeki, sasa huyu kagongelea msumari hapo hapo
 
Anaomba kura ili watoto wa masikini wasome bure kama yeye, na anakumbusha watoto wa masikini ndio walikuwa wanawaburuza wale wa matajiri...
Ubaguzi: watoto wa maskini-shule za kata
watoto wa vigogo-shule za academy
 
Akichaguliwa ataanzisha matumizi ya computer hadi primary...Hii CCm, hawwezi kuipangua sbb hata wao wameahidi, wakikanusha nitawashangaa maana wakisema haliwezekani basi na wao walitudanganya
 
ha!ha!ha!ha!ha!...... eti ukienda hospitali daktari akikushika kichwa akakuona wa moto basi ni malaria, bila kujali yeye ndo mikono yake ina joto.
 
Anazungumzia hospitali sasa... na kuanisha matatizo ya kwenye afya... so far hadi sasa Lipumba hajasema atapataje hela za kulipia Afya na elimu bure, sbb wenzao Chadema wamesema watapunguza matumizi ya serikali na kudhibiti makusanyo ya kodi....sijamsikia Lipumba ila ngoja labda atasema.. huu ni ufa asipouziba CCm watasema hapo kuwa huwezi kutoa hilo bila kodi
 
taifa lazima lihifadhi wazee wote.. wataweka utaratibu wa kupata kiinua mgongo
 
Lupumba anataja kila eneo la ilani yao, to me this is wrong move sababu anashindwa kuelezea kwa makini...ndo maana CHADEMA wao wamekomaa na makazi na kudhibiti matumizi na kukomesha ufisadi..
Here we go..aneelezea vyanzo vya mapato sasa... itakuwa wanasoma JF tu hawa,,,, just kidding!!!
 
kodi za madini, wao watadai kutoka 3% hadi 30% kwenye mikataba
watasimamia matumizi ya kodi na kukancel matumizi ya rais nje
watabana kodi kwenye mafuta, wataziba mianya
 
anachambua posho za rais, na gharama za kuiweka ile jet ya prezidaa hewani, 1hour US$6000...Anachana safari za Jk
Anamchana JK kuwa ni matonya wa kimataifa......TBC1 watasema wametuna tu!!!!
 
Lipumba- Kikwenye ni m,atonya, na rais wakiguu na njia,.. this is so good....ChichiM wanakazi kuapunga hizi hoja, watajuta kwa nini walionyesha TBC1
 
Back
Top Bottom