Kamati ya bunge yaitimua TCRA

Ludewa

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
215
37
Tetesi: habari zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa makati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma poac imekataa kuzipitisha hesabu za shirika la mamlaka ya mawasiliano TCRA kutokana na ubadhirifu mkubwa wa fedha ambao kamati imeubaini katika hesabu za shirika hilo, leo asubuhi wakati lilipopeleka hesabu zake kwa kamati hiyo ktk ofisi ndogo za bunge.

Kamati hiyo, ikiongozwa na makamu mkiti wa kamati hiyo Deo Filikunjombe, iliwajia juu, mwenyekiti wa bodi hiyo jaji mstaafu Chipeta, pamoja na uongozi wa mamlaka hiyo kwa kutumia zaidi ya tshs. 27 bilioni kinyume na taratibu za manunuzi.

Maeneo ambayo wajumbe wa kamati walihoji matumizi ni malipo ya zaidi ya tshs mil 700 yaliyofanywa na DG wa shirika hilo bila idhini ya bodi, na malipo ya usd 350 kila mwezi kwa wajumbe wa bodi kinyume na taratibu, na malipo ya tshs. Mil 600 toka vodacom kwa TCRA ambayo hayakuwemo kwenye vitabu vya shirika.

Mengine ni ujenzi wa jengo la mawasiliano towers kwa bei ambayo ni inflated toka tshs bil. 27 mpaka tshs. bil. 44 kinyume na maelekezo ya consultant aliyesema jengo hilo lisizidi bil. 27

Habari zilizopatikana hivi punde ni kwamba maafisa wa shirika hilo wamekuwa wakihaha kwenye vyombo vya habari kuwataka wasiitoe story hiyo kwenye media zao.

My take: si vema kwa mamlaka kama ya TCRA kuwarubuni newsroom ili waue stori
 
Vituo vya redio vinakamuliwa $2000 kila mwaka,kwa kila kituo.
Haya ndiyo matumizi yake?
Kuliwa na wajumbe wa Bodi?
Hizi regulatory authorities zimeshakuwa kero, zina wakamua "cuatomers" wake ili waweze kutumbua.
Zis iz too much
 
Hizi regulatories ni aina nyingine ya mashirika ya umma ambayo yamefirisi hii nchi kwa kuyapa ruzuku toka serikalini halafu yanazikamua ruzuku zile na faida hamna. Sasa serikali iko bize na kuunda hivi vi authority kila mahali halafu vinategemea ruzuku na kuwakamua wadau wa sector husika pamoja na walaji wake.

Ona hata wale sumatra sijui wale wa mafuta wanafaida gani maana yote wanayotakiwa kudhibiti hayathibitiki?
 
TCRA hawatusaidii wananchi wa kawaida.sasa hivi tigo wanatukamua na hakuna wa kutetea.
 
kuna madudu mengi kwenye taasisi hii likiwemo kuajiri wahasimu wapya pasipo kufuata kanuni za ajira za taasisi za umma...ubadhilifu ni kawaida tu ya mashirika haya
 
Regulatory bodies zife kama parastatals maana hazitufai

Inasemekana kwamba regulatory bodies Kama Ewura, Sumatra, na TCRA zinakusanya fedha Ngingo na kuzifuja vibaya, Kwa mfan Hawa TCRA mwaka jana walitumia tshs. 2.3 bil tshs eti Kwa training ya staff wao, Jambo ambalo haliwezekani Kamwe. 2.3 bil Kwa watt watatu?!?!?!
 
Mengine ni ujenzi wa jengo la mawasiliano towers kwa bei ambayo ni inflated toka tshs bil. 27 mpaka tshs. bil. 44 kinyume na maelekezo ya consultant aliyesema jengo hilo lisizidi bil. 27

Hivi jengo la Mawasiliano Towers lilimalizika lini? Na huyo consultant aliyesema gharama za ujenzi wa jengo zisiwe zaidi ya bil. 27 alizingatia mdundiko wa shilingi yetu?
 
Hii ni Authority inayoongozwa na Bodi yenye wasomi katika level ya jaji,profesa na madokta harafu inakuwa na sura ya kiwizi wizi kweli sasa tunavuna mabua.

Profesa John Nkoma hii ni aibu kwa msomi kama wewe uliyeaminiwa.Nimemuona Board Chairman anajibu kisiasa utadhani hakuwahi kuwa jaji! Kumbe mnavuta dola 350 kila mwezi utadhani waajiriwa huku posho za kila majina mnameza.Hii kweli ni sehemu ya wastaafu wenye shule zao kupumzikia.

Filkunjombe nimekukubali kwani umewatizama kwa dharau na kuwambia kamati haipitishi na special auditing ifanyike.Heshima kwa kamati yako bila kujari majina na elimu walizo nazo hawa mchwa.

Tazama Management Team yao imeundwa kiufundi na kiulaji tu.Yaani wamemdharau mtu wa Finance kabisa, atakuwaje chini kabisa eti ya boss anaitwa Director of Corporate Resource Management. Ofisi ya Wakurugenzi lukuki zaidi ya 20.Hapa kunatatizo hasa katika hizi Regulatory ambazo kwa sasa zinachangia kwa kiasi kikubwa umasikini wetu kwani their ''inputs not equal to outputs''.Shiiit.
 
Kila nikisoma mahali au kusikia jina la hii mamlaka nahisi kifafa kinaninyemelea mwenzenu. Hawana jipya ni muflisi na shimo lingine kubwa la fedha za wavuja jasho wa nchi hii. Hawana msaada wowote kwa wanaotakiwa kuwahudumia.
 
Tetesi: habari zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa makati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma poac imekataa kuzipitisha hesabu za shirika la mamlaka ya mawasiliano TCRA kutokana na ubadhirifu mkubwa wa fedha ambao kamati imeubaini katika hesabu za shirika hilo, leo asubuhi wakati lilipopeleka hesabu zake kwa kamati hiyo ktk ofisi ndogo za bunge.

Kamati hiyo, ikiongozwa na makamu mkiti wa kamati hiyo Deo Filikunjombe, iliwajia juu, mwenyekiti wa bodi hiyo jaji mstaafu Chipeta, pamoja na uongozi wa mamlaka hiyo kwa kutumia zaidi ya tshs. 27 bilioni kinyume na taratibu za manunuzi.

Maeneo ambayo wajumbe wa kamati walihoji matumizi ni malipo ya zaidi ya tshs mil 700 yaliyofanywa na DG wa shirika hilo bila idhini ya bodi, na malipo ya usd 350 kila mwezi kwa wajumbe wa bodi kinyume na taratibu, na malipo ya tshs. Mil 600 toka vodacom kwa TCRA ambayo hayakuwemo kwenye vitabu vya shirika.

Mengine ni ujenzi wa jengo la mawasiliano towers kwa bei ambayo ni inflated toka tshs bil. 27 mpaka tshs. bil. 44 kinyume na maelekezo ya consultant aliyesema jengo hilo lisizidi bil. 27

Habari zilizopatikana hivi punde ni kwamba maafisa wa shirika hilo wamekuwa wakihaha kwenye vyombo vya habari kuwataka wasiitoe story hiyo kwenye media zao.

My take: si vema kwa mamlaka kama ya TCRA kuwarubuni newsroom ili waue stori

sasa LUDOVICK UTTOH anafanya kazi gani?
 
Inasemekana kwamba regulatory bodies Kama Ewura, Sumatra, na TCRA zinakusanya fedha Ngingo na kuzifuja vibaya, Kwa mfan Hawa TCRA mwaka jana walitumia tshs. 2.3 bil tshs eti Kwa training ya staff wao, Jambo ambalo haliwezekani Kamwe. 2.3 bil Kwa watt watatu?!?!?!

No wonder serikali inadai haina pesa
 
sijaelewa hii TCRA ipo kwa ajili ya nani na kwa ajili ya nini. Maana hata ukiangalia tabu tunazopata katika mawasiliano na huduma za internet kutola kwa makampuni. Lakini TCRA hakuna wanachotusaidia tunawaandikia kero kwenye magazeti mitandaoni lakini hamana cha maana wanachotusaidia
TCRA+SUMATRA= WIZI
 
Hii ni Authority inayoongozwa na Bodi yenye wasomi katika level ya jaji,profesa na madokta harafu inakuwa na sura ya kiwizi wizi kweli sasa tunavuna mabua.

Profesa John Nkoma hii ni aibu kwa msomi kama wewe uliyeaminiwa.Nimemuona Board Chairman anajibu kisiasa utadhani hakuwahi kuwa jaji! Kumbe mnavuta dola 350 kila mwezi utadhani waajiriwa huku posho za kila majina mnameza.Hii kweli ni sehemu ya wastaafu wenye shule zao kupumzikia.

Filkunjombe nimekukubali kwani umewatizama kwa dharau na kuwambia kamati haipitishi na special auditing ifanyike.Heshima kwa kamati yako bila kujari majina na elimu walizo nazo hawa mchwa.

Tazama Management Team yao imeundwa kiufundi na kiulaji tu.Yaani wamemdharau mtu wa Finance kabisa, atakuwaje chini kabisa eti ya boss anaitwa Director of Corporate Resource Management. Ofisi ya Wakurugenzi lukuki zaidi ya 20.Hapa kunatatizo hasa katika hizi Regulatory ambazo kwa sasa zinachangia kwa kiasi kikubwa umasikini wetu kwani their ''inputs not equal to outputs''.Shiiit.

Hivi huyu ndio baba yake CARO CHIPETA aliyepelekwa ubalozini London?
 
Back
Top Bottom