Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Tarehe 21 Machi, 2024
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb) kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 amewateua Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi na Bw. Juma Hassan Reli kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi.
Wajumbe hao ni:-
1. Prof. Aloys Ntaturo Mvuma - Mjumbe
2. Dkt. Hanifa Twaha Masawe - Mjumbe
3. Dkt. Irene Charles Isaka - Mjumbe
4. Bw. Mohamed Ame Makame - Mjumbe
Aidha, uteuzi huo umeanza leo tarehe 21 Machi, 2024 kwa kipindi cha miaka mitano (5).