Kamati ya Bunge Yaishauri TAMISEMI Usimamizi wa Miradi ya Elimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI TAMISEMI USIMAMIZI WA MIRADI YA ELIMU

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeshauri Ofisi ya Rais, TAMISEMI kusimamia miradi ya elimu kwa kushirikisha wataalamu wenye taaluma kulingana na mradi husika ili kuangalia ubora wa miradi na ikamilike kwa wakati.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Londo ameyasema hayo Februari 19, 2024 kwenye ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana iliyojengwa Mkoa wa Morogoro Halmashauri ya Wilaya Morogoro Kata ya Mvuha.

Mhe. Londo amemtaka Katibu Mkuu TAMISEMI kuipatia Kamati hiyo muhtasari wa vikao vilivyofanyika vya maamuzi ya kujenga shule hiyo katika eneo hilo, kuangalia tena ubora na utekelezaji wa ujenzi na pia kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kushirikiana na wataalamu wake kuonesha tofauti ya maendeleo ya ujenzi huo.

Naye, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospeter Mtwale ameiahidi Kamati hiyo kuyafanyia kazi maelekezo na ushauri walioutoa kwa manufaa ya wananchi.

Awali, akisoma taarifa ya ujenzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Joanfaith Kataraia amesema sh.Bilioni 3 zilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya wasichana na utekelezaji umefanyika kwa kutumia force account ambapo vifaa vya ujenzi hununuliwa na Halmashauri kupitia kamati zilizoundwa na ujenzi hufanywa na mafundi walioajiriwa katika majengo mbalimbali kulingana na mikataba yao.

Hata hivyo, ameeleza changamoto mbalimbali katika ujenzi wa shule ikiwemo ya ukosefu wa maji ya kutosha katika eneo la ujenzi huku akieleza hatua zilizochukuliwa za uchimbaji wa kisima kirefu ili kuweza kukidhi mahitaji ya maji katika eneo la ujenzi na kuendelea na kazi na kwamba mradi huo ukikamilika utaweza kupanua wigo wa fursa ya wanafunzi kupata elimu.
 

Attachments

  • GGxc2L7XIAAwPDI.jpg
    GGxc2L7XIAAwPDI.jpg
    59.8 KB · Views: 1
  • GGxc2MBXgAAdGS0.jpg
    GGxc2MBXgAAdGS0.jpg
    79.9 KB · Views: 1
  • GGxc2NIWQAAutte.jpg
    GGxc2NIWQAAutte.jpg
    78.5 KB · Views: 1
  • GGxc2NFXIAAOPOr.jpg
    GGxc2NFXIAAOPOr.jpg
    72.9 KB · Views: 1
  • GGxc3jrWIAA2MX8.jpg
    GGxc3jrWIAA2MX8.jpg
    79.2 KB · Views: 1
  • GGxc3jfXMAA1rT4.jpg
    GGxc3jfXMAA1rT4.jpg
    125.2 KB · Views: 1
  • GGxc3jtWEAEEHU8.jpg
    GGxc3jtWEAEEHU8.jpg
    72.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom