Spika Tulia Ackson: Hakuna mazingira ya rushwa ndani ya Kamati za Bunge ili kupitisha maamuzi ya kamati

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Akizungumza na Dailynews digital, Dk. Tulia amezungumzia suala la rushwa kwenye kamati za bunge na kusema kuwa ufanyaji kazi wa kamati hizo hautoi mwanya wa rushwa

Wabunge hawafanyi kazi peke yao, kuna wabunge, kuna watumishi zile kamati ndivyo zinavyofanya kazi. Huwezi kusema ushughulike na mbunge mmoja ukasema hoja yako itapita kwasababu maamuzi yanayotolewa kwenye kamati ni ya wabunge wote.

Kwa maana hiyo kama unataka kutoa rushwa basi uwape wabunge wote, na kama unataka kuwapa wabunge wote, hiyo haiwezi kuwa siri na rushwa sio rahisi sana ukaifanya kwa wazi kwa sura hiyo ili uwape wabunge wote.

Na ukisema umpe mbunge mmoja haisaidii kwasababu hatasaidia kwenye maamuzi yoyote, siyo rahisi yeye mmoja akashawishi kamati kufanya maamuzi.


Bunge hili na lililopita sijaona mazingira hayo kwa maana hatujapata kesi hizo, kwamba kuna mbunge fulani kapita hapa au kule, lakini huko nyuma tulisikia kwamba yalitokea hayo mazingira kwamba labda kuna taasisi fulani imetoa rushwa

 
Back
Top Bottom