Kamati Kuu ya CCM Yaridhia Kikwete kusuka upya Baraza lake la Mawaziri

Yetu macho.Tumeshuhudia mara nyingi vilaza wakiteuliwa,tena mara nyingine hata watu wakawaida kabisa wanashangaa.Mimi binafsi nashindwa kuelewa kazi ya usalama wa taifa,kwakuwa wanapashwa kuchunguza mienendo ya viongozi wanaoteuliwa kwa umakini wa hali ya juu kabla hawajateuliwa.To me usalama wa taifa is a redundant institution.Nadhani Kikwete anadhani it's business as usual,lakini kwa jinsi hali ya taifa ilivyo sasa,he is suposed to realize that it's not business as usual,and that it's time to be serious.Taifa lina-angamia.
Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary
 
kuvunja baraza zima ni kuua nchi. Afukuze wale wezi pekee. Mambo ya kulindana mabaya sana hasa kama unaongoza nchi kichama. CAG haja ongelea baraza zima.
 
Ok na tusubri sura za mafisadi wapya tuwaone ni akina nani?? Maana wanaondoka mafisadi hawa wanaingia wengine mwendo mdundoo uwiiiiiiiiiiiiiii
CCM chukuwa chako mapema kabla ya 2015
 
bado maazimio yake hayatakuwa kama ambavyo wananchi wanataka na wangependa iwe. . maana wangali wanafanya tamthilia tu na wala haitakuwa katika halisia. maslahi binafsi yatatawala zaidi ya maslahi ya nchi
 
Kama ni golden chance kwa Kikwete itakuwa ni hii sasa. Yawezekana alikuwa anawaonea haya au kuwaogopa sasa amepewa rungu la kufagia mawaziri villaza na kuja na team nzuri itakayomletea legacy na siyo dharau baada ya kustaafu.
Namshauri kweli kama ni msikilizaji asirudishe hata mmoja kati ya wanaolaumiwa lakini hata wale ambao hawako kwenye list lakini ni vilaza nao awatimue.
Hii itakuwa fundisha na kwa wengine. ila cheo cha naibu waziri nacho hakina haja..
 
Ok na tusubri sura za mafisadi wapya tuwaone ni akina nani?? Maana wanaondoka mafisadi hawa wanaingia wengine mwendo mdundoo uwiiiiiiiiiiiiiii
CCM chukuwa chako mapema kabla ya 2015

then wakitosheka wanamwita CAG aje awaumbue kisanii,nao wanakaa pemben bila kuchukuliwa hatua z0z0te
 
Hongera Zitto Zubeir Kabwe,Kwenye Posho umeshinda na hili pia umeshinda even 2015 I believe pia utashinda!
 
bado maazimio yake hayatakuwa kama ambavyo wananchi wanataka na wangependa iwe. . maana wangali wanafanya tamthilia tu na wala haitakuwa katika halisia. maslahi binafsi yatatawala zaidi ya maslahi ya nchi

hao watatolewa,WATAKUA MABALOZ
 
kuvunja baraza zima ni kuua nchi. Afukuze wale wezi pekee. Mambo ya kulindana mabaya sana hasa kama unaongoza nchi kichama. CAG haja ongelea baraza zima.
Mkuu kinachohitajika ni kuvunja baraza zima..haina haja ya kuchukua wale nane tu..Kuna wengi tu vilaza ila zamu yao ilikuwa haijafika..
 
Kama ni golden chance kwa Kikwete itakuwa ni hii sasa. Yawezekana alikuwa anawaonea haya au kuwaogopa sasa amepewa rungu la kufagia mawaziri villaza na kuja na team nzuri itakayomletea legacy na siyo dharau baada ya kustaafu.
Namshauri kweli kama ni msikilizaji asirudishe hata mmoja kati ya wanaolaumiwa lakini hata wale ambao hawako kwenye list lakini ni vilaza nao awatimue.
Hii itakuwa fundisha na kwa wengine. ila cheo cha naibu waziri nacho hakina haja..

kikwete yupi unayemzungumzia?
 
I do not expect anything positive here. In fact we have been here and have done that! Kikwete alishalazimishwa kuvunja baraza na Bunge wakati Lowasa alipojiuzulu. Akaunda jingine. Hakukuwa na jipya. Sasa anavunja tena? Tatizo ni baraza au huyu anayeliunda na "kulivunja"?
 
Sasa utaratibu wa kurekebisha baraza la mawaziri ndio umekuwa hivi siku hizi! Haya mapyaaa sijawahi kuona
 
wakuu katiba inasemaje kuhusu waziri mkuu je baraza likivunjwa naye pia anakaa pembeni au inakuwaje hapo
 
JK ni msikivu siku zote

Kusikia tu hakutoshi. Na kuvunja baraza la mawaziri tu pia hakutoshi. Ningempa credit kama dhamira yake ingemtuma kuwawajibisha mawaziri na watendaji woote waliohusika na ubadhilifu ktk ripoti ile, na kfilisiwa mali ambazo moja kwa moja zimepaikana kutokana na ufisadi.

Mfano maige, ngeleja n.k
 
Back
Top Bottom