Kamati Kuu ya CCM Yaridhia Kikwete kusuka upya Baraza lake la Mawaziri

Problems not solved yet, I don't see who will fully be compatible to those posts, all Magamba's members of Perliament ain't capable kwasababu ya Unafiki wao. They are all the same. Old wine in an old botlle to new place:fear:
 
Sikutegema maamuzi ya kuvunja baraza la mawaziri yatatokana na kikao cha chama bali uamuzi wa rais mwenyewe kutokana na sababu zilizomridhisha yeye.

Pengine naweza sema hatua hii imedhihirhsa udhaifu wa JK zaidi kutokana na ile tabia ya kuogopa maamuzi ya CC kama ilivyotokea ktk muswada wa sheria ya Katiba mpya. JK aliwaambia wazi viongozi wa Upinzani kwamba alihofia kuchukua maamuzi tofauti na chama chake japokuwa alikubaliana na hoja zao kimsingi.

Hivyo japokuwa analivunja baraza zima lakini lengo la kina El ndio linafuata hivyo tusubiri kundi la EL ambao sasa wanajiweka ktk nafasi nzuri ya kugombea uchaguzi wa mwaka 2015.

Kifupi shamba linapaliliwa kwa maandalizi ya 2015 sio uwajibikaji kiutawala maana sheria haitafuatwa, hakuna atakaye simamishwa mahakamani wala kuhojiwa baada ya hapa, hivyo CAG haitapata majibu.. DEJAVU kama ile ya EL na kina Karamagi. Tutafungashiwa usafi ambao utakuwepo kwa muda tu kurudisha imani ya wananchi kwa chama tawala. Tujiandae na purukushani za hadaa kujivua magamba bila kutolewa meno ya sumu. Hili ndio lengo la kikao kizima cha CC ili kutufungashia kanyaboya, wananchi msidanganyike!
 
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Hii ni rekodi ya uongozi wa JK, mara 2 anavuja Cabinet kwa tuhuma za rushwa na kuweka wengine ambao wanakula zaidi kuliko wale waliowatangulia!

Taarifa inasema 'KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI' tuseme ndio kuvunja Cabinet au ataweka viraka kusubiria 2015 aende zake?
 
wakuu katiba inasemaje kuhusu waziri mkuu je baraza likivunjwa naye pia anakaa pembeni au inakuwaje hapo

The president has the option to reinstate the same PM or nominate a new one pending approval by the parliament.
 
naomba kufahamishwa maana ya baraza la mawaziri kuvunjwa. je ni pamoja na waziri mkuu kukaa kando? kama waziri mkuu haguswi naona itakuwa kazi bure. Waziri mkubwa tuliyenaye kwa sasa ni sawa na nusu ya mawaziri wabovu wote. itakuwa ni sawa na kuweka supu ya moto kwenye bakuli la baridi
 
kama kweli atateua mawaziri wapya, nashauri wahakikiwe mali zao kabla ya kuanza kazi na ziwekwe hadharani kila mtu ajue anamiliki mali ya kiasi gani, ili hapo baadae iwe rahisi kumjua waziri fisadi. Isije kuja waziri hapo baadae anasema lorry lake linamwingizia dollar elfu 20 kwa mwezi wakati anachota za walipa kodi.
 
kuvunja balaza kutaipa heshima kidogo CCM,na itakuwa fundisho kwa mawaziri watakaobaki na wapya.Watanzania tusikubali kufanywa mambumbumbu, wasipolivunja Balaza au kuwawajibisha mawaziri wenye tuhuma, 2015 tuwawajibishe CCM kwa kura zetu.
 
Swala kwangu si kuvunjwa bali ni nani atateuliwa baada ya hapo na isijekuwa bandika bandua ya kuweka marafiki zetu au wasiokuwa na uwezo.
 
Clouds Tv na Channel 5 si sehemu sahihi ya kuchomoa na kujiaminisha kwa hizi taarifa. Kama vyanzo ni hivyo, mie bado nasubiri kuskia, siamini vyanzo vyenu. Hao saizi yao ni Wema Sepetu na Lulu, huku kwingine sio levo zao
 
Back
Top Bottom