Kahororo secondary school - mpo humu ?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Jitokezeni mlopitia Kahororo ili tupange mikakati ya kuiboresha shule yetu. Wengi nakutana nanyi mijini ila hapa siwezi jua nani na yupi na natumia jina lipi. Nasubiri majibu yenu
 
Kahororian tupo tupo tupo, na tutaendelea kewepo; wapi tukutane walau tujikumbushe vitu kama Nshobyo(kijiko), Enyuka(new comer-form one), Jangili road(nyuma ya bweni la mapinduzi), Karege(uji usiokuwa na sukari), khohikhohi, Enkura, kitanta na uncooked beans(harage lisilo hiva)
 
Jitokezeni mlopitia Kahororo ili tupange mikakati ya kuiboresha shule yetu. Wengi nakutana nanyi mijini ila hapa siwezi jua nani na yupi na natumia jina lipi. Nasubiri majibu yenu

Wanakahororo aka Ishamii mpooooo.Je ule mlori wenu wa Izusu bado upo au umeisha uzwa?teeeehhh
 
kahororo hamjambo jamani? Mimi nlikuwa nakuja pale kahororo kwenye ukwata. watu wengi wa Bukuba wanapafahamu pale kahororo. wanafunzi wa Kahororo mida ya kuanzia saa moja jioni unawakuta pale kashai wakila viazi vitamu kwa uji. siku za mechi unawakuta pale kwa mpemba kashai barabara ya kwenda kahororo. Kahororo, nyakato na omumwani wote sawa tu coz shule zenu zipo ulokoni japo mnajiita wa bukoba mjini.
 
Dubu vipi? Bukuba ndo wapi wengine Geography inatupiga chenga alafu sio wenyeji wa Bukuba! Ila sawa Kahororo, Nyakato na Omumwani ni za Ulokoni (Local/suburb location
 
Jamani wana kahororo secondary, hali ya hii shule si nzuri hata kidogo kwa sasa, mimi nimemalizia pale kidato cha sita mwaka huu, lakini ufaulu wake ni wa chini sana, walimu wamekuwa si wa kuzingatia kuingia katika vipindi vyao, kiasi kwamba inapita hata mwezi mzima mwalimu hajaingia class, sababu hamna, kaamua tu!
Hii imewatokea hasa wanafunzi wenzetu wa masomo ya sayansi(pcm) na kusababisha kufeli kwao.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom