Leseni ya Utumiaji wa bidhaa zitokanazo na mmea wa Bangi

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,128
12,216
Salaam wakuu.

Natumai wote mpo salama na mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida.

Nina swali ambalo pengine naweza pata majibu hapa,

Mmea wa Bangi unatumika kama dawa kwa baadhi ya watu na wengine wanautumia kwa dhumuni la kujistarehesha kihisia si ndivyo?
Sasa maswali yangu ni haya na Chini nitaweka hoja zangu binafsi sipendi kuwa msemaji wa wengine.

1. Kwanini Mmea huu umewekwa kwenye orodha ya Madawa ya kulevya?
2. Madhara yatokanayo na Bangi ni Makubwa kulinganisha na yale yatokanayo na Matumizi ya tumbaku na pombe kali?
3. Je Bangi ni kwa ajili ya watu Maalum tu?
4. Kwa wale watu wa Imani ( Dini ) je Bangi imezungumziwa popote kwamba imekharamishwa watu wasiitumie na wakiitumia watakuwa wametenda dhambi? Na adhabu yake ni ipi?

Hoja zangu kuhusu mmea huu kuomba( natumia kauli kuomba ) uhalalishwe ni hizi hapa.

1. Kama bange ina madhara kwa njia ya kuvuta, ( moshi wake ) basi itafutwe namna iwekwe katika hali ya kimiminika mfano wa ( beer ama juice ) watu waendelea kupata kile kitu roho inapenda kwa njia zingine tofauti na hivyo ya kuvuta( jina la wavuta Bangi linatokana na hilo tendo la kuvuta ) na badala yake iwe watumiaji wa bidhaa zitokanazo na mmea wa Bangi.

2. Watumiaji wa Bidhaa hii ni wengi, wengi mno, kwanini usiwekwe utaratibu maalumu kama kuwasajili watumiaji wa bidhaa hii na wakapewa leseni maalum ama wakapatiwa maeneo maalum ( smoking area ) na wakawa wanalipa kodi na kuiongezea Mapato Serikali?

3. Viwepo viwanda vya usindikaji ama mashamba maalumu, ama vyuo ambavyo vingefanya tafiti mpya kulinganisha madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za tumbaku na utumiaji wa bidhaa za Bangi, na Utumiaji wa Pombe.

4. Bangi ni Tiba, baadhi ya nchi duniani wamejiwekea utaratibu fulani kuhusu utumiaji wa mmea huu, na hawapo nyuma kimaendeleo, kama ishu ni kujifunza kwanini tusiingie chimbo na sisi kufanya uchunguzi kwanini hawa wameamua kuruhusu japo kiwango fulani cha matumizi kwa raia wake? Je hawa hawajui madhara yatokanayo na Bangi mpaka wairuhusu?

5 Tumekuwa tukiangalia Madhara tu, vipi kuhusu faida zake?
6. Kama kwako haifai kuna wale ambao ina faida kwao je wanafikiriwaje? Waharifu?
6. Mtu ambaye amekaa nje kwake anatumia mmea wake bila bughudha na yule ambae amekunywa pombe bar na kuanzisha fujo yupi ni mhalifu?
7. Bangi ni mmea wa Asili ambao ulikuwepo tangu na tangu yaani tangu historia ya dunia inaanza na inasemekana hata binaadam wale wa mwanzo mwanzo walikuwa wakiitumia, je na wao ni nani alikuwa akiikataza wasitumie?
8. Rizla zina kazi gani madukani? Sababu gozo huwezi vutia.
9. Sigara na Bangi ipi ina madhara?
10. Ni Suala la kiimani zaidi, zipo imani( dini ) ambazo bangi inahusika katika kumfanya muumini wa imani hiyo kuwa karibu na kile anachokiamini kiroho, je hawa wamezingatiwa? Ukizingatia kwamba Serikali ipo kwa ajili ya watu wote na ndio msimamizi wa wote na haina dini? Vipi kuhusu hawa?

Pia mtu anakunywa Pombe ili apate nini?
Anayevuta sigara anataka apate nini?

Kwanini Bangi?

Tunaomna kama upo uwezekano wa kupata vibali Maalumu watu wakaweza kutumia mmea huu hata kama ni kwa sehemu maalumu ifanyike hivyo sababu wengine imani zetu huo mmea ni connection kati ya ulimwengu wa roho na huu wa mwili, kukataza kuutumia ni kuingilia imani za wengine.
Bangi ni mmea wa asili ukilinganisha na Vilevi vingine ambavyo vinapitia maabara ama vinaongezwa kemikali,
Tukubaliane kwa pamoja.


Umeshawahi kuona mtu amepata ajali kwa kuwa ametumia Bangi? Pombe je?
Kwanini wana philosofia wengi na wana sayansi waliokuwa wakitumia Mmea pendwa wa Bangi kazi zao zipo hai mpaka leo hii?
Kwa hoja hizi chache, najua wengi wana mawazo yao pia kuhusu hili, ingetaftwa mamna ya kutufikiria sisi ambao imani yetu Bangi ni Connection kati yetu na Uumbaji tukapatiwa japo vibali maalumu ili ibada zetu ziweze kuwa kamilifu.

Si vizuri kumuhukumu mtu kutokana na imani yake, muhukumu kitokana na matendo yake.

Nguvu za kiroho zinapungua siku baada ya siku kutokana na huu mmea kuzidi kuandamwa na tunakuwa watu wa hovyo kabisa sababu connection kati yetu na ulimwengu inapigwa Ban. Sisi tunaamini katika Asili.
 
Ni utamaduni tu ni kama ilivyo kuna jamii zinakula kambale na nyingine hazili kambale.

Ila hata ukiangalia tumbaku, vifo vitokanavyo n matumizi ya tumbaku ni vichache kuliko vifo vitokanavyo na ajali za bara barani ila bado madhara ya tumbaku ni ya msisitizo zaidi sababu tunahitaji taifa hai.
 
Watu wa conspirancy theories watanielewa, dunia inaendeshwa na kikundi cha majangili wachache ndo mana bangi marufuku ila sigara unaipata popote kwa mangi, pombe asili marufuku ila chibuku na k vanga unanunua duka la jirani..

na wanatuendesha kwa kutumia mfumo wa riba (interest), tajiri atajirike maskin ataendelea kuchumia juani!

Uzuri ni kwamba capitalism is collapsing as we speak, dunia itaji reset, cannabis is natural.. u cant fight nature, baadhi ya nchi za kiafrika kama zimbabwe, uganda wameruhusu kilimo cha bangi.
 
Watu wa conspirancy theories watanielewa, dunia inaendeshwa na kikundi cha majangili wachache ndo mana bangi marufuku ila sigara unaipata popote kwa mangi, pombe asili marufuku ila chibuku na k vanga unanunua duka la jirani..

na wanatuendesha kwa kutumia mfumo wa riba (interest), tajiri atajirike maskin ataendelea kuchumia juani!

Uzuri ni kwamba capitalism is collapsing as we speak, dunia itaji reset, cannabis is natural.. u cant fight nature, baadhi ya nchi za kiafrika kama zimbabwe, uganda wameruhusu kilimo cha bangi.
Hawa jamaa sio wanafanya ile ya medication au hata recretional poa tu?
 
Hapa hapa Bongo maeneo ya washua Kuna secret weed cafés, weed shakes, cookies n.k.
Na bei zimechangamka somehow.
Probably hawataki kuhalalisha ili wajinga wajinga wasio na a wala be wasije wakafa kwa kukosa control.
 
Hapa hapa Bongo maeneo ya washua Kuna secret weed cafés, weed shakes, cookies n.k.
Na bei zimechangamka somehow.
Probably hawataki kuhalalisha ili wajinga wajinga wasio na a wala be wasije wakafa kwa kukosa control.

Sent from my Pixel 4 XL using JamiiForums mobile app
Ofkoz hii lazima tu, mana kuna maeneo ukipita...inapulizwa kama fegi na wazee pia wamoo humohumo yani mmeaa ungeruhusiwa tu ulipiwe kodi basi
 
nchi za kiafrika zinaruhusu kwa biashara tu tu, mainly exportation.. recreation bado
Hapa kipindi hiki cha ugumu huu, wangepata source ingine ya kodi. Hivi Kenya pale si inauzwa nje kama kawa? Yani wana-export?
 
88cd511b75bc9e2fcbda61821cb0a50b.jpg
 
Back
Top Bottom