HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Juzi nilikwenda mapumziko Tanga baada ya kuchoshwa na shughuli zangu za kikazi za wikii nzima na foleni za hapa Bongo zisizo na tija! Nikiwa TA nilipata wasaa wa kumtembelea kwa mara nyingine rafiki yangu mpendwa ambaye mwaka juzi alifiwa na mkewe.
Kabla ya kufariki kwa mkewe, kaka huyu alikuwa akiishi na mdada wa kazi ambaye ki umri hakupishana kabisa na mkewe. Dada huyu ambaye nilifanikiwa kumuona mara kadhaa kila nimtembeleapo rafiki yangu ni mpole mtaratibu na mwenye tabia njema.
Katika mazungumzo yake, mkuu alinidokeza kuwa ameamua kufunga ndoa na msichana huyu kwa sababu amemsaidia sana tangu mkewe alipofarikia na hata watoto wawili walioachwa na marehemu, amekuwa akiwatunza na kuwahudumia kana kwamba ni watoto wa kuzaa mwenyewe.
Nilipomuuliza kama alikuwa na mahusiano hapo kabla ya mkewe kufariki, alikana kabisa kuwa hakuwahi kufanya hako kamchezo ila kwa sasa focus yake ni nani hasa anafaa kuwatunza watoto wake. Ndugu zake wamekuja juu kupinga uamuzi wake na sasa ameamu kuomba ushauri kutoka kwangu.
Wadau naomba ushauri nimshauri nini kaka huyu.
Wenu,
HP