Aliniacha na kejeli juu lakini sikumchukia

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Japo uliniacha lakini haikumaanisha nilitakiwa kukuchukia.

Miaka saba iliyopita nilizama kwenye penzi la huyu msichana X aliyekuwa anasoma pale shule moja ya vipaji (wanawake tupu) jijini Dar es Salaam na wakati natoka naye alikuwa kanipita darasa mmoja.

Uzuri wake hauna mfano kwa kweli na mpaka leo hii bado sijapata mwanamke mrembo kama X, maana yake siyo kwa umbo lile, alirithi shape ya mama yake. Kama kashushwa toka mbinguni, mwili fulani hivi wa umbo namba nane kama Sanchoka au Poshy Queen. Rangi yake kama Rihanna hivi, akicheka sasa kama kweli mwanaume ni mzima basi lazima, mjegeje wote unasoma 5G+.

Bila kusahau zile za "Staki bwanaa, nache huko", suti flani hivi nzuri sana kama ya Wema Sepetu akilalamika. Hivi ushawahi kumsikia Wema Sepetu akilalamika, alooo!

Utajikuta suruali inaanza kulowana taratibu! Mshike kiuno sasa uone anavyoruka mita sita, aisee! Mungu alijua kuumba kiumbe chake, hakika Mwenyezi anastahili sifa za ufundi wake wa kipekee.

Nilipitia wakati mgumu sana nakumbuka ndiyo lilikuwa penzi langu la kwanza. Siwezi kuficha, mambo mengi alinifundisha huyu mwanamke japo tulikuwa dini tofauti, ila mwana nilizama na ndoto zangu siku moja nije kumuoa.

Hata sijui nilikuwa nawaza nini, X alikuwa kicheche sana, alifikia hatua alitembea mpaka na mume wa mtu ambaye mkewe anamuita rafiki (dada) na wakina mama mtaani walikuwa wanamsema sana. Miongoni mwa hao wamama ni mama yangu, ila kumsema kwake hakukubadilisha upendo wangu kwake.

X kuwa kicheche nadhani ilisababishwa na hali ya kimaisha ya kwao na tamaa za kike. Ilifikia hatua mpaka X alitembea na marafiki zangu wa mtaani na wale makaka walionizidi umri. niliamini kuwa walionizidi umri nitawapindua kwa vile kipindi kile nilikuwa mpole sana.

Lakini upole haukusaidia kitu, ndiyo nilieelewa kuwa upole hauna faida dunia ya leo zaidi tu utaonewa, na makaka walikuwa wavuta nganja sana lakini upole wangu haukusaidia kitu. X alichukuliwa mbele ya macho yangu naona.

Nakumbuka ile siku ya harusi dada yake X anaolewa napita kichororoni naenda kwao, nikakuta kanabanwa kichochoroni halafu naye kalegea kwa mahaba ya yule kaka muhuni.

Nikapita kama sijamuona baadae nikasikia maneno kutoka kwa rafiki zake wale makaka kuwa, X kaenda kuliwa tunda kimakusudi. Licha ya hivyo bado haikubadilisha kitu, bado niliendelea kumpenda tu.

Alinibadilisha pale aliponifungulia mdomo kwa kuniambia hataki kudate na watoto wa O-Level. Iliniuma sana ile kauli yake ila nikajikaza na sikuwahi kumchukia mpaka leo hii bado nampenda, lakini haina maana kama nitakubali kutoka naye tena.

Maisha yaliendelea kila moja akapotelea kwake, X alikuwa jirani yetu lakini wazazi wake walikuwa wamepanga tu nyumba ya jirani, na mimi baada ya kumaliza elimu yangu ya O-Level nikaondoka nyumbani nikaenda kuishi kwa baba mdogo. nikasikia X ana mtoto lakini sikubahatika kumuona huyo mtoto wake.

Kuna siku nilienda kutembea kwa wazazi wangu nikaonana na X, alikuja kwa bashasha na tabasamu na akanikumbatia. Natamani ile siku ijirudie tena, sikuonesha ushirikiano wa tabasamu lake kabisa yaani. Japo tulipiga stori za hapa na pale lakini hakugusia kuwa ana mtoto na mimi sikumuuliza swala la mtoto.

Siku zikaenda wakina X wakahama, wakahamia nyumba ambayo kajenga baba yake. Kwahiyo nikawa nikienda kwa baba sina matumaini ya kumuona X tena, maana mama aliniambia wakina X wamehama ila hawakuaga kwahiyo mama hakujua wakina X wamehamia wapi!

Siku moja nipo katika harakati zangu hapo mfukoni nina kama laki 1 na elfu 30 hivi, katika pita pita zangu barabarani nikakutana na X. Kimuonekano hakuwa mrembo kama kipindi kile, inawazekana ilitokana na kulea na hali ya maisha. Alikuwa akiwa anauza sabuni chini pale rangi 3 akiwa na mtoto mgongoni. Nilitaka kumpita ili asinione lakini haikuwa hivyo, aliniona na tukaonana macho kwa macho.

Kosa la pili sikutaka hata maongezi naye nilimuacha pale pale akilia machozi yalimtoka sana, lakini haikubadilisha kitu. Nilivyofika nyumbani sikuwa na amani ya nafsi hata kidogo, siku ya pili nilienda eneo lile lile nikiwa na elfu 90, kuna dogo alikuwa anauza maji ya kandolo nilimuita nikamwambia nipe maji akanipa nikampa pesa yake.

Kisha nikamwambia hii pesa mpelekee yule dada X. Nakumbuka yule dogo alienda lakini wakati anaenda na mimi nilikuwa nahama eneo, kiufupi nilihitaji tu kuona pesa ikimfikia lakini sikuhitaji ajue kama mimi ndiyo nimempa. Nilimuona yule dogo kafika kampa pesa X, kama waliongea ongea hivi.

Akataka kuonesha kuwa aliyenipa yule pale lakini wakati anataka kumuonesha muda ule mimi nilikuwa nishasogea pale kwahiyo nina uhakika hakujua nani katoa pesa ile. Tokea siku ile mpaka leo hii sikubahatika kumuona tena X.

Kuna kipindi cha kati nilipoteza line ya simu sasa juzi nilipata kuwasiliana na rafiki tukabadilishana namba, sasa leo hii nikasema acha nimecheck jamaa.

Leo hii asubuhi kuna rafiki yangu ananipa taarifa kuwa X kashafariki, tena kafariki zamani tu tokea miezi minne iliyopita nyuma. Chanzo cha kifo chake familia yake hawakukitaja, walisema kaumwa tu lakini kabla ya kufa afya ya X haikuwa sawa, alikuwa kachoka sana.

Nilibakia kuganda tu huku nikitamani siku zirudi nyuma nijue nini kilimsibu mpaka akashindwa kuendelea na masomo yake ya A-Level.

R.I.P "X"
 
Japo uliniacha lakini haikumaanisha nilitakiwa kukuchukia .

Miaka saba iliyopita nilizama kwenye penzi la huyu msichana X aliyekuwa anasoma pale Shule moja ya vipaji (Wanawake tupu ) jiji Dar es Salaam na wakati na date nae alikuwa kanipita darasa mmoja.
Script ni ile ile. Katika kilele cha usichana x anazingua halafu baada ya miaka michache mbele unakutana naye keshachoka balaa halafu mwanaume ndo hela zimekubali na huna hamu naye tena maana uko level za juu.

Huwa najiuliza kwani ukimsaidia tu kama binadamu mwenzio kama uwezo unaruhusu utapungukiwa na nini? Inafurahisha sana kwamba angalau ulimpa hizo 90K. Huo ndiyo ubinadamu sasa na bila shaka utabarikiwa sana (kama siyo chai) 😁

RIP X wa Ally Nassor 🙏🏿🙏🏿
 
Back
Top Bottom