Novel: The Cruel Existence!

Writter

Member
Jun 22, 2022
39
148
Haki zote zimehifadhiwa Ni marufuku kucopy, kunakili, kuhariri wala kutumia sehemu ya kisa hiki popote bila ridhaa ya mwandishi.

Tabaruku kwa
"kila anayeamini siku mpya ni Zawadi.

Shukrani.
mtakaofuatilia
Sitawaacha njiani.

SEHEMU YA 1


Baada ya majibizano ya muda mrefu Dr Richard alizidi kupandwa na hasira na uso wake kuzidi kua mwekundu kutokana na mazungumzo ya muda mrefu yasiyo na suluhu, Hasira zilimkaba na kujikuta akimnasa vibao vikali usoni Mke wake Bi Laura ambaye naye alirudi nyuma ya mlango na kuokota Fagio na kumrushia Dr Richard na hapo likaamsha hisia za hasira kali ambapo Dr alimrukia tena mke wake kwa magumi ya kila mahali, Bi Laura hakubaki kinyonge aliendelea kulipiza kwa mateke na chumba chao kikageuka ulingo wa ngumi na vile walikua wenyewe nyumbani hakuna ambaye angewaamua.

Waliendelea kupigana kwa zaidi ya Dakika saba wakati Bi Laura akipokea ngumi nzito za usoni na hakuacha kupiga kelele na kurusha mateke kuomba msaada lakini kwa ukubwa nyumba ile kelele ziliishia barazani tu na baada ya ngumi kuendelea kuumiza sana uso wake bi laura aliinua kichwa na kumg'ata mumewe vikali kwenye bega. Maumivu ya meno begani yalimtoa haraka pembeni Richard na kumpa upenyo mkewe ambaye alitoka kwa kasi ya ajabu kuelekea nje ya nyumba.

Baada ya dakika 3 Dr Richard akiendelea kusikia maumivu makali began alisikia mngurumo wa gari yao ndogo nje ikitoka na akaamka akichechemea na kukuta mkewe akifungua geti tayari kuondoka, Dr Richard alirudi ndani haraka na kuchukua funguo za gari nyingine ili kumfuata mkewe asijue ni wapi anaelekea. Baada ya gari ya Bi Laura kushika njia kuu kwa kasi Dr Richard alikumbuka hakufunga geti wala mlango ilibidi asimame kwanza na kurudi kufunga geti na mlango na mara akawaza ya nini kumkimbiza? Akatazama saa yake ni usiku wa karibia saa tano kasoro. Utulivu wa giza la nje na kelele za ndege na chura ukamfanya akatulia na kuwaza cha kufanya.

Akiwa kwenye usukani wa gari Richard aliamua kuelekea polis kutoa taarifa juu ya kupotea kwa mke wake baada ya ugomvi wa siku mzima, lakini pia akawaza kumpigia simu mwanao mkubwa Adam lakini akaona hapana, Mwisho akawasha gari kuelekea mitaa anapoishi kaka yake Mkewe yaani Shemeji yake ili amweleze kilichotokea na kwa pamoja wakubaliane cha kufanya.

Mida ya saa tano na nusu usiku Richard alipiga honi ya gari kwenye geti la Shemeji yake Allen na mlinzi alifungua geti kwa mshtuko mkubwa Richard alishangaa kuona gari aliloondoka nalo mkewe likiwa kwenye parking ya magari ya Allen, hasira zilimjaa upya na ghadhabu ya kuwaza mkewe baada ya yote kakimbilia kwa Allen. Richard alifunga mlango kwa nguvu na kwa kasi ya ajabu akiingia bila hodi kwenye mlango wa nyumba ya Allen na kuanza kushout tena kwa hasira

"Laura what are you doing here? Aliuliza kwa hasira na sauti yenye mkwaruzo mkali

"Calm Down Richard, She's my sister and this is my home place. Allen naye alijibu kwa kiburi

Sijali kuhusu hapa ni kwako au vip huyo ni mke wangu nahitaji kuondoka naye sasa hivi. Please Allen nakuheshimu naomba niheshimu pia.

Sitaki nasema Sitaki sirudi nyumbani Laura naye alipaza sauti kwa hasira.

Dr Richard alishuka kidogo akaketi kwenye kochi na kumtazama Allen na kumuomba Allen kwa mara nyingime kwamba wao ni watu wazima sana na yeye na mkewe wana mambo ya kuweka sawa kabla hapajakucha anaomba na kumsihi sana aondoke na mkewe wakazungumze halafu asubuhi watampatia mrejesho. Richard alimueleza Allen bado hawajashindwana na hawapo tayari kusema kinachowasumbua ila anaomba sana wakajaribu kuongea kwa mara ya mwisho.

Lakini shida ni nini? Aliuliza Allen kwa upole, Richard na Laura walitazamana na hakuna aliyekua tayari kusema shida ni nini.

Laura alianza kutoka machozi na kumwangalia kaka yake na kusema ataniuwa namuogopa "He's going to kill me, I'm not ready to die now" please help me Allen I knew him very well. My kids are everything to me, I don't want to leave them alone, Laura alizidi kulia sana.

Kiumri Allen ni mdogo kwa Laura kwa zaidi ya miaka 5, ingawa Laura anapenda kumuita Allen kaka kwa sababu ndiye mdogo wake wa pekee, Lakini kwa Richard Allen ni mdogo sana, Richard ni mtu mzima anayekaribia kustaafu akiwa na 57 lakini Allen ni kijana wa miaka 34 tu karibu ni kijana wa kwanza wa Dr Richard lakini kutokana na pilika za maisha Allen ni mpambanaji aliyefanikiwa tofauti na umri wake ni mtu asiye na uoga wowote na ni msaada mkubwa sana kwa dada yake Laura kila wakati.

Allen alinyanyuka na kutoka nje na Richard

Listen Richard " Nampenda dada yangu kuliko chochote unajua kwa nini kakimbilia kwangu? Lolote litakalomtokea ni ama zangu ama zako sitajali kuhusu umri wako wala uwezo wako wala ushemeji wetu nitakutia misumari ya macho, na kukata kata mwili wako kwa vipande vya nusu kilo na kukuteketeza kwenye uso wa dunia ndani ya dakika 10. Sisi ni familia kama kuna shida tunahitaji kutafuta suluhu sio kuzozana.

Richard alimtazama Allen kama nyanya mbichi tu wala hakuogopa chochote alimsogelea machoni na kumwambia Allen,Ndio Laura ni dada yako mimi ni mzazi mwenzangu naomba kuondoka na mke wangu kabla hii vita haijawa kati ya mimi na wewe.

Allen hakujibu chochote aliingia ndani moja kwa moja mpaka chumbani kwake akafungua begi moja lililokua katikati ya mabegi mengi akatoa simu yenye Line iliyosajiliwa kisha akaingia kwenye tool box na kutoa bastola moja na kuweka risasi tatu na kurudi sebuleni alipokua ameketi laura akiendelea kulia.

"Nenda Naye lakini akiendeleza ushenzi mpasue ya kichwa kisha nipigie simu kwa namba hii nitakupa maelekezo usitumie namba yako.

Lakini kaka.....alisema Laura lakini kabla hajamaliza Allen akamwambia nenda kwenye gari mfuate.

Acha gari yako hapa hapa!

Laura alifungua mlango wa gari alipokua ameketi Richard, alificha bastola na simu aliyopatiwa na Allen ndani ya sidiria na kujifunga na mtandio bila kuonyesha wasiwasi.

Richard aliwasha gari bila kusema chochote wala kumuaga Allen njia ya kuelekea nyumbani ukimya ukitawala, upepo wa usiku vilitawala matone na ukungu wa umande vikiendelea kukaribisha giza kuu la saa sita usiku, wakati mawazo yakizidi kugonga vichwa Richard asijue Laura anawaza nini na Laura asijue Richard anawaza nini ni utulivu na ngurumo ya engine ya gari tu wakielekea nyumbani.

Haikuchukua dakika 20 Richard alipark gari getini kwao na kushuka kwa ajili ya kufungua mlango, ndani ya gari laura wasiwasi ulizidi kumjaa na kuendelea kurekebisha Nguo yake vizuri ili bastola yake isionekane

Waliingia ndani na baada ya kufunga milango laura alielekea moja kwa moja chumbani akatoa bastola na simu akaweka kwenye tenga la nguo changu na kupanda kitandani na Richard alinyooka moja kwa moja kwenye fridge na kujipimia shots tatu za John Walker kisha akainywa yote kwa mara moja na kunguruma kwa uchungu kisha akaelekea chumbani kwa sauti ya hasira Richard alianzisha tena

"Laura naomba kukuuliza kwa mara ya mwisho, Arnold ni mtoto wa nani???

He's not your fucking Son Richard

Laura alilipuka kwa hasira na kupoteza utulivu uliokuwepo mwanzoni.

Richard kwa kushindwa kuvumilia hasira alimvaa tena Laura na akili ya Laura ilikua tayari kwa chochote, Roho ya kifo ilikua tayari mikononi mwake, hakutaka aibu mbele ya dunia akiwa anaona ni bora mwili wake usemwe kwenye jeneza ukiwa mfu kuliko dhihaka za ndugu na jamaa kuhusu usaliti.

Kwa miaka 25 tangu kuzaliwa kwa mwanao wa pili Anold, Richard alijua Arnold ni mtoto wao lakini haikua hivyo kwa historia ya Anold katika familia hiyo ndio chanzo cha Richard kuzidi kupandwa na hasira na kwa mara ya kwanza aliona kumuacha Laura sio suluhu zaidi ya kumuulia pale ndani na yeye kujipeleka magereza usiku huo, hakutaka mahakaman wala police.

Akili ya Richard ilikua tayari kwa ajili ya kumuua mwanamke huyu aliyesimama mbele yake, hakumuona tena kama mke wake wenye watoto 3 na wapo katika kipindi cha kula matunda waliyochuma tangu ujana wao. Laura na yeye aliona ashapata ruhusa kutoka kwa kaka yake wa pekee kwa ajili ya kumuua mwanaume huyu. Hakujali tena kuhusu watoto wao kubaki yatima wala kuta za magereza kwa sababu alishajua Allen yupo.

Kwa nguvu ya ajabu Laura alijichomoa kitandani na kuzama ndani ya tenga la nguo na ile kutoka tu tayari yupo bastola aliyopewa na Allen, kwa kupanic bila kuangalia alipo Richard, Laura alifyatua risasi ambayo ilimkosa Richard na kupiga ukutani wakati Laura anakoki ili kufyatua risasi nyingine Richard naye hakua na cha kuogopa alijirusha mikononi kwa Laura na wakati laura anafyatua risasi ile mikono yake ilikua tayari imeyumbishwa kwenda chini na kufanya risasi ile kujipiga kwenye Paja la kulia la mguu wa Laura.

Laura alipiga kelele ya nguvu na kuanguka chini na kupoteza fahamu hapo hapo wakati damu zikiendelea kuvuja kwa kasi ya ajabu, sasa akili za Dr Richard zilianza kurejea na kutaka kumaliza jambo hilo ila kutoka kwenye hisia za kawaida alishindwa kuelewa bastola ile imetokea wapi na imekuaje imempiga Laura kwenye paja, Roho ya kifo na uoga ilikua imetanda ndani ya nyumba ilianza kufifia baada ya kuona Laura yupo chini na damu zikivuja. Mawazo ya kuta za Magereza yalimjia Dr Richard kwa ghafla biashara zake na binti wake wa pekee Nancy zilibeba kichwa chake, urafiki wa watoto na mama yao aliyelala kimya sakafuni vilianza kuzunguka Dr Richard.

Amesaliti, yafaa afe...bora afe tu. Alijisemea Dr Richard Hakutaka kwenda magereza ila alitaka kutatua haraka hali hiyo kabla hapajakucha saa ilisema ni saa nane kasoro usiku tulivu Dr Richard aliona bado ana muda wa kufanya jambo..

****

Allen alipoteza amani na utulivu wote aliokua nao baada ya kumuona dada yake Laura akilia, sura ya dada yake ni mfano halisi wa uso wa mama yake na kwa hivyo hapendi kumuona laura analia ni sawa na kutizama mama yake akilia, hasira za machozi ya dada yake ilimlazimu kufanya maamuzi yoyote ili dada yake apate furaha hakuogopa kumvunjia heshima Shemeji yeke Richard lakini baada ya gari ya Richard kuondoka aliwaza kuhusu kitendo cha kumpatia dada yake bastola kwa ajili ya kumuua Richard

Adam ni mtoto wa kwanza wa Dr Richard ambaye ni rafiki mkubwa sana wa Allen ingawa Adam ni mtoto wa mama mwingine ambaye sio dada yake Laura ila mara zote Adam huzungumza na Allen kwa jinsi baba yao mbali na ukorofi alionao ni baba rafiki na aliyepambana sana kuanzia utoto wao ili wapate maisha waliyoyatamani.

Roho ya Allen ilianza kumsuta kuona amemkabithi dada yake bastola kwenda kumuuwa baba wa rafiki zake Adam, Arnold na Nancy bila kujua kosa ni nini na pia mume wa dada yake Laura na hata yeye Allen anaujua mchango wa Dr Richard mara kadhaa kwenye mishe zake.

Allen alitoka alipokaa na kuwasha gari yake chap kuwahi nyumbani kwa Laura ili kujaribu kuzuia mauaji hayo kama inawezekana, kwa kua ilikua ni usiku barabara ilikua ni nyeupe bila magari alitumia dakika chache sana kufika nyumbani kwa Dr Richard

Wakati Allen amefika getini kwa Dr Richard kabla hajapiga honi ya gari alisikia mlio mkali wa kwanza wa Bastola ndani ya nyumba ya Richard kabla hajawaza cha kufanya akasikia mlio wa pili uliotawaliwa na utulivu wa muda, giza likatanda machoni kwa Allen mikono ikatetemeka kwa jasho hofu ikamjaa na kugundua kufika wa kwanza eneo la tukio ambalo fika anajua ni mauaji aliona kizunguzungu na kuamua kugeuza gari haraka na kurudi alipotoka.

Kabla hajafika mbali nguvu zilimuishia aliamua kupaki gari pembeni akitetemeka jasho lilikua likimtoka akijua ni dhahiri Laura kabeba ushauri wake na kuwatia kwenye uyatima wa makusudi vijana watatu. Alijuta kwa nini alitoa bastola baada tu ya kuona dada yake kaumizwa bila kujua chanzo cha ugomvi ule.

Baada ya dakika kumi za kustaajabu pale ghafla gari ya Dr Richard ilimpita kwa speed ya ajabu na bila kuwaza mara mbili kwa kuendelea kuogopa ushahidi wa tukio hilo Allen aliamua kuifuata gari ya Dr Richard taratibu bila kufahamu linaelekea wapi na nani anaendesha.

Baada ya mwendo wa dakika 20 gari ile ilipark pembeni ya kichaka kidogo nje ya mji eneo ambalo ni maarufu kwa uhalifu kwa mbali Allen alishuhudia Dr Richard akishuka haraka kwenye gari na baada ya dakika zisizozidi 5 alifungua bonnet ya nyuma ya gari na kutoa kitu kilichofungwa kwenye kiroba na kukutupa kichakani kisha gari liliondoka kwa speed kubwa.

Jasho lililowesha tshet aliyokua Amevaa Allen na ujasir wa hali ya juu ulimvaa alikanyaga mafuta kwa nguvu na kusogelea mahali kulipotupwa kiroba akiamini ni mwili wa dada yake bila kupoteza muda alibeba kiroba kile na kuweka kwenye seat ya nyuma ya gari yake na kugeuza gari kwa ukali kuelekea nyumbani kwa Dr Richard, alitaka kwenda kufanya tukio lake, huruma juu ya vijana wa Dr Richard kubaki yatima ilipotea urafiki wake na Adam na Anold ulikua sio chochote mbele ya uso wa dada yake

Roho ya ukatili na mauji sasa ulimvaa upya Alleni tena mara 5 zaidi ya Dr Richard na Laura yeye alitaka kwenda kumaliza waliloanzisha.

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom