JWTZ: Msemaji wa Jeshi, Kanali Mgawe atoa kauli kuhusu Jeshi kulinda amani nchini

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,194
tyt.jpg

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe

--
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi kuepuka vurugu zinazohatarisha usalama, na kulinda amani iliyopo nchini

JWTZ imetoa kauli hiyo siku moja baada ya waumini wa dini ya Kiislamu jijini Dar es Salaam kuandamana sababu ya malalamiko kadhaa kama kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 wiki iliyopita kwa tuhuma mbalimbali, kutoweka kwa kiongozi wa UAMSHO Sheikh Amir Farid Hadi, na malalamiko mengine.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, amesema hatua ya wanajeshi kujitokeza katika kuzima vurugu zilizotokea jijini juzi, ilikua na lengo la kuwaonyesha wananchi kwamba JWTZ ipo kikazi zaidi, na anayetaka vurugu atashughulikiwa kisheria.


"Juzi tulionyesha ‘talent show force' ili watujue kama tupo kazini, hata kama wametuona tupo kimya, hatuna mzaha katika kulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa taifa hili, kwa hiyo tulikuwa kwenye sehemu ya utekelezaji wa majukumu yetu, na kwamba atakayekwenda kinyume tutamshughulikia," alisema Mgawe.

Alisema zoezi hilo litaendelea kwa maandamano yoyote yatakayoonyesha dalili za kuhatarisha usalama wa nchi. Aliongeza kwamba wanajeshi watashiriki kikamilifu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafuata sheria na taratibu zilizopangwa, bila ya kuathiri usalama wa nchi.

Alisema kwa sasa wanasubiri kibali cha polisi cha kuhusu kuhitaji msaada ili waweze kuungana nao katika kushughulikia maandamano yenye lengo la kuhatarisha amani na utulivu.

"Tunawataka wananchi kufuata sheria na taratibu zilizopo na kuepuka kuhatarisha amani ya nchi, kama wanataka tuingie kazini tutafanya hivyo, ila tunachowaasa ni kufuata taratibu zilizopo," alisisitiza.

Katika vurugu za juzi, watu 53 walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, watu hao watafikishwa mahakamani Oktoba 22 mwaka huu.
 
kwa hiyo tutajionea talent show forces za kutosha mpaka M4C imalize kazi yake!
Chadema tusiwe na hofu kwani hiyo ni show tu!
 
Eti wanasubiri kibali cha polisi,yakitokea maandamano yoyote wawe tayara kushiriki,hizi ni salamu za 2015 nilijua alivyostaafu Shimbo siasa jeshini zingekwisha kumbe?
 
Hajaongelea ziwa nyasa?

Tunamuagiza kanali mgawe kapambala arejee madhumuni ya kuanzishwa kwa jeshi la wananchi wa Tanzania. Angeeleza nini kinaendelea kuhusiana na kuonekana kwa shughuli za kijeshi maeneo yenye mzozo wa mpaka na Malawi.
 
Very very very good....labda hapo tutasikia waislamu kadhaa wameuawa kwa kufanya fujo mbele ya wanajeshi kwani wanafanya uhalifu mbele ya polisi na kuua polisi lkn hatusikii wakiuawa ila wanauawa watu wasiokuwa na hatia
 
Jeshi haliwezi kulinda usalama wa raia - waache vitisho! Tanzania inakuwaje? jumuiya ya kambale? kila mtu ana shurubu?
 
hii serikali haieleweki, juzi baada ya maandamano kova aliulizwa kuhusu magari ya kijeshi kuwepo mitaani akakanusha kua alikua hana habari na wanajeshi hao na kwamba labda walikuwepo hapo kwa shuhuli zao zingine..leo msemaji wa jeshi anasema walikuwepo pale ili kujionyesha kua wapo kazini na eti wanasubiri kibali cha polisi..huo ni uongo mtupu..hata siku moja jeshi halisubiri kibali kutoka popote hata kwa Rais..

MKUU wa majeshi akiona hali ya nchi si shwari basi ana nguvu ya kuingia mtaani na jeshi lake bila kibali kutoka ikulu wala mahali popote...na mimi ningeomba mkuu wa majeshi akiona hali ya usalama inazidi kua mbaya na wananchi wanazidi kupoteza maisha yao basi waingie na ikulu wawatoe wote tufanye uchaguzi mpya nchi ianze upya.....
 
Mimi ninadhani jeshi lingejipanga kuchukua uongozi wa nchi hii hadi 2015 ndipo wawaachie raia. Ushahidi kuwa raisi aliyeko madarakani ameshindwa kuongoza. Sio siri kila mtu anajua hili. Hata wanajeshi wenyewe wanajua.
 
"talent show Force" was neccessary given the situation at hand. Kama waislam wakikusudia kwenye kumng'oa JK ikulu unategemea jeshi likae kimya. Inteligentsia ilionesha kwambawaislamwalipanga kwenda ikulu kumtoa rais ndio maana jeshi likajitokeza na show yao. Wangeona polisi wamezidiwa kwa hakika lazima wangeingia kazini!
 
Kanali ameongea kwa umakini mkubwa, lengo ni kutuma meseji kuwa wapo. Wako tayari, kikazi zaidi!

Kwa tafakari ndogo ni kuonyesha tu kuwa na wao wamechoshwa na muelekeo wa vurugu hizi ambazo zinalelewa na hazionyeshi dalili za kwisha.

Bila shaka wanaelewa kuwa kimsingi Polisi ndio wenye jukumu hili.Lakini, aidha kwa makusudi, au kwa kuzidiwa na majukumu wamekuwa wakiachia mambo yakienda ndivyo sivyo bila kuchukua hatua serious zenye lengo la kuondoa tatizo hili. Wamefuga tatizo kwa muda mrefu sana wao na viongozi wao wa Kisiasa.

Kwa maana ya ujumbe, Polisi unawagusa zaidi, kuwa wakiendelea kuwachekea hawa watu, JW wataingilia kati.

Kwa wachoma makanisa, ujumbe wao, kama walizoea kuchekewa na Polisi, sasa wajipange upya. Wadau wengine wako tayari kushughulika nao. Ukujumbe huu ni muafaka pia kwa wafadhili na wote wanaojificha nyuma ya pazia.


Kimantiki, hoja kwamba JW wanaingilia majukumu ambayo si yao, ni sahihi lakini inakosa uzito kwani matatizo haya yameanza muda mrefu na yamelelewa pia. Dalili zote zinaonyesha tunaelekea kubaya, sana.

Na wao ni wananchi pia, amani ikitoweka kwa uzembe wa kujitakia kama huu wa kwetu hata wao wataathirika.

Iwapo bado tunao watu wanaofikiri kidogo, changamoto iliyopo ni kukaa na vyombo hivi vya dola na kuwekeana mipaka ya kimajukumu katika kipindi hiki. Ni lini na katika mazigira gani, ni kipi wafanye, wasifanye.

Hata hivyo, matumizi ya Jeshi yakizidi, hayaleti picha nzuri na baadae inakuwa tatizo kuwarudisha makambini! Dawa ni kutatua tatizo na kuondoa hoja ya wao kuwapo mitaani.
 
mi nilijua wanatest vifaa kwa ajili ya kupigania ziwa le2 lisichukuliwe na malawi kumbe wanaitishia CHADEMA duuuuh hii nchi tunaelekea wapi lakini? MUNGU 2SAIDIE!
 
ni bora tulikotoka kuliko tunakoelekea....... na ni muda wa JWTZ kutumia mabomu yao yaliyo expire yasije kuwalipukia tena
 

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe

--
Alisema kwa sasa wanasubiri kibali cha polisi cha kuhusu kuhitaji msaada ili waweze kuungana nao katika kushughulikia maandamano yenye lengo la kuhatarisha amani na utulivu.


Huu ni ujinga wa kutojua mipaka ya madaraka. Jeshi la Wananchi linafanya kazi kwa kibali cha Polisi, tangu lini? Kwa hiyo sasa Mkuu wa Majeshi nchini ataongozwa na Mkuu wa Polisi nchini? Kama kuna umuhimu wa Jeshi la Wananchi kuingilia suala la ndani la uvunjifu wa amani, Mkuu wa Polisi anapaswa kumtaarifu Raisi ambaye ndiye atatoa amri kwa Mkuu wa Majeshi kutoa wanajeshi wakawasaidie Polisi.

Hii nchi inaenda hovyo hovyo tu kama vile hakuna kanuni. Mbofu mbofu.
 
Jamani with all due respect, sikubaliani kabisa na maneno ya Kanali Mgawe, kwa sababu zifuatazo:

1. Jeshi kujihusisha na usalama wa raia na mali si jambo jema hata kidogo. Kimsingi ni kuhatarisha usalama wa taifa.
2. Jeshi kutumika kutuliza ghasia/maandamano kuna hatari ya jeshi kutumiwa kisiasa kama polisi wanavyotumiwa.
3. Jeshi kutumiwa kuzima maandamano ya kidini haina tofauti na kuzima maandamano ya kisiasa: Jeshi halina dini wala
siasa, iweje lijue ni nani anakosea kisiasa au kidini?
4. Jeshi kuingia mitaani ni tangazo la serikali kushindwa - kinachofuata ni jeshi kuiondoa serikali hiyo au kinyume chake,
yaani kuilinda serikali hiyo isiondolewe hata kama imeshindwa kihalali.
5. Jeshi kuingia mitaani ni tangazo kuwa jeshi la polisi limeshindwa, ni ama livunjwe tujue au tuambiwe sababu za
kushindwa kwa jeshi la polisi.
6. Vitisho vya Shimbo wakati wa uchaguzi vingebatilisha matokeo ya uchaguzi kama tungekuwa na katiba huru na
mahakama huru. Tambo za Kanali ni dalili kuwa dola jeshi linapanga kufanya hivyo mwaka 2015.

Kwa hali yoyote ile, maneno ya Kanali ni mabaya, hayastahili na nitashangaa kama Ikulu itakuwa imeridhia maneno haya yasemwe. Jamani mahali pa Jeshi la Wananchi ni Kambini na Porini, si mitaani hata kidogo. Jeshi lituombe radhi.
 
Back
Top Bottom