WA-UKENYENGE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 2,918
- 1,233
Hapa kuna kitu kinatengenezwa, nyie subirini huko mbeleni kama hawa jamaa hawajang'ang'ania magogoni kwa mgongo wa usalama wa nchi. Hehehe yangu macho!!
kwa hiyo busara yako inakutuma kuvunja katiba ili kumchukulia hatua mtu anayevunja katiba!!hujanielewa siongelei kikatiba hapa naongelea kivita...nchi ishashindikana so ni bora jeshi lichukue nchi...katiba yenyewe ingekua inafuatiliwa tusingekua hapa tulipo
Naunga mkono hoja kwa 100% ni lazima wahuni wote washikishwe adabu.
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi kuepuka vurugu zinazohatarisha usalama, na kulinda amani iliyopo nchini
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe
--
JWTZ imetoa kauli hiyo siku moja baada ya waumini wa dini ya Kiislamu jijini Dar es Salaam kuandamana sababu ya malalamiko kadhaa kama kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 wiki iliyopita kwa tuhuma mbalimbali, kutoweka kwa kiongozi wa UAMSHO Sheikh Amir Farid Hadi, na malalamiko mengine.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, amesema hatua ya wanajeshi kujitokeza katika kuzima vurugu zilizotokea jijini juzi, ilikua na lengo la kuwaonyesha wananchi kwamba JWTZ ipo kikazi zaidi, na anayetaka vurugu atashughulikiwa kisheria.
Juzi tulionyesha talent show force ili watujue kama tupo kazini, hata kama wametuona tupo kimya, hatuna mzaha katika kulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa taifa hili, kwa hiyo tulikuwa kwenye sehemu ya utekelezaji wa majukumu yetu, na kwamba atakayekwenda kinyume tutamshughulikia, alisema Mgawe.
Alisema zoezi hilo litaendelea kwa maandamano yoyote yatakayoonyesha dalili za kuhatarisha usalama wa nchi. Aliongeza kwamba wanajeshi watashiriki kikamilifu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafuata sheria na taratibu zilizopangwa, bila ya kuathiri usalama wa nchi.
Alisema kwa sasa wanasubiri kibali cha polisi cha kuhusu kuhitaji msaada ili waweze kuungana nao katika kushughulikia maandamano yenye lengo la kuhatarisha amani na utulivu.
Tunawataka wananchi kufuata sheria na taratibu zilizopo na kuepuka kuhatarisha amani ya nchi, kama wanataka tuingie kazini tutafanya hivyo, ila tunachowaasa ni kufuata taratibu zilizopo, alisisitiza.
Katika vurugu za juzi, watu 53 walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, watu hao watafikishwa mahakamani Oktoba 22 mwaka huu.
Unaunga mkono kwa mtazamo husio mpana lakini mwisho wa siku utajua kwa nini kasema hivyo pale nao watakapoanza kuingilia mikutano ya kisiasa kwa hicho kisingizio cha usalama wa nchi.Naunga mkono hoja Mgawe yuko sahihi.
... talent show force:clap2:mkwara mzito huo, ile ilikuwa ni show tu! Nmeipenda hii
haya maneno ni kama kitisho kwa chadema.!
hii serikali haieleweki, juzi baada ya maandamano kova aliulizwa kuhusu magari ya kijeshi kuwepo mitaani akakanusha kua alikua hana habari na wanajeshi hao na kwamba labda walikuwepo hapo kwa shuhuli zao zingine..leo msemaji wa jeshi anasema walikuwepo pale ili kujionyesha kua wapo kazini na eti wanasubiri kibali cha polisi..huo ni uongo mtupu..hata siku moja jeshi halisubiri kibali kutoka popote hata kwa Rais..
MKUU wa majeshi akiona hali ya nchi si shwari basi ana nguvu ya kuingia mtaani na jeshi lake bila kibali kutoka ikulu wala mahali popote...na mimi ningeomba mkuu wa majeshi akiona hali ya usalama inazidi kua mbaya na wananchi wanazidi kupoteza maisha yao basi waingie na ikulu wawatoe wote tufanye uchaguzi mpya nchi ianze upya.....