Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,218
General JJ Mkunda.
Commissioner General Immigration Anna Makakala.
Jeshi la Wananchi Tanzania kupitia Mkuu wa Jeshi JWTZ, has again done us proud.
Mkuu wa Jeshi, CDF General Jacob John Mkunda amelezea tishio la usalama wa nchi kutoka angle ambayo kuna jeshi lingine lipo kwa ajili hiyo pekee, Jeshi la Uhamiaji.
Je ni kwamba Jeshi la Uhamiaji halijui tishio hilo la Ulinzi na Usalama kwa nchi, na kutoliweka hilo hadharani?
General Mkunda si tu amelezea kuwepo tatizo la wakimbizi wengi nchini waliokaa muda mrefu bila kurudishwa kwao, lakini kaweka wazi kuwa wamefanya utafiti kuwa kuna wakimbizi waliokaa nchini kwa muda mrefu kiasi kwamba watoto wao au wao wenyewe wameanza kupata vyeo vya kimaamuzi ndani ya serikali na taasisi za umma.
Tunamshukuru Gen JJ Mkunda kwa kuiona the bigger picture(Vision) ya kiusalama, vision mbayo Idara ya Immigration imeshindwa kuiona.
Hii natisha
Ulinzi ni pamoja na kuondoa threat ya the 5th Column, adui aliyepandikizwa from within.
Serikali isiposhughulikia hili kwa haraka itajilaumu yenyewe within 5 to 10 years.
Vile vile Jeshi la Uhamiaji lifumuliwe kwa kuota vitambi na kutofanya kazi iwapasayo.