hivi humu ndani kuna watu wanaotazama jumong?ni tamthilia nzuri mno ya kikorea,na iinahusu siasa zaidi kuliko kingine.natamani wana jf wote wawe wanatama jumong,ina fundisha vitu vingi sana,kama ujenzi wa taifa nk,
me ihate it somuch. Nimekuwa naionaona tu bila
kuconcentrate nayo, maana huwa naona mafarasi,
majambia na mavitu ya ukorofiukorofi, so i see it as very
hostile to me. Anyway, after what you said may be i will try
to give a strait eye to it! Thanks
Nadhani tatizo lenu ni kile kidhungu. Ili uielwe inabidi usome zile sub-titles.
Kama husomi zile itakuchanganya tu. Unadhani wameeka zile sub-titles mapambo?
Sasa pengine nyie mnaangalia picha tu halafu mnategemea miujiza itokee muielewe.
Ni tamthilia nzuri sana, na inafunza mengi sana. Kama husomi na kuielewa utaona watu wanapigana mapanga tu.
Kama alivyosema mmoja hapo juu, ni story about building a new nation, challenges ambazo jamaa wanakutana nazo, na wanavyozikabili. Kikubwa ninachokiona pale ni jinsi watu wanavyoweza kushirikisha akili sana katika kuelewa mazingira yanayowazunguka, na kupanga nini cha kufanya.
Halafu pia kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo, itakuwa ngumu sana kuelewa kinachofanyika hata kama ukisoma zile-subtitle.
Tamthilia hii si kwa watoto, au wenye upeo mdogo. Na definately sio kwa wale wanaotaka hadithi rahisi rahis zilizonyooka.
Mimi huwa sikosi kuiangalia labda kwa bahati mbaya.Ina mafundisho mengi sana licha ya siasa na uongozi hata kimaisha.Nadhani hawa Korea wapo juu katika tasnia ya filamu.Kwa kweli wanaact sio kwa kuogopa kamera,wanajua wanachokifanya na wamejiandaa.
Kabla ya Jumong ilikuwepo nyingine huko ITV inaitwa Jewerly in the Palace ambayo ilikuwa inahusu kugombania madaraka ikulu na ugunduzi wa madawa na tiba,kwa sasa inarudiwa Capital TV.
Hej Agika,well sikujua mashabiki wa Jumong wako wengi, anyhow hata mimi naipenda na hasa kwenye upande wa uvumilivu na umakini wa mipango ya Jumong katika kufanikisha anachokiamini, kama vile Jumong anavyopata misukosuko mingi na ambayo atakuja kuipata mikubwa zaidi ili kutimiza ndoto yake ya kujenga taifa kubwa na lenye nguvu duniani.
ukitaka kuangalia episode ulizozikosa waweza kwenda hapa http://www.filipinasoul.com/jumong-episode-56/
Hej Agika,
Tamthilia inaitwa Jumong, na yule stering ni Chumong na sio Jumong.
Asante kwa hiyo link