Niliyodhani kuhusu watu wa JF, na niliyobaini

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Anyo-Ashi-Mikaaa!

Nakumbuka ni kama miaka 5 nyuma, rafiki yangu ambaye alikuwa classmate wangu alinipa clue kuhusu JF kwa mara ya kwanza... akasema ni jukwaa la ajabu sana.

Akanieleza kuna mtu anaitwa 'miminimkulimaakachekasana', nilicheka sana. Akaongeza kuna mtu anaitwa ng'wanamangilingili, aisee sikuwa na mbavu.

Akasema kule kuna wanaoamini uwepo wa Mungu na wasioamini.

Baada ya maongezi hayo nikashawishika kujiunga JF rasmi.
Nika download app na kusajili account.

Wakati huo kwa alivyoniambia na nilivyojua, ni kuwa JF wamejaa wasomi tupu, mabosi wote wa nchi hii, vigogo wakubwa, 'diaspora' wengi nk!

Hivyo nilikaa kwa password sana nikijua nikiyavurunda tu humu hawana mchezo. Wamejaa intellectuals.

Kwanza nilijua wote humu wana hela, wanafanya kazi BOT, wanawake nilijua wote ni wale wenye majengo marefu Sinza, wenye fedha zao.

AJABU...

Kadri siku zilivyoenda mpaka leo hii, nikagundua JF kuna walalahoi wengi sana kuliko wenye hela. Kwa sababu wengi unakuta wanatamba kwenye uzi huu waki expose maisha ya fahari (siyo vibaya), ila unawakuta wamejificha kwenye nyuzi zingine wanaomba ajira za ualimu, upolisi, wakitafuta kazi zozote nk!

Nikagundua wanawake wengi wa humu (samahanini kwa hili), ni wale waliokosa soko huko mitaani, desperate, waliojikatia tamaa na wanaoishi kwa matumaini. Hawana hela kama nilivyodhani... ni walalahoi.

Nikagundua kwa uchunguzi wangu kuwa wenye fedha humu JF si wachangiaji sana mwenye nyuzi. Na hawaingii JF mara nyingi sana. Hilo ndilo nililobaini.

Mwisho, nikagundua si walalahoi tu, mpaka vilaza wamejaa pia JF kwa nyuzi zao. Unachoandika kwa kujirudia rudia kina uwezo wa kukutambulisha wewe nani.

Kuna nyuzi kama vile, "siwezi ku sex bila chupi kichwani", "nimelala na malaya jana", "mke wangu hajambi", "kula mbususu", "sijui kugegeda", "natamani kunywa damu ya mpenzi wangu", "siwezi kulala na mke wangu bila kumtoa damu" nk, zinatambulisha waandishi wao. NB, siyo vibaya kuandika ni uhuru wao, ila inatoa picha wana nini akilini.

Nilisikitika mno baada ya kubaini haya.!
 
Hapa ni wapi
20230812_151724.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom