JK na miaka 50 ya UDSM: Nipo hivi nilivyo sababu ya UDSM

Calnde

JF-Expert Member
Oct 7, 2008
1,373
277
Katika kipindi maalum kilichoandaliwa na udsm kwa miaka 50 ya udsm, raisi wetu kasema yupo hivyo alivyo kwa sababu ya udsm.

Kwa maana nyingine yeye na utendaji wake ni reflection ya product ya udsm!

Pili anasema ana nia ya dhati kufanya udsm kuzalisha viongozi in next 50 yrz! Sina hakika kama naamini haya hasa hili la pili!

Sijui nani kamponza nani,... Labda ni Kikwete aliye mponza Lowasa au vice versa.

Lakini binafsi, baada ya kuchomwa jua mda mrefu nikisubiri kumuona Museveni pamoja na wenzangu,sikutegemea kusikia niliyoyasikia,ingawa nilikua na hamu kweli kujua wana UDSM wata react vipi baada ya viongozi hawa kufika.

Ilikua hivi:-
Nikiwa mbali kidogo nilisikia kilele za kushangilia,... Na mara nikasogea karibu,lakini niliye kuta akishangiliwa huku anaingia ukumbini ni Prof.Shivji.

Baada ya mda mrefu sana aliingia JK na team yake ya viongozi (akiwemo Lowasa),...ndipo nilipo ishiwa nguvu ghafla ingawa sikuwa mlengwa wa kelele hizo.

Zilisikika kelele za "mafisadi,mafisadi",...."miaka 50 tunalala nje",....
"tunataka mabadiliko",....mara JK alisimama kwa sekunde kadhaa kusoma moja ya mabango yaliyo kuwa yame kamatwa na wanachuo (sijui liliandikwa vipi, bango lilikua upande sawa na wangu ila mbali kidogo).

Yeah,nilihisi aibu na kuhisi sina nguvu.
Niliingia kwenye viatu vya JK,ila sidhani kama ame feel nilivo feel.

Ni aibu sana raisi kupokelewa nchini kwako kwa dhihaka kiasi hiki.
 
hii point ni ya muhimu sana kuisikia, nilisikia hapo nyuma baadhi ya Wakenya wakikitaka UDSM kumvua shahada Mh. Kivuitu kwa kufanya mambo ambayo hayakuwaridhisha na sikumbuki hoja hiyo iliishia wapi!

Sasa wanaJF na hasa wale waliopitia hapo UDSM ni muda wenu kuchallenge hii statement au la sivyo muache kumuandama JK amalizie miaka yake minne!
 
inasemekana huyu bwana huogopa kwenda udsm mana atazomewa! Hata wanafunzi walimkataa mbele ya mkandala mwaka jana kuwa mgeni rasmi
 
Sijajua urafiki wake na M7 ni kwasababu wamesoma pamoja au kwa vile waswahili husema ndege wanaofanana huruka pamoja!
 
siyo kosa lake...ni wajibu kukishukuru chuo kwa angalau kumfanya hivyo alivyo. asingepita hapo ingekuwaje? tuwapongeze udsm kwa kujaribu kumbadilisha jameni!!! chuo kimemshepu
 
siyo kosa lake...ni wajibu kukishukuru chuo kwa angalau kumfanya hivyo alivyo. asingepita hapo ingekuwaje? tuwapongeze udsm kwa kujaribu kumbadilisha jameni!!! chuo kimemshepu

Duh! In that perspective, hongereni udsm. Otherwize ingekuwa janga la taifa+++
 
Amekidhalilisha udsm daaa! Lakini kuna kaukweli aaati si hata wasaidizi wake weengi ni udsm,
na nivilaza daaaaa!
 
Kwa statement hii ya JK anakidisvalue chuo kikuu cha dar es salaam. Hebu watz tuamke sasa tuangalie graduate wengine ufanisi wao kwenye utendaji wa kazi.
 
jamani niwe mkweli, jk anaingia ukumbini na M7! Wanafunzi hawapigi makofi wala kushangilia. Nje wanafunzi wanaimba kama sio juhudi zako nyerere mafisadi wangesoma wapi!?
 
Niwapongeze wanafunzi wa udsm waliojipanga na mabango nje ya ukumbi wa nkuruma na kuyanyanyua wakati kikwete na museveni wanapita kuingia ndani ukumbini.

Pia niwapongeze kwa kupaza sauti kwa ule wimbo maarufu wa ''kama sio juhudi zako Nyerere'' bila shaka kikwete na museveni wamepata joto la kuwafaa watakapoondoka watakuwa wameipata.
 
Back
Top Bottom