JK na miaka 50 ya UDSM: Nipo hivi nilivyo sababu ya UDSM

Sura za wakuu zinatia huruma! Nje wanafunzi wanaimba balaa! Full kelele nje, wanazomea! Kikwete katajwa ndani wanafunzi nje, boooooo! Dah
 
Katika kipindi maalum kilichoandaliwa na udsm kwa miaka 50 ya udsm, raisi wetu kasema yupo hivyo alivyo kwa sababu ya udsm. Kwa maana nyingine yeye na utendaji wake ni reflection ya product ya udsm! Pili anasema ana nia ya dhati kufanya udsm kuzalisha viongozi in next 50 yrz! Sina hakika kama naamini haya hasa hili la pili!
mkuu hii typical mind fallacy anaileta huyu mkuu wa kaya
The typical mind fallacy is the mistake of making biased and overconfident conclusions about other people's experience based on your own personal experience; the mistake of assuming that other people are more like you than they actually are.
kwanini atakujificha kwenye kimvuli huyu..........agrrrrrrrrrrrh
failure zake asitubeshe atuhusikiii kwa vyovyote vile ahaaah..
mweeh...
 
Sura za wakuu zinatia huruma! Nje wanafunzi wanaimba balaa! Full kelele nje, wanazomea! Kikwete katajwa ndani wanafunzi nje, boooooo! Dah
nilitegemea hii kitu nafikiri atajua kwanini walimzoea maghembe mbele ya museveni na yule msolwa peter mbele ya thabo mbeki
ile ni intellectual society
 
Niwapongeze wanafunzi wa udsm waliojipanga na mabango nje ya ukumbi wa nkuruma na kuyanyanyua wakati kikwete na museveni wanapita kuingia ndani ukumbini.

Pia niwapongeze kwa kupaza sauti kwa ule wimbo maarufu wa ''kama sio juhudi zako Nyerere'' bila shaka kikwete na museveni wamepata joto la kuwafaa watakapoondoka watakuwa wameipata.
naipenda mlimani nafikiri ile solidarity bado ipo na huu wakati muafaka wa kumfikishia mkuu ujumbe direct vijana ujasiri unahitajika unosheni tofauti
 
Kuna sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya chuo kikuu cha dsm ambapo itv wapo live, wageni wa adabu ni JK na Mseveni, tumeona walau kwa muda wanafunzi ambao wapo nje wakiimba nyimbo za kumsifu Kambarage na kulaani mafisadi.

Wakiwa na mabango! Mliopo eneo la tukio mtujuze kinachojiri.

Nawasilisha.
 
jamani niwe mkweli, jk anaingia ukumbini na M7! Wanafunzi hawapigi makofi wala kushangilia. Nje wanafunzi wanaimba kama sio juhudi zako nyerere mafisadi wangesoma wapi!?

Mkuu hata mimi nimeiona hiyo kupitia itv, kikwete amenywea!
 
Nimesikia makelele yenye ishara ya kuzomea wakati JK alipokuwa akiingia ukumbini!
Source: radio 1

aliyeko eneo tukio atupe habari kamili!
 
Sijui nani kamponza nani,... Labda ni Kikwete aliye mponza Lowasa au vice versa.

Lakini binafsi, baada ya kuchomwa jua mda mrefu nikisubiri kumuona Museveni pamoja na wenzangu,sikutegemea kusikia niliyoyasikia,ingawa nilikua na hamu kweli kujua wana UDSM wata react vipi baada ya viongozi hawa kufika.

Ilikua hivi:-
Nikiwa mbali kidogo nilisikia kilele za kushangilia,... Na mara nikasogea karibu,lakini niliye kuta akishangiliwa huku anaingia ukumbini ni Prof.Shivji.

Baada ya mda mrefu sana aliingia JK na team yake ya viongozi (akiwemo Lowasa),...ndipo nilipo ishiwa nguvu ghafla ingawa sikuwa mlengwa wa kelele hizo.

Zilisikika kelele za "mafisadi,mafisadi",...."miaka 50 tunalala nje",....
"tunataka mabadiliko",....mara JK alisimama kwa sekunde kadhaa kusoma moja ya mabango yaliyo kuwa yame kamatwa na wanachuo (sijui liliandikwa vipi, bango lilikua upande sawa na wangu ila mbali kidogo).

Yeah,nilihisi aibu na kuhisi sina nguvu.
Niliingia kwenye viatu vya JK,ila sidhani kama ame feel nilivo feel.

Ni aibu sana raisi kupokelewa nchini kwako kwa dhihaka kiasi hiki.
 
Kwakweli leo ni siku ambayo wanafunzi wa udsm wamenifurahisha kupita maelezo!hawawezi kumshangilia mtu wakati hawana hata pa kulala,mikopo,madarasa ya kutosha,sehemu za kusomea nk!viongozi wetu wanatembea vifua mbele wakati wanafunzi wanamatatizo kibao! Dawa ya mtu anayechekacheka huku watu wana uchungu ni kama hiyo Udsm waliyompa leo.
 
Sura za wakuu zinatia huruma! Nje wanafunzi wanaimba balaa! Full kelele nje, wanazomea! Kikwete katajwa ndani wanafunzi nje, boooooo! Dah

Sidhani kama atathubutu kwenda udsm siku nyingine manake vijana wakisikia tu jina la kikwete linatajwa wanapiga bonge la booooooooooooo! Aibu
 
I wish camera ingebaki kule nje maana hapa hili lisura la mkandara linaleta njaa tu, kakunja uso bila shaka kwa sababu za sauti za vijana huko nje
 
mi ngeleja keshanihanith!!! sina umeme, nasikia kupitia radio 1. tupeni facial expressions mlioko live ukumbini na mnaoangalia itv

pole sana, mkandala anaongea lakini sura yake ina huzuni si kama alivyokuwa wakati wa presidential dina juzi juma5
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom