JK na miaka 50 ya UDSM: Nipo hivi nilivyo sababu ya UDSM

Nipo chuoni sasa hivi......NIMESHUHUDIA KWA MACHO YANGU RAISI AKIZOMEWA LIVE..... YAANI AMEZOMEWA NA WANAFUNZI WA CHUONI MPAKA AMEONA AIBU.:embarassed2:
 
You get what you choose........ndivyo maisha yalivyo

Hivi mara ya mwisho kwa JK kwenda UDSM ilikuwa mwaka gani vile? Alishakuwa president?
 
You get what you choose........ndivyo maisha yalivyo

Hivi mara ya mwisho kwa JK kwenda UDSM ilikuwa mwaka gani vile? Alishakuwa president?

sidhani kama amewahi kuja kwenye tukio kubwa kama hili.
Kama amekua akija basi ni kimya kimya au wanachuo wakiwa hawapo
 
Kwa kwel kilichomkuta jk leo ni aibu,jamaa wamemzomea yeye na museven wake ile mbaya.
 
Mmmh!! Kwa hiyo matatizo yote haya yanatokana na udsm?

Inamaana UDSM isingalikuwepo watanzania tusingekuwa kwenye hali mbaya kama hii tuliyonayo. Udsm mmetuletea balaa gani hili?
 
Wakuu,

Kuna mtu wangu wa karibu yupo UDSM ameniambia JK kazomewa wakati anaingia ukumbini Nkurumah. Wanafunzi maelfu wameudhuria na walipoingia wanazuoni kama Shivji, Dr. Mwami na wengine walishangiliwa mno. Aliyepo Nkurumaha hall atujuze pls
 
Hiyo nimeishuhudia LIVEEEE:photo: .... SAFI SANA UDSM, NIMEONA FIRST YEAR WAMEMTOLEA HASIRA ZAO ZA KUKOSA MAKOPO..
 
Sijui nani kamponza nani,...
labda ni Kikwete aliye mponza Lowasa au vice versa.
Lakini binafsi, baada ya kuchomwa jua mda mrefu nikisubiri
kumuona Museveni pamoja na wenzangu,sikutegemea kusikia niliyo
yasikia,ingawa nilikua na hamu kweli kujua wana UDSM wata react vipi
baada ya viongozi hawa kufika.

Ilikua hivi:-
Nikiwa mbali kidogo nilisikia kilele za kushangilia,...
na mara nikasogea karibu,lakini niliye kuta akishangiliwa huku
anaingia ukumbini ni Prof.Shivji.

Baada ya mda mrefu sana aliingia JK na team yake ya viongozi
(akiwemo Lowasa),...ndipo nilipo ishiwa nguvu ghafla ingawa sikuwa mlengwa wa
kelele hizo.

Zilisikika kelele za "mafisadi,mafisadi",...."miaka 50 tunalala nje",....
"tunataka mabadiliko",....mara JK alisimama kwa sekunde kadhaa kusoma moja
ya mabango yaliyo kuwa yame kamatwa na wanachuo.
(sijui liliandikwa vipi,bango lilikua upande sawa na wangu ila mbali kidogo).

Yeah,nilihisi aibu na kuhisi sina nguvu.
Niliingia kwenye viatu vya JK,ila sidhani kama ame feel nilivo feel.

Ni aibu sana raisi kupokelewa nchini kwako kwa dhihaka kiasi hiki.

sasa nimerudi rasmi baby. nilipita kwa sababu sikuelewa somo.

tupe habar ila angalia wasikudabue.
 
safi sana udsm...wamzomee sana mpaka ajute kuwa rais na kutuongoza lkipumbavu na bila mwelekeo....miahadi mingi na utekelezaji zero!!!!
 
na bado..atajamba puto mwaka huu!! kama ana hasira ameze boga tumuone komando, si kanali yule?? alidhani tunafurahi kuhongwa kwake kaptura na vijambakoti..
 
Nipo chuoni sasa hivi......NIMESHUHUDIA KWA MACHO YANGU RAISI AKIZOMEWA LIVE..... YAANI AMEZOMEWA NA WANAFUNZI WA CHUONI MPAKA AMEONA AIBU.:embarassed2:

vizuri sana vijana! Watu wamechoka maisha magumu, unamaliza chuo ajira hakuna kama zipo wanapeana kindugu.
 
Back
Top Bottom