Kudhibiti Uongozi Mbaya, Kuwe na Review ya Viongozi Wakuu Kila Baada Ya Miaka Minne.

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,058
Tatizo la Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni uongozi mbaya. Uongozi mbaya umesababisha udumavu wa kila nyanja ambayo ingeleta maendeleo ya Taifa.

Uongozi mbaya kwa Taifa letu zaidi upo katika makundi mawili:
1) Uovu unaotokana na tamaa ya utajiri. Tamaa ya utajiri imewafanya viongozi kuingia kwenye mikataba ya kifisadi, wao wenyewe kuwa mafisadi, viongozi kuwa na upendeleo kwa watu wao iwe ni kwenye tauzi za upe deleo au kuwapa rasilimali za nchi ili wawe matajiri.

2) Uongozi mbaya unaosababishwa na uwezo mdogo. Kwenye hili ni viongozi kuwa na mipango isiyo na maana, kuwateua viongozi wanaoendana na uwezo wao mdogo, kuingia kwenye mikataba ya hovyo, na kutengeneza sera na sheria zisizo sahihi katika kutatua matatizo yanayolikabili Taifa.

NINI KIFANYIKE
1. Upatikanaji wa haraka wa katiba mpya
2. Katiba ifute kinga ya kutoshtakiwa kiongozi yeyote yule wa nchi.
3. Rais asihusike kwa namna yeyote ile katika kuteua majaji na jaji mkuu, katibu wa Bunge, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkurugenzi wa TAKUKURU na wala asihusike na uteuzi wa IGP.
4. Kuwepo na kamati maalum ya majaji inayofanya review ya uongozi na vitendo vya Rais, Makamu wa Rais, IGP CDF na Waziri Mkuu kila baada ya miaka 4. Review ipelekwe Bungeni na kutangazwa kwa umma, kisha kujadiliwa kwa uwazi na Bunge. Review hiyo izingatie uadilifu wa hao viongozi wakuu na uwezo wao katika kufikia malengo ya Taifa kwenye kila nyanja. Kutokana na hiyo review, Bunge liunde kamati za uchunguzi dhidi ya wahusika kama review ya majaji itaonesha kasoro kubwa kwa viongozi hao. Ikithibitika viongozi hao ama wamekosa uadilifu au wana uwezo mdogo, Bunge linaweza kupitosha azimio na wahusika hao kutoruhusiwa kugombea cheo chochote cha umma baada ya kumalizia kipindi cha uongozi wao. Lakini pia azimio la Bunge halitazuia uwezekano wa viongpzi hao kufikishwa mahakamani kama itathibitika walizitumia nafasi zao vibaya.

5) Kuwepo na kamati maalum ya wabunge inayofanya review ya utendaji kazi wa Jaji Mkuu na wakuu wote wa mahakama, kila baada ya miaka 3. Wahusika wakithibitika kuwa na uwezo mdogo wa kuisimamia mahakama au wao wenye kuwa na maadili yanayotia mashaka, uchunguzi maalum utaanzishwa, na ikithibitika, wahusika wote waondolewe kwenye nafasi zao.

Tukiwa na mfumo huo, tutaweza kuyazuia mambo makubwa matatu kwa wakati mmoja:

a) Kutokuwa na viongozi wa wasio waadilifu au viongozi wenye upeo na uwezo duni.

b) Ikitokea tukampata kiongozi asiye mwadilifu au mwenye uwezo mdogo, ataongoza kwa miaka mitano tu. Na hivyo kutoleta uharibifu mkubwa.

C) Kila mhimili utakuwa na nafasi ya kuchunguza uadilifu wa mhimili mwingine.
 
Bila katiba inayotoa nguvu kwenye taasisi za serikali na sio mtu mmoja
 
Bams kwenye nini kifanyike..
1. Kwenye namba 2 ongeza kusiwepo kinga kwa maafisa wa TISS pia.
2. Katika orodha ya uliowataja namba 3 Rais asiteu pia mkurugenzi wa TISS kuwepo utaratibu wa kupata candidates na hata maafisa wa TISS wengine hasa wakati Rais mpya anaingia madarakani.
 
Kiongozi anaweza kuwa mzuri as an individual. Lakini mob inayomzunguka ika muahiri. Kwaa hiyo aanaajiikuta anajaribu kutimiza matarajio ya wwennzake na kusahau mabosi halisi ambao ni wananchi.
 
Back
Top Bottom