JK aenda Uingereza kikazi

Hivi anafuata nini huko tena jamani!?? arghh i'm gonna be sick! kwa nini asitulie nyumbani??

Yaani nashindwa hata kujijibu mwenyewe. Mimi kama mdada, au mwanamke, ningekuwa Rais, nisingekubali kejeli kama hizo hapo, licha ya yote niende kwenye hiyo nchi. Rais wetu kusema kweli anatia aibu
 
Yaani nashindwa hata kujijibu mwenyewe. Mimi kama mdada, au mwanamke, ningekuwa Rais, nisingekubali kejeli kama hizo hapo, licha ya yote niende kwenye hiyo nchi. Rais wetu kusema kweli anatia aibu

Aibu anajitia mwenye na familia yake, kwanza mimi sio rais wangu na wala siwezi kuwa na rais mji*** kama huyo
 
Hivi huyu jamaa anataka wa Tanzania tumfanye nini? mbona analazimisha kitu ambacho si sahihi kwa watanzania jamani?
 
Kwa kweli inakera sana sasa! Yaani kucha kulala yeye safari hazimuishi hata safari ambaya waziri angeweza kwenda yeye anakwenda. Mara utasikia Mh. Rais aenda Denmark kujifunza jinsi Wanavyosindika maziwa!!! Kitu kama hiki kinatija kweli? Kama si ufujaji ni nini? Tena unaambia gharama anazotumia raisi kwa safari moja kama hiyo unaweza kujenga vyumba saba vya madarasa ya shule ya msingi huu je si ufujaji? Inasiktisha sana kibaya zaidi anadai anakwenda kutafuta wawekezaji!!!!?

Hebu tuangalie mifano ya wawekazaji waliopo ambao Mh Rais hujinasibu kwamba anachangia Kuwaongeza anapokwenda nje:

1. Muarabu wa Loliondo alimilikishwa Loliondo kwa miaka 90.....Matokeo yake badala ya taifa kunufaika yeye anawinda pamoja na kupeleka wanyama Uarabuni!!! Akili zako changanya na zakeee!

Mbaya zaidi waarabu wanaharibu vijana wetu. Kwa umasikini wa Watanzania (kwa kuibwa rasilimali zao) wanakubali kurubuniwa na wamekuwa Ubwabwa. Dangerous life
 
Yaani hata mwezi wa pili haujaisha yeye tayari kashatoka safari zaidi ya tatu yaani kila mwezi lazima asafiri wakati hapo Jirani Kibaki hajasafiri tangu mwaka uanze
 
IMG_1034.JPG



JK AELEKEA UINGEREZA LEO KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi.(picha na Freddy Maro).

Ama kweli JF ni kiboko!!! huyu babu mkuu wa dar sasa anavaa kiutu uzima?? ameacha kuwaonyesha wajukuu kifua!!! te te te ha ha ah !!!!
 
Kama tungeambiwa kuna enterview Ikulu ya kumshauri Rais kupunguza safari naamini hakuna yeyote kati yetu angekuwa mshauri mzuri kama angepata ajira hiyo. Kumshauri Rais kupunguza safari kunahitaji hoja za nguvu ili hata kama kuna wasaidizi wanapita JF waondoke hapa wakijua namna bora ya kumshauri.


Wengi tumetumia dhihaka, kejeri na udhalilishaji kama hoja ya nguvu kuishauri Ikulu. Kazi ya kushauri si rahisi kama wengi tunavyodhani hata sisi hapa imetushinda tunategemea nani amshauri Jk kwa hoja za msingi ambazo msingi wake ni kukubaliana nasi.
 
Nimepitia thread ya kwanza mpaka ya mwisho kabla sijatoa maoni yangu. Hakuna mwenye hoja zaidi ya kejeri. Tutawashawishi vipi watanzania ambao hawaelewi hoja ya kupunguza safari kama sisi wenyewe tunakosa hoja?

Tukumbuke sio watanzania wote wanaoelewa hoja hii. Tutumie jukwaa hili kujenga hoja ambazo zitaungwa mkono na wengi kama zitabainishwa wazi hapa.
 
Mkuu wa kaya kachomoka kwenda uk baada ya kuitwa na ka bwana mdogo. Kweli ombaomba haheshimiki, kwa nini huo mkutano usifanyike dar au Arusha? Ok mwambie akupe chenji ya rada
 
Mimi naomba tu baba riziwani asikubali hoja za huyo mwehu(david) za kuhalalisha mashoga.

kama hataki kutupa chakula asitupe tu kulikoni uwoupumbavu wake.
 
kusema tu hatutaki JK asafiri si hoja tuzame ndani kueleza madhara ya kusafiri kwake ili wasomaje tupime kama zina nguvu. Mada hii hakika siielewi nakutana na matusi tu.

mods kama kejeri hizi zingetupwa kwa yule Rais wetu aliyeshindwa kuingia Ikulu ingeishaondolewa lakini kwa sababu thread haina hoja bali matusi tu dhidi ya Jk itaachwa iendelee.

Siko hapa kumtetea Jk bali nipo kutaka tujenge hoja za maana ambazo zina maslahi kwetu na taifa letu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom