makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
JK AELEKEA UINGEREZA LEO KWA ZIARA YA KIKAZI
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi.(picha na Freddy Maro).
Huyu tangu aingie madarakani anaitwa ni RAIS WA NCHI ZA NJE na si Rais wa Tanzania. Kwanini hizi safari asimwachie Bernad Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya nje??
Hakika JK anatia aibu maana kila siku yuko nje ya nchi na ndiyo maana kuna matukio yanayolikumba Taifa letu na yeye akiwa hana habari kabisa au kwa yale anayoyajua HUYAKIMBIA!!!!
Katika awamu zote za Urahisi,JK ndiyo ameonekana kuwa Rais dhaifu,mbambaishaji na asiyejiamini kwa jambo lolote!