JK aenda Uingereza kikazi

valour

Senior Member
Aug 3, 2010
168
71
Nimesoma kwenye michuzi blog, JK ameenda UK leo asubuhi kwa ziara ya kikazi.

Ni juzi tu nilikuwa najiuliza kama ameshawahi kukaa japo mwezi akiwa ofisini anaangalia files au anasoma vitabu au ku'review' mambo mbalimbali yanayoendelea nchini sikupata jibu.

Vile imeandikiwa ziara siwezi kujua kama ina tija kwa Taifa au ila ifike wakati ambapo ziara zake ziwe zinaratibiwa ili kupunguza matumizi. Nchi yetu ni tajiri lakini inakuwa maskini kwasababu ya kutokuwa na maono na vipaumbele
 
IMG_1034.JPG

JK AELEKEA UINGEREZA LEO KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi.(picha na Freddy Maro).
 
Mbona jana usiku nimemwona arusha ? Duh sio mchezo hata kidogo . Anakula nyara kweli.
 
Mwacheni afaidi jamani.....URAIS afrika maana yake ni kula bata mfululizo mpaka hapo........!!
 
IMG_1034.JPG

JK AELEKEA UINGEREZA LEO KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi.(picha na Freddy Maro).
hapo ni kama anamuambai wewe jamaa bana nasikia ofisi yako inanuka mavvi bhana hadi kule JF wamekurusha bana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom