Mkuu wangu kwa nini tuandikie mate wakati wino Upo.... Yeye sii anajua hizo kanuni nimemwomba hivi:- Sasa wewe unayejua kanuni za NCCR nambie ama nionyeshe mahala inaposema mtu asipokuwa na confidence na kiongozi mwenyekiti afukuzwe uanachama. Ukinionyesha hilo tu, sina maelezo zaidi na kama hutakuja na jibu hilo basi sina sababu ya malumbano..Mkandara, yaya alikuuliza jambo moja la msingi kabisa kama unajua umuhimu wa katiba, kanuni na miongozo katika vyama vya siasa. Unaweza kutuambia ni ngazi gani mathalani ndani ya NCCR-M inayoweza kumvua uanachama mwanachama wake au ukishakuwa mwanachama basi huwezi kufukuzwa.
Ieleweke hapa sitetei chama wala Kafulila natetea principles, ilichokifanya NEC ya NCCR ni kutafsiri kanuni na miongozo ya chama na ikaonekana Kafulila kakiuka misingi ya katiba yao na kulingana na katiba yao inakiruhusu kikao kumvua uanachama mtu yeyote regardless ya wadhifa wake sasa hapo kosa liko wapi, hapa ndipo Lema anaposimamia. Kama ni kosa si la chama kama chama bali ni la mjumbe mmoja mmoja ndipo hapa linakuja suala la maadili ya wajumbe na Mbatia inclusive.
Vyama havianzishwi ili kupata wabunge vinaanzishwa ili viongoze watu kwa hiyo hakiwezi kusita kumfukuza mtu kama ni mtovu wa nidhamu kwa vile tu yeye ni mwakilishi afterall yeye ndiye alitakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa jamii. Kuhusu Lema, umeuliza amesema kama nani ndani ya NCCR je wewe unasema kama nani, hayo ni mawazo yake tu kama yalivyo yako na kuwa kiongozi haufungwi kuwa na mawazo binafsi, halafu nawashangaa sana watu wanaodai freedom of expression ilhali linapokuja suala la Lema wanasahau kama na yeye anahitaji hiyo freedom of expression.
Akiweza kunionyesha hilo ubishi huu wa nini maana tutakuwa tumejifunza wengi hapa janvini maana yeye anajua sana ya NCCR!