Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Mkandara, yaya alikuuliza jambo moja la msingi kabisa kama unajua umuhimu wa katiba, kanuni na miongozo katika vyama vya siasa. Unaweza kutuambia ni ngazi gani mathalani ndani ya NCCR-M inayoweza kumvua uanachama mwanachama wake au ukishakuwa mwanachama basi huwezi kufukuzwa.

Ieleweke hapa sitetei chama wala Kafulila natetea principles, ilichokifanya NEC ya NCCR ni kutafsiri kanuni na miongozo ya chama na ikaonekana Kafulila kakiuka misingi ya katiba yao na kulingana na katiba yao inakiruhusu kikao kumvua uanachama mtu yeyote regardless ya wadhifa wake sasa hapo kosa liko wapi, hapa ndipo Lema anaposimamia. Kama ni kosa si la chama kama chama bali ni la mjumbe mmoja mmoja ndipo hapa linakuja suala la maadili ya wajumbe na Mbatia inclusive.

Vyama havianzishwi ili kupata wabunge vinaanzishwa ili viongoze watu kwa hiyo hakiwezi kusita kumfukuza mtu kama ni mtovu wa nidhamu kwa vile tu yeye ni mwakilishi afterall yeye ndiye alitakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa jamii. Kuhusu Lema, umeuliza amesema kama nani ndani ya NCCR je wewe unasema kama nani, hayo ni mawazo yake tu kama yalivyo yako na kuwa kiongozi haufungwi kuwa na mawazo binafsi, halafu nawashangaa sana watu wanaodai freedom of expression ilhali linapokuja suala la Lema wanasahau kama na yeye anahitaji hiyo freedom of expression.
Mkuu wangu kwa nini tuandikie mate wakati wino Upo.... Yeye sii anajua hizo kanuni nimemwomba hivi:- Sasa wewe unayejua kanuni za NCCR nambie ama nionyeshe mahala inaposema mtu asipokuwa na confidence na kiongozi mwenyekiti afukuzwe uanachama. Ukinionyesha hilo tu, sina maelezo zaidi na kama hutakuja na jibu hilo basi sina sababu ya malumbano..

Akiweza kunionyesha hilo ubishi huu wa nini maana tutakuwa tumejifunza wengi hapa janvini maana yeye anajua sana ya NCCR!
 
Mkuuwangu kwa nini tuandikie mate wakati wino Upo.... Yeye sii anajua hizo kanuninimemwomba hivi:- Sasa wewe unayejua kanuni za NCCR nambie ama nionyeshe mahala inaposema mtuasipokuwa na confidence na kiongozi mwenyekiti afukuzwe uanachama.Ukinionyesha hilo tu, sina maelezo zaidi na kama hutakuja na jibu hilo basisina sababu ya malumbano..

Akiweza kunionyesha hilo ubishi huu wa nini maana tutakuwa tumejifunza wengihapa janvini maana yeye anajua sana ya NCCR!
Mkandara kilichomponza Kafulila si hayo unayomuuliza Lema ila ni NIDHAMU yake, hata Kafulila aki file case mahakamani na kusema amefukuzwa NCCR kwa kumpinga mwenyekiti definitely atashindwa kesi. Unaweza kuwa uko sahihi kuwa Kafulila alikuwa sahihi kutokuwana imani na mwenyekiti wake kitu ambacho hata mimi sikipingi lakini je alitumia njia sahihi kupresent hoja yake bila kukiuka kanuni za chama?
 
Mkandara kilichomponza Kafulila si hayo unayomuuliza Lema ila ni NIDHAMU yake, hata Kafulila aki file case mahakamani na kusema amefukuzwa NCCR kwa kumpinga mwenyekiti definitely atashindwa kesi. Unaweza kuwa uko sahihi kuwa Kafulila alikuwa sahihi kutokuwana imani na mwenyekiti wake kitu ambacho hata mimi sikipingi lakini je alitumia njia sahihi kupresent hoja yake bila kukiuka kanuni za chama?
navyokumbuka mimi kama nilisoma vizuri, Kafulila na wajumbe wengine wali file case hii ktk kikao cha Nec mwezi jana na habari hizi tulizijua wengi tu na Kafulila alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ni baada ya kuwakilisha malalamiko yao.

Mkuu wangu chama chochote kinapomfukuza uanachama hadi mgombea Urais wake na wajumbe wengine sijui 20 kwa tuhuma za kutoa siri ambayo inamweka mwenyekiti kufanya kazi na CCM, kisha mnadai ilikuwa siri ya chama hapo mnawatisha hadi wananchi na wanachama...NCCR inajiweka mahala pabaya zaidi kwa sababu katibu hakutakiwa kutoa maamuzi yoyote hadi kikao kijacho cha Nec na kama ni dharura mwenye kushtakiwa alikuwa Mbatia na sio Kafulila wangeharakisha hilo basi kumsafisha kwanza.

Swala la Mbatia liliahirishwa hadi kikao kijacho cha chama ya Kafulila kikao cha dharura hivi kweli unatakiwa kuitisha kikao cha dharura kwa madai gani mazito! madai gani mazito kati ya Mwenyekiti anayefanya kazi na chama kingine au mtuhumu anayezungumza na magazeti. Kikao cha dharura kingekuwa dhidi ya Mbatia bila hata kufikiri sana...Nimemaliza mengine mtajaza wenyewe. Lema alitakiwa kushtuka kwa habari hizi na sio kuwasifia chama ambacho kinatia mashaka hata sisi wananchi kujiunga nacho - Ati siri za chama!

Simtetei Kafulila hata kidogo lakini Uongozi wa NCCR hawakutumia akili kabisa...wao ndio wanatisha sasa hivi it seems kama kuna conspiracy ya viongozi wote wa juu kuhusiana na ushirika wao na CCM na which makes them CCM - C.
 
soma kisha tafakari........*

*“nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa mbunge**david**kafulila na nilipata fursa**ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa jamii forum na kuona mawazo ya**watanzania mbali mbali juu ya jambo hili.

Na ninafikiri ninao wajibu**kama kijana tena mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana bwana david kafulila.

“ kwanza kabisa bwana david kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo , utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa**changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye**hekima zaidi**kwani katika kila changamoto kubwa duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea duniani.

*ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha nccr-mageuzi**kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba**“ nidhamu katika chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika taifa,**binafsi**sifurahi wewe kufukuzwa katika chama lakini nimefarijika na jinsi chama**kinachukuwa**taratibu kama nccr kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya taasisi ya chama cha siasa.

Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini david katika maisha ya siasa na nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio**na hauwezi kuviepuka**ndio maana , mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa “ huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na**baadae vifaranga watatotolewa.

lakini vile vile mtu huyu mwenye hekima akasema tena**“ haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia “ kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni*muhimu katika kufikia malengo makuu.

Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu**na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu**? Na vile vile tufikirie kama leo mbunge au diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu**nidhamu ndani ya vyama vyao**,je*vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?


nccr mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ? Kama nafasi ya ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi**dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ?

**sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia**njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? Nina wasi wasi kuwa**siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa**na**waziri mkuu wa uingereza ili muweze**kula lakini**kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .


hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio**kuwa ni**pamoja na**nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji**yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu,**na ni hatari**wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala , kwani ugomvi wetu**vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera**bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea taifa madhara makubwa.

*aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa david , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha**na jambo la kushangaza hapa,**ni kwanini watu wameshituka sana mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu**, hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua**sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana ,
sasa nimalizie kwa kusema**david bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi**kama,**martin luther king jr.**alivyopata*kunena***“*the ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.

naibu katibu mkuu wetu mh zitto nimesoma habari mbali mbali kuwa amekukaribisha chadema ,**lakini mimi kwa sasa**nakukaribisha**arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ?

Mfano ,ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi mungu lakini**pia itakupasa kwenda hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio mbunge tena


*“jipe moyo david kafulila na hongera nccr-mageuzi. . Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa**“ the 21 most powerful minutes in a leaders day “ kilichoandikwa na na mwandishi maarufu “ john c. Maxwell.
*
if you are a leader , it’s not enough to know what to do . You have to know when to act. “ john c. Maxwell.

godbless lema . (mb)

word...
 

Similar Discussions

30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom