Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Mawazo kama haya ni sehemu ya udhaifu wa jamii yetu, hasa vijana wa leo. Hamwamini katika mawazo ya kujitegemea. Hamuwezi kutoa mawazo yenu kwa uhuru hadi muone fulani amesemaje. Bahati mbaya ni kwamba mnafikiri kila moja hapa anawakilisha mawazo ya mtu fulani-this is what we call the- 'we suscepct in others what we feel in ourselves'- attitude. Kijana sio kila mtu yupo kama wewe. Kama wewe huwezi kusimama kwa mawazo yako mwenyewe ni wewe; wengine tuna uhuru wa kuandika tunachokiamini bila kujali kama kitamuudhi au kumfurahisha nani. Jikomboe, uwe na fikra huru-usijiegeshe kwenye mawazo na fikra za mtu/watu wengine-ni hatari kwa afya ya akili yako. Be warned!

asante
 
umenena kaka ila mbatia naye si mungwana katika kukuza upinzani hata kidogo anatumika sana na ccm
Binafsi si mpenzi wa haya mambo ya siasa, lakini hili la James kuwa anakisaidia chama cha mapinduzi linasemwa sana , lakini hakuna hata mmoja anayeweka ushahidi ni jinsi gani mbatia anatumika na ccm:juggle:
 
Lema, watanzania hatuna utamaduni wakusema "sorry" kwa hiyo usitegemee kitu kama hicho toka kwa Kafulila, sababu angeweza kusema neno hili hili miaka michache iliyopita baada ya kuzuka mgogoro baina yake na uongozi wa CHADEMA then mambo haya yote yaliyotokea yasingekuwapo sababu angekuwa bado CHADEMA, but instead aliamua kuhama kwa hasira zake - Sasa dhambi ya kutosamehe inakuwa inakuandamana popote uendako.

YES, aseme "Sorry" aanze upya na NCCR yake hata kama atabakia kuwa mwanachama wa kawaida lakini itajenga heshima zaidi rather than deciding to jump into another Political Party - ningekuwa mimi ningefuata ushauri wa Mbunge Lema.
 
Nakubaliana na Lema pale anaposema kuwa Kafulila anatakiwa kujirekebisha na sio kuhama chama. Call a spade a spade. Huyu Kafulila alifukuzwa CHADEMA kwa makosa haya haya yaliyomkumba huko NCCR.

Na mapema mwaka huku akiwa NCCR-Mageuzi alikuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kubadili kanuni za bunge ili tafsiri ya 'kambi rasmi' ibadilike, lengo likiwa ni kuhujumu CHADEMA.

Sasa, leo unamkaribisha CHADEMA kwa lipi? Ugonjwa ulimtoa CHADEMA umepona? Kama alileta vurugu CHADEMA, na huko NCCR-Mageuzi what makes you think he will behave differently this time around?
Kafulila hakufukuzwa CHADEMA alijiondoa mapema baada ya kuona mambo hayamwendei sawasawa, hakufukuzwa uanachama wala uongozi,. na swala la kuhama Lema hakutofautiana na Zitto ila amemshauri apumzike kwanza asikurupuke na ikibidi aombe msamaha, Kafulila ni mwanadamu ila ana papara sana papara ndizo zina m cost
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.

Mkuu, ungekuwa makini na real great thinker ungesoma na kuelewa kilichoandikwa na Mhe. Lema, siyo huo utumbo niliouwekea rangi nyekundu hapo juu. Quotes za watu wenye hekima waliopita ni kitu cha kawaida na huonesha kwamba muandishi aliyenukuu ana kumbukumbu na ufahamu kiasi gani, hadi kufikia kuoanisha tukio husika na nini watu werevu walipata kusema kuhusu tukio kama hilo. Lakini kwa kuwa uelewa wako ni finyu unadhani alichokifanya Mhe. Lema ni kusoma, kukariri na kuibilizia!!!
 
Nakubaliana na mawazo ya Lema! Na si kwa ushabiki wa kisiasa bali kwake yeye kuwa mwazi na mkweli! Lema anafahamu dhana dhaifu ya watanganyika tuliyo wengi kwemba tumeshapumbazwa na siasa hizi isiyo siasa inayotamalaki katika nchi yetu. Kwamba kanuni na taratibu zote karibia katika kila secta zimebaki kwenye makaratas tui! Mtu anapokosea badala ya watu kuangalia sheria husika inasemaje ktk kosa kama hilo, wanacho tanguliza kufikiria ni kwamba mtu huyo aliyetenda kosa ni wa hadhi gani. Wakiona si mlalahoi basi sheria hupindishwa. Kwa vyovyote vile Lema anafuraishwa sana namna NCCR kilivyofata taratibu na katiba yake. Na si kwamba amefurahia kufukuzwa kwa Kafulila! Huyo mheshima ametoa darasa makini hapa linalohotaji kuzingatiwa!!!

Hilo neno
 
yani pamoja na kua wewe ni mbunge wa chadema lkn unamshauri zaidi kuomba radhi kuliko kuja chama chenu? inaonekana huu ushauri ni wa kijasiri na umetoka moyoni wala si wakinafiki, napenda watu wenye kuelezea ukweli kama wewe bila kujali maslahi binafsi au ya chama, hongera sana muheshimiwa ingawaje sijui wanachama na viongozi wako watakuelwaje.

Ushauri wa kinafiki wala si ujasiri.Soma tena na utafakari“Mh.Zitto kakukaribisha CDM mimi nakukaribisha Arusha......
 
Unajua tabia za ushabiki hazina maana kabisa isipokuwa tazameni haki, kanuni na sheria zinazokuongoza hata wewe, Kesho unaweza kuwa ktk hali hii iliyomkuta Kafulila na ukajifunza mipaka na maeneo unayoweza kulitumikia Taifa au hata Chama...

Wengi wana hasira na Kafulila kuhama Chadema, hivyo hata akili zao zimefungwa kutolitazama swala hili vizuri na kulichambua, na wengine wanaliweka swala hili sawa na lile la madiwani wa Chadema kule Arusha bila kujali tofauti zilizopo. Binafsi sioni sababu kabisa ya Lema kujiingiza ktk swala hili isipokuwa nadhani kuna beef fulani ama karopoka bila kuelewa anasema nini kwa sababu zake mwenyewe.

Kafulila alifanya makosa ya Uongozi ndani ya Chadema akafukuzwa Uongozi na ndivyo ilivyotakiwa kufanyika NCCR - MAGEUZI japokuwa mimi naamini kabisa kwamba kiongozi wako anapokosea usisubiri hadi vikao vya chama wakati anauza chama maana inaweza kuwa too late kurekebisha na kuweza kufanya la maana. Kama Leo Mbowe anakiuza chama mimi naomba kabisa na nitamheshimu mtu anayekuja hapa na kuzungumzia mabaya ya Mbowe hadharani na sii kusubiri vikao vya chama maana hii itakuwa kuiga mfumo wa CCM..Na siku za nyuma wametokea wengi tukabishana weee lakini sijasikia mtu kafukuzwa uanachama.

Huku majuu Obama akionyesha mwelekeo usiopendeza kwa chama ama sio mwelekeo wa chama kisera, hupakwa na maseneta waziwazi, tena vyombo vya habari huwaita viongozi hao ktk Luninga na wakazungumza kwa nini hawakubaliani na Obama. Majuzi tu kulikuwa na swala la Obama kukubali makato ktk matumizi ya Healthcare wajumbe wengi tu wa chama chake walieleza wazi wazi kwamba hawatapiga kura ya ndio kukubaliana na Obama kabla hata vikao havijafanyika. Na wengine kufikia kusema Obama hawakilishi mawazo ya wapiga kura (Democratic) na anakiuza chama...Bahati mbaya sikumbuki ni senate gani aliyasema haya lakini ilitokea..

Hivyo, Kwanza uongozi wa NCCR mageuzi ulitakiwa kufanya uchunguzi wa madai na sio kusikiliza hearsay maana kama hujamshika mtu na ngozi kwa mswahili huyo sio mwizi. Uchunguzi ulitakiwa na hata kama ingebainika Mbatia ama Kafulila mmoja wao ana makosa itategemea na makosa yenyewe maana kusema uongo inategemea na uzito wake. Pengine alichokifanya Mbatia hakikuwa na uzito kama alivyosema lakini kilitokea kama vile Obama alivyokubali kuuza Healthcare, lakini kufikia maamuzi ya kumfukuza mtu UANACHAMA hii inatakiwa lazima ifike ktk kuvunja KANUNI za UANACHAMA...

Wale Madiwani wa Arusha walivunja kanuni za chama kwanza kufanya maamuzi ya Uongozi wa Halmashauri na CCM, Na Pili wakavunja tena kanuni za Uanachama walipoambiwa na makao makuu wajitoe ktk Halmashauri ya Mji wakakataa hapa ina maana they are above the party kwa imani kwamba wao ni wawakilishi wa wananchi (Independent). Hivyo wale waliokubali kujitoa ingawa walikuwepo ktk maamuzi ya kwanza wamebakia wananchama isipokuwa wale waliokataa hata maamuzi ya kamati kuu ya chama ndio waliovuliwa Uanachama. Kafulila hakuambiwa ili abakie mwanachama anatakiwa kufanya kadhaa wakadhaa akapinga! Isipokuwa maamuzi ya kumfukuza chama yametokana na sijui kuvunja kanuni ya Uongozi ambayo inasema (pengine) - Hutakiwi kutokuwa na imani na Mwenyekiti - Mungu mtu..
 
Mkandara,

Mkuu wangu utapata shida sana kuwaelewesha baadhi ya watu.Thank you for your excellent post!
 
Mkuu Mkandara, hongera kwa mchango wako mrefu. Ila ninapata wasiwasi kidogo na uelewa wako kuhusu taasisi zenye katiba, kanuni na miongozo. Kwa sababu, mchango wako umejaa dhana kuliko ukweli, (angalia maeneo niliyoyawekea wino mwekundu). Kwanza kabisa niseme Mhe. lema alichokifanya ni kuchangia hoja kuhusu tukio la kufukuzwa uanachama wa NCCR-M kwa Mhe. Kafulila kama ambavyo wewe na mimi na wengineo walivyofanya. Sasa hiyo dhana ya bifu baina umeitoa wapi? Ni dhana.
Pili, kila taasisi ina katiba na kanuni zake zinazoongaza namna ya kurekebishana, sivyo kama unavyotaka wewe kwamba, mtu aseme au akosoe vyovyote na popote apendapo,???!!! Kisa nini? Ati Marekani nao wanafanya hivyo. Aliyekwambia Katiba ya NCCR-M ni ya kimarekani ni nani?
Lakini pamoja na yote hayo bado katika mchango wako unataja neno kanuni??? Nashindwa kukuelewa, kwa nini unajichanganya hivyo? Ni kweli huelewi maana ya neno kanuni??? Kama unaelewa kwa nini unalaumu kilichotokea. Aliyetendwa kama hakuridhika sheria zipo. Ikionekana zilivunjwa sheria zitamlinda.
 
Nimekubali mh.Lema G ni jembe si kwa CDM tu bali pia wanaAusha wote. Hongera kaka Tuko pamoja.
 
Special kwa Davild kafulila wenzetu mbele wanasema hivi "If u can not beat them, then join them" Omba msamaha na kubali kubali kuanza upya ukiwa safi.
 
hamna nidhamu ya kijinga kama hii,au kwa kuwa na nyie vidole juu (viwili) mlifukuza wenzenu kwa kusingiazia nidhamu?
 
Mkuu, ungekuwa makini na real great thinker ungesoma na kuelewa kilichoandikwa na Mhe. Lema, siyo huo utumbo niliouwekea rangi nyekundu hapo juu. Quotes za watu wenye hekima waliopita ni kitu cha kawaida na huonesha kwamba muandishi aliyenukuu ana kumbukumbu na ufahamu kiasi gani, hadi kufikia kuoanisha tukio husika na nini watu werevu walipata kusema kuhusu tukio kama hilo. Lakini kwa kuwa uelewa wako ni finyu unadhani alichokifanya Mhe. Lema ni kusoma, kukariri na kuibilizia!!!

Nadhani lengo la pasco lilikuwa kumdhalilisha Lema, hii ni tabia ile ile ya watu kutokubaliana na kuheshimu mawazo ya wengine, binafsi sikubaliani na mawazo ya Lema, lakini naheshimu mawazo yake na kimsingi amejenga hoja yake vizuri na nampongeza kwa hilo.
Kufukuzana si jambo jema hata kidogo hata kama kanuni zilifuatwa, ndiyo maana kuna suala la kuvumiliana wakati huo huo sote tukijifunza. katika hili la kafulila nadiriki kusema kwamba Busara ziliwekwa pembeni. Ni mategemeo yangu kwamba NCCR M. watarudi hatua moja nyuma na kusahau yaliyopita hatimaye kumsamehe kijana.
Lakini pia kwa nini tuiingize nchi kwenye gharama zisizo za msingi na zinazoweza kuepukika.ingekuwa vema tukawafikiria watanzania wanaotaabika kwa kukosa chakula, dawa, makazi bora na hata umeme, tukatumia japo hata busara kidogo kuahirisha maamuzi japo kwa miaka mitatu na nusu ili tusiingize Nchi kwenye gharama zisizotarajiwa. think of 19 billions of money!!!!
Ubinafsi ni kitu kibaya sana hata kama tunaamini demokrasia ina gharama zake.
 
ritz kajipange sawasawa ili ulinde heshima yako, usikurupuke,soma vizuri "MADINI" hayo yaliyotolewa na Mh.Lema! The man is unbiased indeed. Big up Lema!

Pilu,
Unaangaika bure na Lema, ndege wafananao ndio wanaruka pamoja...wewe ni pumba kama mbunge wako..

Huwezi kujisifia eti mimi ni mtu makini, kivipi kuiba magari?
 
Mkuu Mkandara, hongera kwa mchango wako mrefu. Ila ninapata wasiwasi kidogo na uelewa wako kuhusu taasisi zenye katiba, kanuni na miongozo. Kwa sababu, mchango wako umejaa dhana kuliko ukweli, (angalia maeneo niliyoyawekea wino mwekundu). Kwanza kabisa niseme Mhe. lema alichokifanya ni kuchangia hoja kuhusu tukio la kufukuzwa uanachama wa NCCR-M kwa Mhe. Kafulila kama ambavyo wewe na mimi na wengineo walivyofanya. Sasa hiyo dhana ya bifu baina umeitoa wapi? Ni dhana.
Pili, kila taasisi ina katiba na kanuni zake zinazoongaza namna ya kurekebishana, sivyo kama unavyotaka wewe kwamba, mtu aseme au akosoe vyovyote na popote apendapo,???!!! Kisa nini? Ati Marekani nao wanafanya hivyo. Aliyekwambia Katiba ya NCCR-M ni ya kimarekani ni nani?
Lakini pamoja na yote hayo bado katika mchango wako unataja neno kanuni??? Nashindwa kukuelewa, kwa nini unajichanganya hivyo? Ni kweli huelewi maana ya neno kanuni??? Kama unaelewa kwa nini unalaumu kilichotokea. Aliyetendwa kama hakuridhika sheria zipo. Ikionekana zilivunjwa sheria zitamlinda.
Shukran sana na asante kwa kunisoma na kunielwa kisha umenipa nafasi ya kujibu hoja zako..Huu ndi ustaarabu..

Kwanza kabisa unasema kweli kabisa kwamba mimi sina ueweo mkubwa wa taasisi zenye katiba, kanuni na miongozo maana sii mwanachama wa taasisi hizo unless niptie na kuzisoma na muhimu zaidi kama zinanihusu..Nilichoandika hakitokani na dhana bali nashindwa kuelewa huyu Lema pamoja na ueleo wake umekuwaje kunigilia katiba, kanuni na miongozo ya chama ambacho yeye sii mwanachama wakati anajua fika taasisi, kanuni na miongozi hiyo hiyo ndio ilomlinda Kafulila asifukuzwe UANACHAMA akiwa Chadema hadi alipojiengua mwenyewe na kuingia NCCR.

Lema hazungumzia kama mimi wala wewe ingawa sikujui isipokuwa anazungumza kama mwanasiasa na mwanachama kiongozi wa Chadema. Hii inamweka mahala pabaya sana kisiasa hivyo hakutakiwa kutoa mawazo yoyote ya kichama maana alichoandika yeye kilitakiwa kuandikwa na kiongozi wa NCCR sio yeye..Halafu hakuna chama hata kimoja acha vya siasa hata vya kijamii iwe Yatch Club au cha masusi, mwanachama hawezi kufukuzwa kwa kusema makosa yanayofanyika na Uongozi au kiongozi mmoja...

Vyama vyote hutafuta wanachama kama mtaji wao, wananchama ni investment hivyo huwezi kuichezea hovyo isipokuwa tu kama mwanachama huyu atakiuka kanuni za chama na sii mwenyekiti au viongozi..Kafulila ndiye aliongea kama mwanachama na sii Kiongozi lakini Mbatia ali act kama Mwenyekiti hakuna cha kuiga Marekani wala Kenya. Huwezi kumfukuza mtu uanachama kwa makosa ya kiuongozi ila unamwondoa Uongozini kwisha na kama lipo swala kubwa la uvunjaji kanuni inabidi upelelezi kutafuta ukweli na sio hearsay kuchukuliwa kama ushahidi tosha wa ku vote kumvua mtu uanachama..

Pima kitu hiki:- Hivi ili wewe ufikie kuvuliwa Uraia wako unatakiwa kufanya makosa gani? Je, kuna kanuni gani za kisheria ambazo zinaweza kukuondoa wewe ktk uraia...Je, kutokuwa na imani na rais mathlan JK kunaweza kukunyang'anya wewe uraia?.. huu ndio msingi alotumia Mbatia na kamati yake..
Kafulila alikosea na kitendo cha kumnyang'anya Uongozi tu kilitosha haiwezi kwenda hadi kumvua uanachama kwa sababu Ubunge wake ni mtaji kwa chama uwakilishi wa chama wanachama na wananchi wa jimbo hilo na wala hajakiuka kanuni za chama bado ni mtetezi wa chama bungeni na anafuata taratibu zote za sera za chama...Wewe Lema nani ndani ya NCCR hadi kusema yaliyofanyika ni sawa ili Kafulila ajifunze...

Pili, Katika swala la Chadema kuwafukuza madiwani nilisema wazi kwamba wamevunja kanuni za chama maana walikuwa tena hawawakilishi chama bali CCM hivyo wamevuka mpaka na kuvunja kanuni. Sasa wewe unayejua kanuni za NCCR nambie ama nionyeshe mahala inaposema mtu asipokuwa na confidence na kiongozi mwenyekiti afukuzwe uanachama. Ukinionyesha hilo tu sina maelezo zaidi na kama hutakuja na jibu hilo basi sina sababu ya malumbano..
 
kama sikosei magistu haile mariam (alipata kuwa raisi wa ethipia) alipofanya mapinduzi kwa kumuua aliyekuwa raisi
teferi bante na wenzake wakati wa mkutano wa baraza la mapinduzi alisema "those who wanted me for dinner i took them
for breakfast".

sasa inawezekana kafulila kawahiwa. yawezekana tuhuma zake dhidi ya mbatia zilikuwa na lengo la kumuondoa
mwenyekiti wake katika uongozi na hatimaye kumuondoa katika chama. katika hili inawezekana kabisa mbatia aliliona
hili hivyo akaamua kumuwahi kafulilaa kabla yeye mbatia (hajapigwa chini).

kama kweli mkakati wa kafulila ulikuwa kumng'oa mbatia madarakani na chamani akubali yaishi na ajitibu majeraha tuu.

pamoja na yote ni nadra sana kwa mtu kutamka hadharani kwamba yeye ni bora zaidi ya kiongozi wake na akasalimika.
pamoja na nguvu zote tunazoambiwa el anazo ndani ya ccm sijawahi msikia akisema yeye ni zaidi ya mwenyekti wake.
namshauri kafulila asome yaliyompata kanali ojok wa uganda.

pole sana kafulila ndio siasa hiyo
 
Vyama vyote hutafuta wanachama kama mtaji wao, wananchama ni investment hivyohuwezi kuichezea hovyo isipokuwa tu kama mwanachama huyu atakiuka kanuni zachama na sii mwenyekiti au viongozi..Kafulila ndiye aliongea kama mwanachama nasii Kiongozi lakini Mbatia ali act kama Mwenyekiti hakuna cha kuiga Marekaniwala Kenya. Huwezi kumfukuza mtu uanachama kwa makosa ya kiuongozi ilaunamwondoa Uongozini kwisha nakama lipo swala kubwa la uvunjaji kanuni inabidi upelelezikutafuta ukweli na sio hearsay kuchukuliwa kama ushahidi tosha wa ku votekumvua mtu uanachama..

Pima kitu hiki:- Hivi ili wewe ufikie kuvuliwa Uraia wako unatakiwa kufanyamakosa gani? Je, kuna kanuni gani za kisheria ambazo zinaweza kukuondoa wewektk uraia...Je, kutokuwa na imani na rais mathlan JK kunaweza kukunyang'anyawewe uraia?.. huu ndio msingi alotumia Mbatia na kamati yake..
Kafulila alikosea na kitendo cha kumnyang'anya Uongozi tu kilitosha haiwezi kwenda hadi kumvua uanachamakwa sababu Ubunge wake ni mtaji kwa chama uwakilishi wa chamawanachama na wananchi wa jimbo hilo na wala hajakiuka kanuni za chama bado nimtetezi wa chama bungeni na anafuata taratibu zote za sera za chama...Wewe Lema nani ndani ya NCCR hadikusema yaliyofanyika ni sawa ili Kafulila ajifunze...
Mkandara, yaya alikuuliza jambo moja la msingi kabisa kama unajua umuhimu wa katiba, kanuni na miongozo katika vyama vya siasa. Unaweza kutuambia ni ngazi gani mathalani ndani ya NCCR-M inayoweza kumvua uanachama mwanachama wake au ukishakuwa mwanachama basi huwezi kufukuzwa.

Ieleweke hapa sitetei chama wala Kafulila natetea principles, ilichokifanya NEC ya NCCR ni kutafsiri kanuni na miongozo ya chama na ikaonekana Kafulila kakiuka misingi ya katiba yao na kulingana na katiba yao inakiruhusu kikao kumvua uanachama mtu yeyote regardless ya wadhifa wake sasa hapo kosa liko wapi, hapa ndipo Lema anaposimamia. Kama ni kosa si la chama kama chama bali ni la mjumbe mmoja mmoja ndipo hapa linakuja suala la maadili ya wajumbe na Mbatia inclusive.

Vyama havianzishwi ili kupata wabunge vinaanzishwa ili viongoze watu kwa hiyo hakiwezi kusita kumfukuza mtu kama ni mtovu wa nidhamu kwa vile tu yeye ni mwakilishi afterall yeye ndiye alitakiwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa jamii. Kuhusu Lema, umeuliza amesema kama nani ndani ya NCCR je wewe unasema kama nani, hayo ni mawazo yake tu kama yalivyo yako na kuwa kiongozi haufungwi kuwa na mawazo binafsi, halafu nawashangaa sana watu wanaodai freedom of expression ilhali linapokuja suala la Lema wanasahau kama na yeye anahitaji hiyo freedom of expression.
 
Back
Top Bottom