Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

duh!!! nadhani weengi mliosoma hii hamjaelewa mh lema......lema anasoma sana filisofia za ukombozi!!!

huyu jamaa ni hatari sanaaaaaa..... mbaya zaidi ni mwanafalsafa...........hadi leo hii watu wanapambana kuelewa Yesu alikuwa anamaananisha nini kila alipokuwa akiongea.....

hii barua si ya kusoma juu juu....kimsingi lema amezungumzia mambo kadhaa kama vile...

1. chama kama nccr si chama makini kupewa dola.....kinapaswa kujitafakari juu ya uwepo wake....

2. kafulila anapaswa kutafakari nafasi yake ndani ya chama......

3. kafulila kama kijana yeyote anapaswa kuwa mwerevu na kujua chess za siasa, na kufahamu adui yake anafikiria nini......

4. nidhamu katika vyama ni msingi kwa ajili ya kujenga taifa lenye nidhamu, ikiwemo CCM na Chadema......

tuendelee....
 
Safi sana Mh lema for good advice to Mr kafulila,nidhamu ni kitu muhimu sana,Chadema ulileta vurugu ukakimbia na sasa umeenda NCCR hata mwaka hujaisha nako umeleta vurugu umefukuzwa,unaonekana unamatatizo,huna cha kujitetea zaidi ya kubadilika.
 
duh!!! nadhani weengi mliosoma hii hamjaelewa mh lema......lema anasoma sana filisofia za ukombozi!!!

huyu jamaa ni hatari sanaaaaaa..... mbaya zaidi ni mwanafalsafa...........hadi leo hii watu wanapambana kuelewa Yesu alikuwa anamaananisha nini kila alipokuwa akiongea.....

hii barua si ya kusoma juu juu....kimsingi lema amezungumzia mambo kadhaa kama vile...

1. chama kama nccr si chama makini kupewa dola.....kinapaswa kujitafakari juu ya uwepo wake....

2. kafulila anapaswa kutafakari nafasi yake ndani ya chama......

3. kafulila kama kijana yeyote anapaswa kuwa mwerevu na kujua chess za siasa, na kufahamu adui yake anafikiria nini......

4. nidhamu katika vyama ni msingi kwa ajili ya kujenga taifa lenye nidhamu, ikiwemo CCM na Chadema......

tuendelee....

Yesu tena kwenye mambo ya vyama?
 
Hii ndio Democracy kueleza kile unachodhani ni sahihi - (Freedom of speech),ila kwa hili Mh.Lema nimekutoa from Hero to Zero,mimi sio mshabiki sana wa siasa ila nikisoma hii kitu yako naona kama mna kaugomvi fulani na Mh.David Kafulila...ni mawazo yangu tu.
 
Olanganyira akashwahili tinkamanyage! ka kitali kipaji ebyoyagamba byona iwe wakubikariri alafu obigamba okwo bili? pamoja ne ekipaji lazima ne ejuhudi zibeo! bati Mungu mbela naiwe otaileo agae!
Kama nakumbuka mahali, ni kosa kutumia native venaculars humu!
 
Du, mambo ya kosoma kukariri na kuibilizia!, ...kaazi kweli kweli!.

Mhe. Godbless Lema, katika hili la Kafulila.... Bure Kabisa!.
Humu ndani kuna watu kama ifuatavyo;
  1. Thinkers wa kuibua hoja
  2. Wataalam wa kuchangia hoja
  3. Mabingwa wa kukosoa hoja endapo haitakuwa sawa na mitizamo yao
  4. Wazee wa ku-like
  5. Wasomaji with no comment.
Kwa mtizamo wangu ni kwamba kama mtu katoa hoja ambayo haina mashiko au mvuto kwako BINAFSI hunasababu ya kuanza kumponda bali wewe elezea unachoona ni kizuri zaidi ya kile alichoeleza yeye ili sisi wasomaji tufahamu zaidi nadhani hiyo ndiyo maana halisi ya great thinkers. Ninachofaham mimi what is good to you is not necessary to be good to me, and vice versa!
Ikitokea nimesoma hoja yoyote isiyoendana na kile ninachoamini mimi huwa ninasoma tu kisha naipotezea na ikitokea imekuwa na mashiko nitachangia au kama kuna aliyechangia kinachofanana na mtizamo wangu basi huwa nina like tu kisha naenda zangu. Nakushauri uige mfano huu mkuu japo sio shurti
 
duh!!! nadhani weengi mliosoma hii hamjaelewa mh lema......lema anasoma sana filisofia za ukombozi!!!

huyu jamaa ni hatari sanaaaaaa..... mbaya zaidi ni mwanafalsafa...........hadi leo hii watu wanapambana kuelewa Yesu alikuwa anamaananisha nini kila alipokuwa akiongea.....

hii barua si ya kusoma juu juu....kimsingi lema amezungumzia mambo kadhaa kama vile...

1. chama kama nccr si chama makini kupewa dola.....kinapaswa kujitafakari juu ya uwepo wake....

2. kafulila anapaswa kutafakari nafasi yake ndani ya chama......

3. kafulila kama kijana yeyote anapaswa kuwa mwerevu na kujua chess za siasa, na kufahamu adui yake anafikiria nini......

4. nidhamu katika vyama ni msingi kwa ajili ya kujenga taifa lenye nidhamu, ikiwemo CCM na Chadema......

tuendelee....
Sidhani kama umemsoma vizuri... ebu nitafsirie hapa alikuwa na maana gani..

Lema anasema:-
Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi**kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba**“ Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa,**Binafsi**sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama**kinachukuwa**taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa.
 
Lema ndio kaandika ule upupu? Hivi kiwango cha elimu ya Lema ni kipi kabla sijachangia nataka kujua...sijuhi kwa nini umeweka hizi dot***
Ni upupu kwa nyie ccm, maana nyie mnawekeana zamu kula nchi kwa hiyo hamuwezi kulinda nidhamu ila mtalinda maslahi yenu.
Safi sana Lema tunahitaji viongozi wanaojua wanachokipigania na wapo tayari kupigania bila kuona aibu. Kafulila lazima ajue kuwa kinachotofautisha vyama ni sera na kwahiyo kama aliona sera za Chadema hazifai ila zile za NCCR ndio zinazomfaa basi anatakiwa kuzipigania kwa kubaki ktk chama chake na sio kwenda tena kwenye chama kilicho na sera asizoziamini. Akishindwa kubaki NCCR basi dawa ni kuanzisha chama kinachoendana na sera anazoziamini.
 
Hii ndio Democracy kueleza kile unachodhani ni sahihi - (Freedom of speech),ila kwa hili Mh.Lema nimekutoa from Hero to Zero,mimi sio mshabiki sana wa siasa ila nikisoma hii kitu yako naona kama mna kaugomvi fulani na Mh.David Kafulila...ni mawazo yangu tu.
Wewe sio tu kuwa sio mshabiki bali pia hujui maana ya chama cha siasa ndo maana kwako wewe cha msingi ni kuwa na mbunge bila kuangalia itikadi yake. ndo nyie mnaosema vyama vya upinzani viungane, sijui kwanini hamshauri pia kuwa dini ziungane ili tuwe na dini moja.
 
Nimejaribu kuupitia huo waraka. Nimeshindwa kupata malengo yake hasa yalikuwa nini. Naona kama amejaribu kuegemea pande zote.

Kama ameamua kuzungumza kwanini asiwe wazi. Mbona kama anazunguka zunguka!

Pia ktk swala la kujisifu, ameamua kidogo kujipa promo. Amejiita kiongozi makini. Kiongozi makini anahamasisha maandamano yasiyo na kichwa wala miguu. Vigezo gani alivyotumia kuji-asses.

NB.
Swala la uandishi halipo po, sijui hizo * zinamaanisha nini.
 
Lema ndio kaandika ule upupu? Hivi kiwango cha elimu ya Lema ni kipi kabla sijachangia nataka kujua...sijuhi kwa nini umeweka hizi dot***

ritz kajipange sawasawa ili ulinde heshima yako, usikurupuke,soma vizuri "MADINI" hayo yaliyotolewa na Mh.Lema! The man is unbiased indeed. Big up Lema!
 
Nimejaribu kuupitia huo waraka. Nimeshindwa kupata malengo yake hasa yalikuwa nini. Naona kama amejaribu kuegemea pande zote.

Kama ameamua kuzungumza kwanini asiwe wazi. Mbona kama anazunguka zunguka!

Pia ktk swala la kujisifu, ameamua kidogo kujipa promo. Amejiita kiongozi makini. Kiongozi makini anahamasisha maandamano yasiyo na kichwa wala miguu. Vigezo gani alivyotumia kuji-asses.

NB.
Swala la uandishi halipo po, sijui hizo * zinamaanisha nini.

Hujaelewa nini sasa acha mambo yako wewe, afu jiheshimu ,unaposema anachochea "maandamano yasio na kichwa wala miguu" vinahusiana vp na swala la kafulila kama mada husika.Nawasiwasi na wewe!
 
duh!!! nadhani weengi mliosoma hii hamjaelewa mh lema......lema anasoma sana filisofia za ukombozi!!!

huyu jamaa ni hatari sanaaaaaa..... mbaya zaidi ni mwanafalsafa...........hadi leo hii watu wanapambana kuelewa Yesu alikuwa anamaananisha nini kila alipokuwa akiongea.....

hii barua si ya kusoma juu juu....kimsingi lema amezungumzia mambo kadhaa kama vile...

1. chama kama nccr si chama makini kupewa dola.....kinapaswa kujitafakari juu ya uwepo wake....

2. kafulila anapaswa kutafakari nafasi yake ndani ya chama......

3. kafulila kama kijana yeyote anapaswa kuwa mwerevu na kujua chess za siasa, na kufahamu adui yake anafikiria nini......

4. nidhamu katika vyama ni msingi kwa ajili ya kujenga taifa lenye nidhamu, ikiwemo CCM na Chadema......

tuendelee....

heshima kwako mkuu!
 
. Swali la mwisho, Je does the punishment fit the crime? ...I don't think so, it's too harsh.
Hii ndiyo hoja ambayo wengi wetu imetutumbukia nyongo. Adhabu aliyopewa kafulila ni ya kikatili sana na yenye kuonyesha watoaji wana hofu naye kama akiendelea kukaa karibu yao.

Mambo mengi aliyokuwa anayafanya Kafulila akiwa Mbunge nilikuwa sikubaliana naye, lakini adhabu aliyopewa ndiyo sikubaliani nayo kabisa!!
 
Hujaelewa nini sasa acha mambo yako wewe, afu jiheshimu ,unaposema anachochea "maandamano yasio na kichwa wala miguu" vinahusiana vp na swala la kafulila kama mada husika.Nawasiwasi na wewe!

nimekusoma ndg.

Naomba unijibu hili swali. Je! Lengo kuu la waraka wake ni nini?.

Hapo mwisho, jamaa amejisifu kuwa yeye ni kiongozi makini. Umakini wake uko wapi?. Amefanya kipi cha kudhibitisha umakini wake?
 
Wewe sio tu kuwa sio mshabiki bali pia hujui maana ya chama cha siasa ndo maana kwako wewe cha msingi ni kuwa na mbunge bila kuangalia itikadi yake. ndo nyie mnaosema vyama vya upinzani viungane, sijui kwanini hamshauri pia kuwa dini ziungane ili tuwe na dini moja.

Chama cha siasa sio baba wala mama,na pia sio dini ni muunganiko wa watu wenye common interest...kwa hili unatakiwa kumuangalia mara mbili mwanamapinduzi uchwara lema,wahenga walisema ngoma ikilia sana ujue inakaribia kupasuka,lema anakaribia kupasuka kisiasa soma vizuri hauhitaji PHD kuelewa nini au anafikir nini wakati anaandika.Jamaa nilikua namkubali sana ila kwa hili kaangukia nose.
 
nimekusoma ndg.

Naomba unijibu hili swali. Je! Lengo kuu la waraka wake ni nini?.

Hapo mwisho, jamaa amejisifu kuwa yeye ni kiongozi makini. Umakini wake uko wapi?. Amefanya kipi cha kudhibitisha umakini wake?

Mzee ni hivi kwa kifupi kupitia wakala wake Mh.Lema kaonyesha yafuatayo;-
1] ni vema chama kua tayari kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya chama na wananchi pale inapobidi, ndomana kawapongeza nccr, pia hata wao cdm waliyaweza hayo kwa kuwatimua madiwani kadhaa , nasio kama magamba sugu walivoshindwa kufanya maamuzi magumu.
2]pia kamtia nguvu kafulila kwa kumjuza kua katika jambo lolote kuna mambo makuu mawili so unapokutana na changamoto ni vema kutafakari yaliyokufikisha katika hizo changamoto ili ujue njia sahihi kama mfano kufukuzwa kwa kafulila atazame sababu then awe makini katika maamuzi atakayofikia na ndomana tofauti na Mh.zitto yeye kamanda Lema kamkaribisha kafulila Arusha akapumzike na kutafakari uelekeo wake katika ndoto zake za kisiasa.
3]pia Mh.LEMA kaonyesha uzalendo wa hali ya juu na sio ushabiki tu yani yuko unbiased.

Mbali na mengi alofanya Arusha yeye mh.lema binafsi pia kupitia madiwani, pia amekua ni chachu au role model{pamoja na kusakamwa napolisi} kwa vijana,so wanachapa kazi wakiamini watafikia malengo yao.
So kwa kifupi anasababu zooote za kujiita kiongozi makini upo hapo!!
So an
 
Kama nakumbuka mahali, ni kosa kutumia native venaculars humu!

Waimukayo waitu, shumalamu! " kwa maana hiyo kama hukumbuki mahali itakuwa sio kosa" kweli wakoloni wamekupumbaza kabisa ww! ipende lugha yako! iwe oli wo owaitu anga munyamaanga?
 
Soma kisha tafakari........*

*“Nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge**David**Kafulila na nilipata fursa**ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa Jamii Forum na kuona mawazo ya**Watanzania mbali mbali juu ya jambo hili.

Na ninafikiri ninao wajibu**kama kijana tena Mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta Mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana Bwana David Kafulila.

“ Kwanza kabisa Bwana David Kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo , utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa**changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye**hekima zaidi**kwani katika kila changamoto kubwa Duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea Duniani.

*Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi**kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba**“ Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa,**Binafsi**sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama**kinachukuwa**taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa.

Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini David katika maisha ya siasa na Nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio**na hauwezi kuviepuka**ndio maana , Mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa “ huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na**baadae vifaranga watatotolewa.

Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena**“ haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia “ kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni*muhimu katika kufikia malengo makuu.

Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu**na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu**? na vile vile tufikirie kama leo Mbunge au Diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu**nidhamu ndani ya vyama vyao**,je*vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?

NCCR Mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ? Kama nafasi ya Ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi**dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ?

**sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya Ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia**njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? nina wasi wasi kuwa**siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa**na**waziri Mkuu wa Uingereza ili muweze**kula lakini**kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .

Hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio**kuwa ni**pamoja na**nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji**yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu,**Na ni hatari**wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala , kwani ugomvi wetu**vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera**bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea Taifa madhara makubwa.

*Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa David , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha**na jambo la kushangaza hapa,**ni kwanini watu wameshituka sana Mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini Mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu**, hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua**sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana ,
Sasa nimalizie kwa kusema**David bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi**kama,**Martin Luther King Jr.**alivyopata*kunena***“*The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.

Naibu Katibu mkuu wetu Mh Zitto nimesoma habari mbali mbali kuwa amekukaribisha Chadema ,**lakini mimi kwa sasa**nakukaribisha**Arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama Chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ?

Mfano ,ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi Mungu lakini**pia itakupasa kwenda Hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama Chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio Mbunge tena

*“Jipe moyo David Kafulila na Hongera NCCR-MAGEUZI. . Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa**“ THE 21 MOST POWERFUL MINUTES IN A LEADERS DAY “ Kilichoandikwa na na mwandishi maarufu “ John C. Maxwell.
*
If you are a leader , it’s not enough to know what to do . You have to know when to act. “ John C. Maxwell.

Godbless Lema . (Mb)

"Eibara libi lita nyinalyo" KAFULILA ameFULIA
 
Km unasoma ili ukalili bas kalili vizur ili unapokisema au kukiandika ili wenzako wasome kiwe hakijakosewa,hata mimi siung mkono mawazo ya lema.hatutaki wanasiasa wenye nidhamu ya uoga kwa mabos wao
Libasket,elewa basi anachosema mtu.siyo unajifanya kuelewa halafu mwenyewe unatoa upupu.lema anachoongea ni umuhimu wa taasisi dhidi ya mtu.Kafilila nccr ilimjenga alipotoka chadema,sasa alitaka aiharibu.upuuzi kabisa. kama mbatia ana kasoro anzisha thread tofauti tujadili.makosa ya kafulila hayahalalifshi ya kafulila.unaposema mabosi unaonyesha usivyoelewa topic ya lema. sasa utamkosoa vipi
 
Back
Top Bottom