Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Soma kisha tafakari........*

*“Nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge**David**Kafulila na nilipata fursa**ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa Jamii Forum na kuona mawazo ya**Watanzania mbali mbali juu ya jambo hili.

Na ninafikiri ninao wajibu**kama kijana tena Mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta Mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana Bwana David Kafulila.

“ Kwanza kabisa Bwana David Kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo , utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa**changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye**hekima zaidi**kwani katika kila changamoto kubwa Duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea Duniani.

*Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi**kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba**“ Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa,**Binafsi**sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama**kinachukuwa**taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa.

Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini David katika maisha ya siasa na Nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio**na hauwezi kuviepuka**ndio maana , Mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa “ huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na**baadae vifaranga watatotolewa.

Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena**“ haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia “ kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni*muhimu katika kufikia malengo makuu.

Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu**na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu**? na vile vile tufikirie kama leo Mbunge au Diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu**nidhamu ndani ya vyama vyao**,je*vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?


NCCR Mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ? Kama nafasi ya Ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi**dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ?

**sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya Ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia**njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? nina wasi wasi kuwa**siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa**na**waziri Mkuu wa Uingereza ili muweze**kula lakini**kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .


Hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio**kuwa ni**pamoja na**nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji**yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu,**Na ni hatari**wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala , kwani ugomvi wetu**vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera**bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea Taifa madhara makubwa.

*Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa David , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha**na jambo la kushangaza hapa,**ni kwanini watu wameshituka sana Mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini Mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu**, hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua**sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana ,
Sasa nimalizie kwa kusema**David bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi**kama,**Martin Luther King Jr.**alivyopata*kunena***“*The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.

Naibu Katibu mkuu wetu Mh Zitto nimesoma habari mbali mbali kuwa amekukaribisha Chadema ,**lakini mimi kwa sasa**nakukaribisha**Arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama Chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ?

Mfano ,ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi Mungu lakini**pia itakupasa kwenda Hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama Chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio Mbunge tena


*“Jipe moyo David Kafulila na Hongera NCCR-MAGEUZI. . Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa**“ THE 21 MOST POWERFUL MINUTES IN A LEADERS DAY “ Kilichoandikwa na na mwandishi maarufu “ John C. Maxwell.
*
If you are a leader , it’s not enough to know what to do . You have to know when to act. “ John C. Maxwell.

Godbless Lema . (Mb)
 
umenena kaka ila mbatia naye si mungwana katika kukuza upinzani hata kidogo anatumika sana na ccm
 
Nakubaliana na Lema pale anaposema kuwa Kafulila anatakiwa kujirekebisha na sio kuhama chama. Call a spade a spade. Huyu Kafulila alifukuzwa CHADEMA kwa makosa haya haya yaliyomkumba huko NCCR.

Na mapema mwaka huku akiwa NCCR-Mageuzi alikuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kubadili kanuni za bunge ili tafsiri ya 'kambi rasmi' ibadilike, lengo likiwa ni kuhujumu CHADEMA.

Sasa, leo unamkaribisha CHADEMA kwa lipi? Ugonjwa ulimtoa CHADEMA umepona? Kama alileta vurugu CHADEMA, na huko NCCR-Mageuzi what makes you think he will behave differently this time around?
 
Km unasoma ili ukalili bas kalili vizur ili unapokisema au kukiandika ili wenzako wasome kiwe hakijakosewa,hata mimi siung mkono mawazo ya lema.hatutaki wanasiasa wenye nidhamu ya uoga kwa mabos wao
 
Du! Ama kweli dunia duara, wabunge ni wawakilishi na sio leaders sema wanaharibu zaidi wanavyojitahidi kujitwika uongozi na kusahau uwakilishi ndio maana wametufikisha hapa tulipo.
Wengi wanakosa qualities za kuwa leaders DK na GL ni mifano tu, Fayol alitoa 14 principles waanza kujipima nazo
 
Pasco huwezi kumwelewa Lema; yuko juu kidogo (samahani, sio kama nakudharau). Unafikiria kibinadamu sana na kufanya kila kitu hivo hovyo kibinadamu sana; lakini jamaa naona anafikiria ktk super power zaidi (Kimungu mungu). Sawa tu na fikra ya jamaa aliyelewa kilabuni tofauti na mtu anaye concetrate for a purpose. Once again hongera Mbunge ambaye hakina kuna kitu umekisimamia na umeendelea kukisimamia- "Kweli daima inakuweka huru" no matter how thorn to others the issue is. Thanks Lema
 
yani pamoja na kua wewe ni mbunge wa chadema lkn unamshauri zaidi kuomba radhi kuliko kuja chama chenu? inaonekana huu ushauri ni wa kijasiri na umetoka moyoni wala si wakinafiki, napenda watu wenye kuelezea ukweli kama wewe bila kujali maslahi binafsi au ya chama, hongera sana muheshimiwa ingawaje sijui wanachama na viongozi wako watakuelwaje.
 
Nilisoma kwenye magazeti kufukuzwa kwa huyu bwana! so sina uhakika sana na matukio halisi yaliyotokea!
Binafsi kilichonisikitisha ni pale niliposoma kuwa alilia na kuomba msamaha walipotangaza kumfukuza! Mimi naamini kuwa kama alikuwa sahihi basi alipaswa kusimamia kwenye huo ukweli hata alipofukuzwa. kwangu, kuomba msamaha unapokuwa uko sahihi ni dalili ya kutokuwa na msimamo, na ni unafiki!
 
Nakupongeza kwa ushauri muhimu saana si 2 kwa Kafulila na sisi wenye kulinda na kushabikia uovu Thnx G Lema MB
 
Nakubaliana na mawazo ya Lema! Na si kwa ushabiki wa kisiasa bali kwake yeye kuwa mwazi na mkweli! Lema anafahamu dhana dhaifu ya watanganyika tuliyo wengi kwemba tumeshapumbazwa na siasa hizi isiyo siasa inayotamalaki katika nchi yetu. Kwamba kanuni na taratibu zote karibia katika kila secta zimebaki kwenye makaratas tui! Mtu anapokosea badala ya watu kuangalia sheria husika inasemaje ktk kosa kama hilo, wanacho tanguliza kufikiria ni kwamba mtu huyo aliyetenda kosa ni wa hadhi gani. Wakiona si mlalahoi basi sheria hupindishwa. Kwa vyovyote vile Lema anafuraishwa sana namna NCCR kilivyofata taratibu na katiba yake. Na si kwamba amefurahia kufukuzwa kwa Kafulila! Huyo mheshima ametoa darasa makini hapa linalohotaji kuzingatiwa!!!
 
Du! Ama kweli dunia duara, wabunge ni wawakilishi na sio leaders sema wanaharibu zaidi wanavyojitahidi kujitwika uongozi na kusahau uwakilishi ndio maana wametufikisha hapa tulipo.
Wengi wanakosa qualities za kuwa leaders DK na GL ni mifano tu, Fayol alitoa 14 principles waanza kujipima nazo
Baba au labda kaka,kwanza kabisa kubali kuwa hujielewi na hiyo imekufanya usieleweke. Hivi unaelewa vigezo vinavyompa mtu sifa ya kuwa kiongozi? Naamini huelewi. Nijuavyo [ki mantiki]tukiwa kama group lenye watu kumi wenye nia moja ya kutatua tatizo/matatizo. Tuliyonayo. Kwa muda husika. Ni uungwana usiopingika kuweka utaratibu utakaotupeleka kwenye utatuzi wa tatizo husika. Na hii hujumuisha. Mawazo ya mtu mmojammoja,yatakayo zaa maamuzi ya kundi husika,na kama kuna sababu/umuhimu wa kutafuta mtu m1 kuwakilisha mawazo yetu basi mtu huyo hakika atakuwa mwakilishi wetu. Ila baada ya kutuwakilisha haitamaanisha kuwa kazi yake imeishia hapo. Bali ataitajika/lazimika. Kutuongoza katika utaratibu.wa hatua inayofuata ya. Utekelezaji wa matokeo ya uwakilishi wake kwetu. Hapo ndipo dhana ya uongozi inapopata mashiko. So since then hutaweza kamwe kutenganisha. Ubunge na. Uongozi kama unavyojaribu sasa.
 
Nakubaliana kwa kipengele kimoja kwamba vyama vya upinzani vinataka kurejesha nidham na uwajibikaji vilivyopotea ndani ya chama tawala.Kujivua gamba kuliyeyuka maana gamba gumu halikuguswa yaani mkulu.Wakamsingizia kiongozi shupavu lowasa eti ni gamba.Ilikula kwao pale EL alipofunguka kwamba yeye alishabaani siku nyingi kuwa richmondi ni feki lkn mkulu ndo alositisha kufutwa kwake.So maadili na uwajibikaji ni mhinu
 
Back
Top Bottom