Jipe moyo Kafulila; Hongera NCCR-Mageuzi, Godbless Lema

Kwani mbunge ni kamusi ya watu wote au yeye akisema wengine wote wawe kimya. Mimi hoja yangu kwenye suala hili ni hii. NCCR - Mageuzi wamekosea kumfukuza chama Kafulila njia sahihi ni ile waliyoitumia kwa Felix Mkosamali. Kwani adhabu zote ni ile ya kumfukuza chama Kafulila?

Tanzania tunaanza kujenga tabia ya viongozi wenye nafasi za kitaifa kutokupingwa. Kwenye vyama vyote vya siasa wenyeviti "hawagusiki" na tabia hii inakuzwa na vibaraka wa viongozi hao wanaotumia vyombo vya habari na mitandao jamii kuwachafua wale wenye mawazo tofauti na viongozi wanaowashabikia.

Kafulila kosa lake ni kusema Mbatia hafai na kuonana na Kikwete ni kufanya makosa. Kwangu mimi haya si makosa ya kumfukuza mtu chama na kusababisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo ambao naamini NCCR hii haiweze kushinda hata kwa dawa na kwa tabia za Mbatia ufa kati ya CHADEMA na NCCR utazidi kuongezeka.

NCCR walipaswa kumvua Kafulila vyeo vyote vya kichama na kumweka kwenye uangalizi kwa kipindi fulani kabla ya kumruhusu kugomb ea vyeo vya kichama. Lakini kumvua uanachama ni ujuha uliopindukia na ushamba wa matumizi wa madaraka. Hivi vikao vinavyoitwa Halmashauri/Baraza Kuu vya hivi vyama vyetu vyenyewe havijitambui.

Wakati mwingine unaweza kujiuliza ilikuwaje Halmashauri Kuu ya TLP iliruhusu kutungwe Katiba inayompa madaraka Mwenyekiti wa chama kumfukuza mtu kwenye nafasi ya uongozi au uanachama bila ya kupitia kikao chochote. Ni madudu mangapi yanafanyika kwenye Halmashauri kuu ya CCM, ni mambo mangapi hayajadiliwi kina kwenye Baraza Kuu la CHADEMA ua CUF?

KAFULILA KAHUKUMIWA KWA NJIA HALALI LAKINI ADHABU ALIYOPEWA NI YA UONEVU!!

Sio uasi?
 
Binadamu wanapenda kusikia au kuambiwa mazuri tu na pindi anapoambiwa ukweli anamchukia mtoa ukweli.Magamba.com ni matokeo wa huu mfumo wa kutotaka kusema ukweli..............
ukomavu katika jambo lolote ni kusimamia ukweli daima, kama ulisema hili ni jembe na ukapewa adhabu kwa kusema hivyo,

Mytake: Nini maana ya kuomba msamahaa baada ya hukumu kutoka:
  1. Umegundua kuwa ulikosea kusema Jembe?
  2. Na umekubali kuwa hilo siyo Jembe ni Shoka
kwa maana hiyo ulikuwa una testi kiberiti kama kilikuwa kimejaa?Ni vizuri kama aliona kuwa yale haliyoyasema halikuwa yupo sahihi hakukuwa na haja ya yeye kuomba msamaha coz alitafakari kabla hajasema.

Lema ameeleza ukweli ambao wengi wetu hatupendi kuusema zaidi ya kutoa sifa za kijinga.
Hili la Kafulila kuomba radhi mimi binafsi nalielewa. Yeye alipoingia kwenye kikao alidhani siasa za hoja zina nafasi kwenye vikao vya vyama vyetu kumbe kinyume chake siasa za mikakati ndiyo nguzo zinazohimili nguvu ya ushawishi ndani ya vyama hivi. Hapa tunaweza kujifunza kwa Mutungirehi, Salim Ahmed Salim, Chacha Wangwe, Kolimba na wengineo.

Siamini kama Kikwete anamzidi uwezo wa kiuongozi Salim, lakini mikakati ilimweka Kikwete kwenye Uongozi na kumtupa pembeni Salim. Ndani ya kile kikao Kafulila aligundua hakuna hata mtu mmoja (Zaidi ya kundi la kina Rungwe) aliyetayari kumuunga mkono kweye madai yake dhidi ya Mbatia. Kafulila badala ya Ku - retreat yeye aka - capitulate. Kwangu mimi kuomba msamaha ni sehemu ya uungwana lakini Kafulila aliomba msamaha au alikuwa analilia Hisani (favor)?
 
Selous, ukiwa mwanafunzi wa Social Psychology utakumbuka vizuri nilivyowafundisha ubaya wa 'group think' na 'conformity' jinsi zinavyofifisha uwezo wa kufikiri. Nami sijaongelea habari za kutukana kiongozi; naongelea habari za kumkosoa. Kumtukana kiongozi au mtu yeyote ni jambo la ovyo ndani au nje ya vikao. Mtu yeyote anayetukana anastahili kuchukuliwa hatua za nidhamu awe ametukana ndani au nje ya vikao. Lakini napinga kwa nguvu zangu zote watu kujijengea uimaya wa kutukuguswa hata pale wanapofanya madudu
!
Dr.Kitila tafakari kisha uje na hoja ya kumjenga kafulila...Well hivi alichokifanyaKafulila.. wewe unaona siyo tusi? ama kutukana we najua ni kuongea neno lenyewe? Unaleta hoja ya kumkosoa alichomkosoa Mbatia ni kipi?

andiko la GL linasema hivi "...Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena**" haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia " kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana .." hapa anamaanisha Kafulila japo anampenda sana Zitto... hawezi kumsaidia kubeba mimba yake ya kugombea urais 2015 kupitia NCCR. na tunajua DR. Kitila ni Pro Zitto siku zote please mimba ya Zitto itawatokea puani.

Sio uasi?
Kwenye hivi vyama vyetu ndugu yangu ukisema kwamba Mwenyekiti kakosea ndiyo uasi wenyewe, na tena ukisema unaitaka nafasi ya mwenyekiti ndiyo unakuwa mhaini kabisa. Hamad Rashid inawezekana kweli ana makosa yake lakini uhaini wake ni kuitaka nafasi ya Seif kabla ya Seif mwenyewe hajafa. Uongozi ndani ya vyama vyetu hivi vya siasa ni aina fulani ya Usultani. Ama uwe kibaraka au mla makombo.

Unadhani leo hii ndani ya CHADEMA hata mtu awe na sifa nyingi kiasi gani atathubutu kusema kwamba anatamani kugombea Urais mwaka 2015? Thubuutu! Mwenyewe yupo na wapambe wake wako tayari kumtoa mtu nyongo ili lao lifanikiwe.
 
Okukariri nakyo kipaji! iwe nobasa? kalale ofile na wivu wa kiume!
Kukariri siyo kipaji ni juhudi binafsi ya mtu,ila ni binadamu wenyewe wanaamua wakariri nini. Wapo walioamua kukariri majina ya Mabasi ya abiria yanayokwenda mikoani, wengine nyimbo za taarabu, wapo waliobobea kwenye majina ya meli, wengine hisabati. kwa hiyo kukariri si kipaji!!
 
Dr.Kitila tafakari kisha uje na hoja ya kumjenga kafulila...Well hivi alichokifanyaKafulila.. wewe unaona siyo tusi? ama kutukana we najua ni kuongea neno lenyewe? Unaleta hoja ya kumkosoa alichomkosoa Mbatia ni kipi?

andiko la GL linasema hivi "...Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena**" haijalishi**unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia " kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda**sana .." hapa anamaanisha Kafulila japo anampenda sana Zitto... hawezi kumsaidia kubeba mimba yake ya kugombea urais 2015 kupitia NCCR. na tunajua DR. Kitila ni Pro Zitto siku zote please mimba ya Zitto itawatokea puani.

Don't take it personal bros!!
 
Tatizo la Watanzania Ni Ushabiki na tabia hii imetoka na kutazama sana mipira ya league ya Uingereza. League hii imezua taifa la Wabishi watu wanaopenda kubishana hata kama kuna mamkosa ili mradi mtu kasimama upande gani. Maajabu makubwa ni kwamba huku majuu watu hawabishani kuhusu Mpira, huwezi kuta watu wamekaa na kubishana kuhusu mpoira kila mshabiki na watu wake ktk kundi lake, huwezi kuta washabiki wa team tofauti ktk kijiwe kimoja wakibishana..

Chadema itajiua yenyewe kutokana na makundi yaliyojitokeza. Zitto ana matatizo yake na kweli niliwahi kusema Zitto sii mwanasiasa ni mwanataaluma zaidi na siasa haziwezi kwa sababu siasa zina mpangilio wake. Tatizo la Zitto na Kafulila sii la kwao wao bali la Kimfumo maana Wataalam wetu wanaotakiwa kuwa viongozi ama mawaziri ndio hao hao wanakuwa wanasiasa. Hivyo kipimo cha mwanasiasa ni uwezo wake kushika uwaziri ama kuongoza shirika..Na ndio maana Kafulila haoni makosa yoyote kumsema kiongozi wake kwa sababu ktk utendaji kazi hili ni jambo la kawaida kabisa lakini kisiasa ni makosa ya kinidhamu..

Maadam vitu hivi vimechanganywa na hamtaki kuvitenganisha nitawambia tu ya kwamba Kafulila hana makosa isipokuwa mwenye kmakosa ni Mbatia kumvua mtu uanachama. Chama hakiwezi kabisa kukubali kupoteza kura zake kwa ujinga unaofanywa na Mbatia mwenyewe kwanza kabisa he lost General election na inamweka mahala pabaya zaidi kuwakilisha wananchi. Kumfukuza Kafulila he went way far beyond... Mbatia ni Dikteta na opportunist kama vijana wengine wengi wa NCCR - MAGEUZI wanaotumia siasa kama njia ya kutokea kimaisha....
 
Tatizo la Watanzania Ni Ushabiki na tabia hii imetoka na kutazama sana mipira ya league ya Uingereza. League hii imezua taifa la Wabishi watu wanaopenda kubishana hata kama kuna mamkosa ili mradi mtu kasimama upande gani. Maajabu makubwa ni kwamba huku majuu watu hawabishani kuhusu Mpira, huwezi kuta watu wamekaa na kubishana kuhusu mpoira kila mshabiki na watu wake ktk kundi lake, huwezi kuta washabiki wa team tofauti ktk kijiwe kimoja wakibishana..

Chadema itajiua yenyewe kutokana na makundi yaliyojitokeza. Zitto ana matatizo yake na kweli niliwahi kusema Zitto sii mwanasiasa ni mwanataaluma zaidi na siasa haziwezi kwa sababu siasa zina mpangilio wake. Tatizo la Zitto na Kafulila sii la kwao wao bali la Kimfumo maana Wataalam wetu wanaotakiwa kuwa viongozi ama mawaziri ndio hao hao wanakuwa wanasiasa. Hivyo kipimo cha mwanasiasa ni uwezo wake kushika uwaziri ama kuongoza shirika..Na ndio maana Kafulila haoni makosa yoyote kumsema kiongozi wake kwa sababu ktk utendaji kazi hili ni jambo la kawaida kabisa lakini kisiasa ni makosa ya kinidhamu..

Maadam vitu hivi vimechanganywa na hamtaki kuvitenganisha nitawambia tu ya kwamba Kafulila hana makosa isipokuwa mwenye makosa ni Mbatia kumvua mtu uanachama. Chama hakiwezi kabisa kukubali kupoteza kura zake kwa ujinga unaofanywa na Mbatia mwenyewe kwanza kabisa he lost General election na inamweka mahala pabaya zaidi kuwakilisha wananchi. Kumfukuza Kafulila he went way far beyond... Mbatia ni Dikteta na opportunist kama vijana wengine wengi wa NCCR - MAGEUZI wanaotumia siasa kama njia ya kutokea kimaisha....
umewaona wenyewe walivyofura lakini??
 
Umenena vema mh. Lema. Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi. Ni kweli pia mh David anayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kwa hiyo fursa bado anamstakali ktk maisha ya siasa na mengine. Tufauti kubwa kati ya walioko na wasio madarakani kati ya mengine mengi yapaswa kuwa ni nidhamu,uadilifu,uzalendo n.k. Tukizingatia hayo tutafika tutakako kama taifa na mtu mmoja mmoja.
 
Hili la Kafulila kuomba radhi mimi binafsi nalielewa. Yeye alipoingia kwenye kikao alidhani siasa za hoja zina nafasi kwenye vikao vya vyama vyetu kumbe kinyume chake siasa za mikakati ndiyo nguzo zinazohimili nguvu ya ushawishi ndani ya vyama hivi. Hapa tunaweza kujifunza kwa Mutungirehi, Salim Ahmed Salim, Chacha Wangwe, Kolimba na wengineo.

Siamini kama Kikwete anamzidi uwezo wa kiuongozi Salim, lakini mikakati ilimweka Kikwete kwenye Uongozi na kumtupa pembeni Salim. Ndani ya kile kikao Kafulila aligundua hakuna hata mtu mmoja (Zaidi ya kundi la kina Rungwe) aliyetayari kumuunga mkono kweye madai yake dhidi ya Mbatia. Kafulila badala ya Ku - retreat yeye aka - capitulate. Kwangu mimi kuomba msamaha ni sehemu ya uungwana lakini Kafulila aliomba msamaha au alikuwa analilia Hisani (favor)?

Hapo kwenye Red ni Swali la msingi hilo.......Kwanza kabisa Kafulila alikuwa anachukulia poa kuwa hawataweza kumvua uanachama coz ya ubunge sasa lilipomfika ndo akaona kuwa ubunge ni kama ua lililoota kwenye chupa.Uhai wake unategemea uwepo wa chupa sasa alipovuliwa uanacha ndo akashtuka kumbe hata ubunge nao umekwenda. alichokuwa anaomba ni kusamehewa ubunge. SWALI la kizushi.Hivi wakisema wamrudishie uanachama ila asiwe mbunge(Japo sijui sheria inasemaje kwenye hilli)atakuwa tayari?
 
Lema anasoma sana vitabu vya philosophy, point anazojenga zinanikumbusha kitabu kimoja cha Socrates wakati alipokuwa anatetea uamuzi wa yeye kuuliwa.
 
Kwani wakati kafulila anakashfu viongozi wake kwanjia zisizo na utaratibu kama kupeleka kwenyekamati kuu,hamkumshauri kafukuzwa ndio mnajifanya mnasympath naye!
 
Lema next time jaribu kuwauliza wasomi kitu unachotaka kuandika. Hapo umeandika upupu.
 
Mimi namsifu Lema kwamba ni mtu anayefikiri nje ya sanduku na kusema ukweli ameleta hoja hii ambayo kiasi ni controversial ili watu tuijadili, kusema Lema ni mjinga kama alivyosema Mzee hapo juu, bila ya kuonyesha ujinga wake ni kufilisika kimawazo. Mimi naamini itakuwa sio sawa, kumtetea mtu simply kwa sababu ni kijana mwenzetu na wakati huo itakuwa sio haki pia kumpinga mtu kutokana na ujana wake.

Sasa wale ambao wana hoja za msingi za kupinga ki8le Lema alichosema na waseme sasa, tuache hoja zisizo na vichwa wala miguu.
 
Chadema itajiua yenyewe kutokana na makundi yaliyojitokeza. Zitto ana matatizo yake na kweli niliwahi kusema Zitto sii mwanasiasa ni mwanataaluma zaidi na siasa haziwezi kwa sababu siasa zina mpangilio wake. Tatizo la Zitto na Kafulila sii la kwao wao bali la Kimfumo maana Wataalam wetu wanaotakiwa kuwa viongozi ama mawaziri ndio hao hao wanakuwa wanasiasa. Hivyo kipimo cha mwanasiasa ni uwezo wake kushika uwaziri ama kuongoza shirika..Na ndio maana Kafulila haoni makosa yoyote kumsema kiongozi wake kwa sababu ktk utendaji kazi hili ni jambo la kawaida kabisa lakini kisiasa ni makosa ya kinidhamu..

Maadam vitu hivi vimechanganywa na hamtaki kuvitenganisha nitawambia tu ya kwamba Kafulila hana makosa isipokuwa mwenye kmakosa ni Mbatia kumvua mtu uanachama. Chama hakiwezi kabisa kukubali kupoteza kura zake kwa ujinga unaofanywa na Mbatia mwenyewe kwanza kabisa he lost General election na inamweka mahala pabaya zaidi kuwakilisha wananchi. Kumfukuza Kafulila he went way far beyond... Mbatia ni Dikteta na opportunist kama vijana wengine wengi wa NCCR - MAGEUZI wanaotumia siasa kama njia ya kutokea kimaisha....[/QUOTE]
Kwenye red unanikumbusha UDSM somo linaitwa PL= Critica thinking and argumentation... yaani vilaza tulikuwa tunawajua fast.. primises deffer with conclusion
 
Kukariri siyo kipaji ni juhudi binafsi ya mtu,ila ni binadamu wenyewe wanaamua wakariri nini. Wapo walioamua kukariri majina ya Mabasi ya abiria yanayokwenda mikoani, wengine nyimbo za taarabu, wapo waliobobea kwenye majina ya meli, wengine hisabati. kwa hiyo kukariri si kipaji!!

Olanganyira akashwahili tinkamanyage! ka kitali kipaji ebyoyagamba byona iwe wakubikariri alafu obigamba okwo bili? pamoja ne ekipaji lazima ne ejuhudi zibeo! bati Mungu mbela naiwe otaileo agae!
 
Back
Top Bottom