Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Tangu siku ya kwanza taarifa imetolewa ya wananchi kuvamia nyumba za watu na kukata nguzo za Tanesco, nilisema wazi kwamba hawa wananchi ni hamnazo. Yaani hawana kiongozi mwenye akili kabisa. Maana wanaharibu mali zao wenyewe na kuwaibia masikini wenzao badala ya kupambana na serikali ambayo ndiyo imewadhulumu. Wao wadeal na mkuu wa wilaya au mkurugenzi. Sasa wanachoma kituo cha polisi wakati sisi mtaani kwetu tunachangishwa kujenga kituo cha polisi baada ya kupeleka maombi ya kituo hicho miaka karibu kumi iliyopita, wao wanachoma. Hawa wananchi ni waajabu kupata kutokea katika historia ya nchi. Bora wangekiteka na kuwatoa waandamanaji waliokamatwa sasa wanachoma? Je wanatandahimba waliokuwa mahabusu humo?ipo siku utawatafuta pamoja na mapungufu yao. uzuri taasisi hii bwana, ni utumishi wa umma, leo unaiponda kesho upo kwao wakutatulie baadhi ya shida zao. Mleta mada hajasema chochote zaidi ya kutaka maelezo kwa wadau, badala ya kumpa maelezo mnawapongeza wananchi kuchoma kituo cha polisi. kama ndo utawala bora sawa.
lakini suala la msingi ni kuwa, wananchi wa maeneo hayo wana madai na serikali kama sio mzabuni kuwa alichukua KOROSHO zao lakini hataki kuleta mafao yao.
juzi walikata hadi nguzo za tanesco, wameangusha barabara, wamekata miti na kuziba barabara na uharamia mwingi. sasa kuchoma kituo cha polisi ndo polisi itawalipa hizo pesa zao?
kwa nini wasimwendee aliyechukua mazao yao na kumwajibisha?