Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya Tandahimba linaungua moto!

ipo siku utawatafuta pamoja na mapungufu yao. uzuri taasisi hii bwana, ni utumishi wa umma, leo unaiponda kesho upo kwao wakutatulie baadhi ya shida zao. Mleta mada hajasema chochote zaidi ya kutaka maelezo kwa wadau, badala ya kumpa maelezo mnawapongeza wananchi kuchoma kituo cha polisi. kama ndo utawala bora sawa.

lakini suala la msingi ni kuwa, wananchi wa maeneo hayo wana madai na serikali kama sio mzabuni kuwa alichukua KOROSHO zao lakini hataki kuleta mafao yao.

juzi walikata hadi nguzo za tanesco, wameangusha barabara, wamekata miti na kuziba barabara na uharamia mwingi. sasa kuchoma kituo cha polisi ndo polisi itawalipa hizo pesa zao?

kwa nini wasimwendee aliyechukua mazao yao na kumwajibisha?
Tangu siku ya kwanza taarifa imetolewa ya wananchi kuvamia nyumba za watu na kukata nguzo za Tanesco, nilisema wazi kwamba hawa wananchi ni hamnazo. Yaani hawana kiongozi mwenye akili kabisa. Maana wanaharibu mali zao wenyewe na kuwaibia masikini wenzao badala ya kupambana na serikali ambayo ndiyo imewadhulumu. Wao wadeal na mkuu wa wilaya au mkurugenzi. Sasa wanachoma kituo cha polisi wakati sisi mtaani kwetu tunachangishwa kujenga kituo cha polisi baada ya kupeleka maombi ya kituo hicho miaka karibu kumi iliyopita, wao wanachoma. Hawa wananchi ni waajabu kupata kutokea katika historia ya nchi. Bora wangekiteka na kuwatoa waandamanaji waliokamatwa sasa wanachoma? Je wanatandahimba waliokuwa mahabusu humo?
 
Haonekani!! Kama vp tujuze kilichotokea na kinachoendelea!!
Binafsi nimewachoka hawa Policcm, acha wananchi wachukue uamzi sitahiki!!

Wafanyakzi tunaishi roho mkononi...

Baadhi wamesafirisha familia zao,na wanaendelea kusafirisha familia zao..

Squad za polisi kutoka wilaya za Mtwara na Newala zinakuja kuongeza nguvu.. Inasemekana na Wanajeshi wa Nachingwea waweza kuja nao..
 
Na si kituo cha polisi.. Ni ofisi ya OCD..

Ofisi ya OCS iko salama salimini..
 
Mbona Huko Hata Vuguvugu la M4C halijafika? ni likifika itakuwa Balaa!!!
 
yaani ocd kusaidia ufunguaji wa canteen za vinywaji vikali na baridi ndio mnamwona mwema!!!???

amegharika huyu, toka lini askari wa tanzania akawa mwema kwa raia badala ya kuwa mtiifu kwa mabwana zake? Mie niko hapa na namjua vizuri huyu mzee, anatabia za undumila kuwili, mfano juzi alikwenda mihambwe kusuluhisha, akawahakikishia wananchi amani na kwamba hakuna atakayekamatwa! Leo alfajiri askari wameingia wamepora maduka na kamata kamata mtindo mmoja, ndio wema huo?
 
Tangu siku ya kwanza taarifa imetolewa ya wananchi kuvamia nyumba za watu na kukata nguzo za Tanesco, nilisema wazi kwamba hawa wananchi ni hamnazo. Yaani hawana kiongozi mwenye akili kabisa. Maana wanaharibu mali zao wenyewe na kuwaibia masikini wenzao badala ya kupambana na serikali ambayo ndiyo imewadhulumu. Wao wadeal na mkuu wa wilaya au mkurugenzi. Sasa wanachoma kituo cha polisi wakati sisi mtaani kwetu tunachangishwa kujenga kituo cha polisi baada ya kupeleka maombi ya kituo hicho miaka karibu kumi iliyopita, wao wanachoma. Hawa wananchi ni waajabu kupata kutokea katika historia ya nchi. Bora wangekiteka na kuwatoa waandamanaji waliokamatwa sasa wanachoma? Je wanatandahimba waliokuwa mahabusu humo?

Ofisi ya OCD ndiyo iliyoungua.. Si ya OCS,yenye mahabusu,silaha,magari na pikipiki..

Hawa Wanatandahimba walitajiwa bei ya 1,200 kwa kilo moja ya korosho..

Advance wakapewa sh800 bado sh 400. Huu mwezi wa saba sasa hawajapata! Na muda wa kuandaa mashamba umewadia,hawana hela za pembejeo.. Na hilo ndilo zao lao kuu..

Ukumbuke pia kuwa hata hizo sh800 serikali haikuwa nazo,imekopa kwenye mabenki.. Ikitegemea ikiuza italipa mabenki na kumalizia wakulima..

Wahindi ambao ni wanunuzi wa Korosho za serikali,wanasita kuzinunua kutokana na kwamba kwa mwaka huu zimekuwa nyingi zaidi,na soko lake kimataifa limeshuka..
 
amegharika huyu, toka lini askari wa tanzania akawa mwema kwa raia badala ya kuwa mtiifu kwa mabwana zake? Mie niko hapa na namjua vizuri huyu mzee, anatabia za undumila kuwili, mfano juzi alikwenda mihambwe kusuluhisha, akawahakikishia wananchi amani na kwamba hakuna atakayekamatwa! Leo alfajiri askari wameingia wamepora maduka na kamata kamata mtindo mmoja, ndio wema huo?

SALOK unaishi wapi mkuu?

Suluhu iliombwa na wazee wa hapa mjini..kwa maaskari waache vipigo na kamatakamata zao.. Lakini raia wakadai wanaipa serikali hadi Ijumaa ya kesho kutwa..

Cha ajabu jana mnamo saa moja ofisi ya OCD inaungua moto.. Na intelijensia zao imeonesha ni hujuma,sasa wao wafanyeje..!

We kama unawatetea hao vijana wa Mihambwe sijui unawatetea kwa lipi kwani wamefukuza walimu 16 na kumpiga askari nusu ya kumuua.. Walimu wamepangiwa vituo vingine na huenda wasipate huduma ya elimu kwa muda mrefu..

Mtu afanye wema gani mwingine.. Kijana ametoka alikotoka kuja kufanya kazi OCD akampangia Mihambwe.. Askari apigwe,walimu wafukuzwe,mali zao zichukuliwe na wanaojiita wakulima wanaodai malipo ya korosho zao.. OCD anakuja kuwabembeleza bado mnaona hafai..

Kwa taarifa yako,hadi mbunge anayesemekana kushindwa 2010..ana uswahiba mkubwa sana na OCD..
 
This country Bwana, kazi ipo; Police wajifunze kusimamia na kutenda haki, na sio kutumiwa; maana wananchi wakishakuwa sugu, hali itakuwa mbaya sana.
 
Mkuu GambaChovu umeongea kwa hisia kali sana pengine hukunielewa! kimsingi siwatetei BOKOHARAMU wala sikuridhishwa na matukio ya vijana mihambwe kwani mie pia ni muathirika wa matukio hayo kwa namna nyingine, ninachokisema na naendelea kusema askari si wa kuaminika kiasi hicho! kule mihambwe waliopigwa na kukamatwa, kuporwa maduka yao sio waliompiga huyo askari na hakukuwa na vurugu yoyote, watu wamevamiwa alfajiri wakiwa wamelala! kuhusu tukio la jana hizo hujma zinahusiana vp watu wa mihambwe?
 
Haiwezi kujulikana kwa haraka kwa kweli kama ni watu wa Mihambwe ndiyo waanzilishi wa fujo za jana ama la.. Ila wameenda hata na Namikupa pia..

Mambo ya kiintelijensia sina uzoefu nayo.. Labda ndiyo namna yao askari ya kufanya kazi,sielewi.. Pole sana kwa kuathirika mkuu..
 
Halafu si wajua askari wanafanya kazi kwa msaada wa raia pia.. Wenyewe wanawaita "raia wema".. Ndiyo wanaoleta taarifa za siri,labda za kutaja matukio ya kihalifu yaliyopangwa,na kutaja wapangaji na watekelezaji wa matukio hayo ya kihalifu..

Katika hali tete,na dharura kama hii,sidhani kama ni rahisi kufanya uchunguzi na kuwabaini hao wanaoojiita boko haram au washirika wao..

Nadhani raia yeyote mwema mwenye kufahamu angalau wawili tu angesaidia Jeshi la Polisi pa kuanzia..
 
Mkuu GambaChovu, Hivi uswahiba wa Kattan Ahmad Kattan na OCD, ndio kipimo cha wema wa mzee huyu kwa raia? vitendo vya uporaji vilivofanywa na polisi leo alfajiri kule mihambwe ni ktk wajibu wao? hapa usijesema hata polisi wameshambuliwa kwani walistahili hayo! kwanini wasitumike viongozi wenye ushawishi mkubwa kwa jamii kama diwani kupata suluhu kule mihambwe? unavyoona wewe ni halali kutopeleka watumishi na waliopo kuwahamisha kwa muda 2yrs ktk kata mihambwe? NARUDIA TENA HUYU NI NDUMILA KUWILI...!!!
 
Haya mkuu..

Ila nilimtaja huyo kwa kuwa anaonekana ni kipenzi cha raia wengi wa Tandahimba. Vijana kwa wazee..

Lakini unadhani hao wanaojiita BH wanawakilisha maslahi yao,au ya ndugu na jamaa zao?

Na je njia wanayotumia ni sahihi?!
 
Kwangu BOKOHARAMU ni WANAHARAMU! Nalaani na kupinga vikali harakati zao? na wengine wasiokuwa hao BK lakini wanaendesha harakati hizi haramu!

Kilio cha wakulima kilishasikika kupitia maandamano na yaliisha kwa amani!
 
Hali bado ni tete... Barabara ziko kimya kabisa! Wengi wanataka kuhama mji!..
 
Kwangu BOKOHARAMU ni WANAHARAMU! Nalaani na kupinga vikali harakati zao? na wengine wasiokuwa hao BK lakini wanaendesha harakati hizi haramu!

Kilio cha wakulima kilishasikika kupitia maandamano na yaliisha kwa amani!

Kwa hali ilivyo na jinsi ninavyoathirika.. Ningeweza kuikopesha serikali iwalipe wakulima,ili mradi amani irudi...(kama ningalikuwa na uwezo)

Maana hii yote naona ni kuzima moto,ila chanzo chake(madai ya wakulima) bado hakijashghulikiwa..

Gee Cee
 
Nasikia mkuu wa mkoa aliyestaafu ndugu Anatory Tarimo alikuwa anawajali sana wakulima wa korosho huko. Vipi huyu Luteni Simbakalia anawajali wakulima au vipi? Msimamo wake ukoje ktk hili?
 
Kazi nzuri sana, kama polisi hawawezi kufana kazi yao, tutawasaidia, wao si wanatumiwa na magamba kutupiga mabomu, tutaona 2015 kama watatupiga nchi nzima....

TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED...YES WE CAN....GOD BLESS CDM.....AND ALL OF US
 
Back
Top Bottom