Serikali Iko Mbioni Kujenga Ofisi ya OCD Wilaya ya Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

SERIKALI IKO MBIONI KUJENGA OFISI YA OCD WILAYA YA KALIUA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Bungeni, Mhe. Aloyce Andrew Kwezi amekiri kuwa Serikali katika mpango wake wa miaka 10 wa kujenga vituo vya Polisi ngazi ya Wilaya, Kaliua itapewa kipaumbele

"Wilaya ya Kaliua hatuna Ofisi ya OCD (Jengo la Polisi la Wilaya ya Kaliua), Je, Serikali iko tayari kutenga bajeti kwaajili ya ujenzi na eneo liko tayari pale Kaliua" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Serikali iko tayari kusaidiana na Wilaya ya Kaliua kuhakikisha kituo cha Polisi Kaliua kinajengwa. Na kwa vile tayari wana eneo tutawasiliana na IGP ili kwenye mpango wake wa miaka 10 wa kujenga vituo vya Polisi ngazi ya Wilaya Kaliua pia iweze kupewa kipaumbele" - Mhe. Jumanne Sagini, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-09-04 at 11.21.49.mp4
    11.6 MB
Back
Top Bottom