Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya Tandahimba linaungua moto!

ipo siku utawatafuta pamoja na mapungufu yao. uzuri taasisi hii bwana, ni utumishi wa umma, leo unaiponda kesho upo kwao wakutatulie baadhi ya shida zao. Mleta mada hajasema chochote zaidi ya kutaka maelezo kwa wadau, badala ya kumpa maelezo mnawapongeza wananchi kuchoma kituo cha polisi. kama ndo utawala bora sawa.

lakini suala la msingi ni kuwa, wananchi wa maeneo hayo wana madai na serikali kama sio mzabuni kuwa alichukua KOROSHO zao lakini hataki kuleta mafao yao.

juzi walikata hadi nguzo za tanesco, wameangusha barabara, wamekata miti na kuziba barabara na uharamia mwingi. sasa kuchoma kituo cha polisi ndo polisi itawalipa hizo pesa zao?

kwa nini wasimwendee aliyechukua mazao yao na kumwajibisha?

Ni kweli mkuu tukiwa raia wa nchi inayojivunia upendo na amani hatupaswi kushabikia maasi kama haya,lakini pia tujiulize swali moja la msingi
*serikali yetu {simaanishi polisi}inakuwa wapi kusikiliza na kuvifanyia kazi vilio vya wananchi kama hawa hadi wanafikia kukata tamaa na kuyafanya maasi yote haya bila huyo aliyewatapeli kuchukuliwa hatua?
Nadhani hii inatokana na baadhi ya makampuni kuwahusisha baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali za kitaifa na katika halmashauri zetu nchini.
Na linapojitokeza suala kama hili wanabaki kutumia nguvu kulizima kwa sababu fweza kama fweza wanakuwa walikwisha gawana na kuitafuna kitambo.sasa hata kuripoti tukio ngazi za juu hawalipeleki kama lilivyo bali wanavyoona wao na matokeo yake ndo inakuwa kama TANDAHIMBA
 
Helikopta imeingia,ila aliyemo sijui ni nani kwa kweli..

Angekuwa Waziri Mkuu sawa,lakini IGP,hatakuwa na jipya nadhani..

Hawa vijana wa Inteligensia huwa kila kitu utasikia ni SIASA; vipi hawajahusisha na mambo ya SIASA hapo??

Chunguza kauli zao zinasemaje. KWani haya matukio hata kwenye TV au vyombo vya habari hawatangazi sijui vipi hawa.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Chanzo cha moto kitajulikana hapo kesho..
(shoti ya umeme huenda)

Ila,baada ya jengo hilo kuungua kwa muda,umeme ukakatika..

Askari wanapatrol mitaani na kupiga mabomu kutuliza ghasia..

Jirani na ofisi hiyo pana maduka ya wafanyabiashara,ambao huenda maduka yao yakaathirika kwa moto huo,maana huduma za kuzima mioto mawilayani,ndiyo hivyo tena..

2230.....
Hakuna taarifa juu ya kudhibitiwa ama kutodhibitiwa kwa moto huo hadi sasa,wala hasara iliyopatikana..

Updates zaidi kesho..
0605hrs:

Inasemekana maduka yote yameteketea kwa moto ulioanzia kwenye ofisi ya OCD.. Maeneo hayo ni jirani na soko,hivyo mabanda mengi ya biashara yameathirika!

-Watu wameanza safari kwenda vijijini na sehemu nyingine za jirani

- Kwa wenye ndugu,wasio na ndugu wamepanda basi la Dar..

0700hrs
- Yasemekana chanzo cha moto ni hujuma!
-Baadhi ya familia zaomba hifadhi kituo cha Polisi(kwa OCS) ambako kuna ukumbi mkubwa wa canteen unaotumika kwa sherehe na vinywaji baridi na vikali...

1320hrs:
- Helikopta ya Polisi inarandaranda juu..
Gee Cee

wengine wanasifu kituo kuchomwa, wengine wanaomba hifadhi kwa polisi hao hao ambao baadhi ya wananzengo humu mnawaponda na kusema bora wamechomewa. shame on you
 
Ni kweli mkuu tukiwa raia wa nchi inayojivunia upendo na amani hatupaswi kushabikia maasi kama haya,lakini pia tujiulize swali moja la msingi
*serikali yetu {simaanishi polisi}inakuwa wapi kusikiliza na kuvifanyia kazi vilio vya wananchi kama hawa hadi wanafikia kukata tamaa na kuyafanya maasi yote haya bila huyo aliyewatapeli kuchukuliwa hatua?
Nadhani hii inatokana na baadhi ya makampuni kuwahusisha baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali za kitaifa na katika halmashauri zetu nchini.
Na linapojitokeza suala kama hili wanabaki kutumia nguvu kulizima kwa sababu fweza kama fweza wanakuwa walikwisha gawana na kuitafuna kitambo.sasa hata kuripoti tukio ngazi za juu hawalipeleki kama lilivyo bali wanavyoona wao na matokeo yake ndo inakuwa kama TANDAHIMBA

kwa nini usiwakamate wahusika na kuwapa kipigao? kwa nini uchome majengo na kuharibu miuondombinu ambayo kesho pia utalipa kodi ili ijengwe? mchawi unamjua, halafu anapigana na kitu kisichokuwa na uhai?
 
Dah!! Nimehangaika kuitafuta hii thread majukwaa kibao kumbe imeletwa huku? Na nyie mods muwe mnatoa taarifa bana da! Mpaka nikalazimika kuigoogle!
 
kwa nini usiwakamate wahusika na kuwapa kipigao? Kwa nini uchome majengo na kuharibu miuondombinu ambayo kesho pia utalipa kodi ili ijengwe? Mchawi unamjua, halafu anapigana na kitu kisichokuwa na uhai?

unaonekana wewe ni mvivu wa kufuatilia comment halafu unaharaka ya kuchangia! Na kwa namna unavochangia nachelea utanisababishia ban! Kilichoungua ni ofisi ya ocd na chanzo hakijajulikana, cha ajabu askari waliwazuia watu kuokoa mali zao zikateketea kwa moto, nyambaf we!!
 
Kwanini una imani na Pinda na wala si IGP?.

Mambo wanayodai yako kwenye dhamana ya serikali.... Na viongozi wa serikali kuu ni Rais,Makamu na PM..

Huyu ni Askari wa Usalama wa Raia wa Taifa.. Jibu la madai ya wenyeji hatakuwa nalo..
 
Hawa vijana wa Inteligensia huwa kila kitu utasikia ni SIASA; vipi hawajahusisha na mambo ya SIASA hapo??

Chunguza kauli zao zinasemaje. KWani haya matukio hata kwenye TV au vyombo vya habari hawatangazi sijui vipi hawa.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!

Siasa imehusishwa sana...

TBC wanatangaza bila kutoa picha.. Ila kwa kuwa IGP kaja,huenda atakuwa na mwandishi wa serikali..
 
wengine wanasifu kituo kuchomwa, wengine wanaomba hifadhi kwa polisi hao hao ambao baadhi ya wananzengo humu mnawaponda na kusema bora wamechomewa. shame on you

Shida ni kuwa msako wa polisi wa nyumba hadi nyumba hauangalii huyu ni mfanyakazi,mkulima,misheni town,mzururaji,mzee,kijana,mke,mume,wengine hadi watoto hawana huruma nao!
Unapigwa virungu,mpaka uje utoe kitambulisho,ushapigwa sana..
Kwa hiyo jana ili kuliepuka hilo,ni kukimbilia hukohuko kwa OCS!
 
Mkuu, hauwezi ukapiga picha na ukaitupia humu?

Tatizo ni kuwa natumia kilongalonga,picha ninazo nashindwa kuziupload kwani sina laptop,na mambo kama haya si vizuri kujulikana unayaweka hewani..

Ila nimeiona land cruiser "mkonge" ya TBC..itakuwa imechukua matukio..
 
IGP kasema atafanya mazungumzo Alhamisi na waathirika wa vipigo na wale waliounguliwa na mioto..

Chopper imepaki uwanja wa mpira na askari kibao wanalinda..

IGP kaenda kulala yapata saa nzima iliyopita..
 
Nashindwa kuja na updates kwa sasa kwani IGP haijajulikana ataongea saa ngapi .. Ila napata habari ambazo si za kuaminika... Ambazo haziwezi kuwekwa hadharani..

Asanteni kwa kunifuatilia..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom