Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Dua,
Mjomba hapa nakubaliana sana na Bin Maryam kwa kutazama vielelezo vilivyotangulia..
Siku zote tunasema Amani yetu imejengwa na Ujamaa lakini mbona hata Zambia na Malawi ambao walikuwa Mabepari nao wana amani kama yetu na Ukabila sii swala kabisa linaloongelewa ndani ya nchi zao... Je, ni kipi ambacho tunafanana nao hawa watu... Utakuta ni kuwa sote tulipata Uhuru wetu kibwelele yaani jitihada za Uhuru wetu hazikuanzishwa na wananchi wenyewe kwa kuingia mwituni isipokuwa sheria za UN ndiuzo zilitupa Uhuru huo laa sivyo labda who knows tungekuwa tukitawaliwa hadi leo. Na trust me kuna tofauti kubwa sana kati yetu bara na Zanzibar na ndio maana tunawaona wao kuwa wana matatizo hali sisi Bara ndio wenye matatizo na hiyo slogan ya amani na utulivu yetu.
Sasa huo utulivu wetu wa amani mahala ambapo haki zetu zinachukuliwa na wachache ati tukiita watu wa amani ni Ujanja kweli ama ndio Ujinga wenyewe?...Mbona Tanzania, Zambia na Malawi ndizo nchi ambazo tunaliwa zaidi na viongozi kila siku kazi yao ni kubadilisha mashati tu.... (Ofisi za kazi). Na sii kwamba hatujui kuwa hawa ni Mafisadi lakini ndio kwanza tunawabeba ktk KURA na kuwaita waheshimiwa.
Sasa ukirudi ktk kuuliza mchango gani Bin Maryam kautoa, mzee wangu hapo utakuwa umechukia.... maanake hapa ni kijiweni tu sote ni Wadanganyika ambao miaka yote tumeukumbatia Ujinga huo wa amani na utulivu...Lakini kama walivyosema wahenga kuwa siku zote idea huanza na mtu mmoja kisha ikapata support na mwishowe ikatumika kuleta mabadiliko na ndio changes tunazopigania hapa. Ni kutokana na michango yenu imenisaidia sana mimi hapa kutokubali kuendelea kuwa chini ya viongozi wabovu.. leo nipo mimi kesho mtampa mtu mwingine na wimbi la msukumo wa fikra hizi utazidi kupanua wigo kati ya Wadanganyika.
Hata hiyo hoja yako ya kuuliza mchango wake nadhani pia ni msukumo wa fikra ambayo kesho itampa nguvu Bin Maryam afikirie kuchangia kivitendo fikra hizi za Mapinduzi ya fikra...
I guess hapa ndipo tulipo sasa hivi ktk Mapinduzi ya fikra na labda jambo kubwa zaidi ni jinsi ya kuzieneza hizi fikra ziwafikie Wadanganyika wengi zaidi.
Mkandara:
Mtu yoyote atakayeleta suala la amani ni lazima aangalie historia yetu. Machafuko makubwa yalikuwa wakati wa majimaji na baada ya hapo nchi imekuwa ya amani.
Tunachojua ni kuwa amani siku zote inakuja na maendeleo ya kijamii. Ukiona watu wana amani kwa muda mrefu na maendeleo hayapatikani ni lazima kutakuwa na kitu kinachowakwamisha.