Ubepari Vs Ujamaa, tuanzie hapa!

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Na bwana Kenge,

Kuna kitu kinatawala sana fikra zangu.Ubepari ni mfumo wa kiuchumi ambao mali nyingi zinamilikiwa na Sekta/watu binafsi. Katika Syllabus yoote ya Tanzania masomo yote Civics, History, Economics hakuna Kipengele utachoona wameelezea vizuri mada hii yani ni ile kupita Juujuu tu. Lakini amini kama Taifa kuijua mifumo hii itasaidia sana sana sana kujikwamua kiuchumi.
_90677226-b887-4ac5-a6ea-6de10e2c6580.jpeg

Ubepari/Capitalism
Wazungu au Makaburu kule bondeni wanashikilia uchumi kwa Mfumo huu wa Ubepari. Kwenye Ubepari kabla ya kutajirisha Serikali. Serikali inahakikisha Mali nyingi Viwanda, n.k zinamilikiwa na Watu binafsi. Yani serikali inaweka nguvu nyingi kwenye rasilimali watu.

Leo ukianza kuchambua Matajiri wa US asilimia kubwa ni watu wa Sekta Binafsi ambao hawahusiki na Serikali kabisaa.Ila ukija huku Africa chukua any Random country kisha tafuta Matajiri wa nchi hiyo 70% utakuta waliwahi kuwa Wabunge, mawaziri e.t.c

Mimi sio mfuasi sana wa Siasa ila moja ya kitu kinachotukwamisha Africa ni huu mfumo wa maisha ya UJAMAA ambayo tumerithi kutoka kwa babu na Baba zetu.

Kwenye Ujamaa:
Hapa waamini katika mfumo wa kuishi kwa ujamaa,Mali, Mashamba, Viwanda humilikiwa na Mtaa, jamaa, kata, wilaya ambayo ndio Serikali yenyewe. Kwahiyo unakuta Serikali ndio Tajiri na inaendelea kujitajirisha kujitanua kila Leo. Ndio maana nchi nyingi zenye Ujamaa raia hupigania kwa jasho na damu ili kuingia Serikalini ambapo ndio SYSTEM yenyewe.

Kenge watakushambulia vibaya sana:
Kwa bahati mbaya kama unataka Vita na Raia wa Ujamaa.jaribu kuwachokonoa kwa kuleta Mada kama hizi za kupinga ujamaa.

Mfano 1:
Unakuta familia kuna Kabati lina vyombo vizuri vya kuvutia,Guess what?Vile vyombo vinaweza kumaliza miezi havitumiwi mpaka mende wanaweka makazi mule.kwasababu ni maalumu kwa WAGENI hii ndio mentallity ya Ujamaa.Yani apo zamani na mpaka sasa miji mingine ukitaka kuchezea kipigo tumia hivyo vyombo kwenye kabati ambavyo viko maalumu kwa WAGENI .Aisee unaweza kuchezea kipigo kama ngoma.
Screenshot_20231212-154749_1.jpg

Mfano 2:
Mtu mwenye Mentallity ya Ujamaa na mtu wa Ubepari wakiwa na Safari.Huyu wa ujamaa ataanza kuangalia list ya ndugu alionao kwenye Mkoa au Nchi anayoenda.Atachambua kisha atapiga simu kwa ndugu huyo kumjulisha kuwa atafikia hapo.Akifika ataweka kambi hapo haijalishi nduguye anawatoto au hana.Na huyo nduguye aliemkaribisha alivyo MJINGA kwakuwa anamentality ileile ya kuishi kwa UJAMAA atampa chumba mgeni wake pengine chumba kimoja na watoto.Unahisi kesi za Mjomba kulawiti mtoto zitaisha ??

Ila kwa mtu anaeamini "Kufa kisabuni" yani Bepari akipata safari atajianda na kutenga garama zote na yuko tayari alale Stend ila sio kufikia kwa ndugu na jamaa labda kusalimu tu kisha kwenda kutafuta Makazi ya kufikia. Mtu huyu atafungua AirBnB na kuanza kutafuta mandhari ambayo inaendana na uchumi wake ila Sio kufikia kwa Ngugu,Jamaa na Marafiki.

Watu hawa wawili watakua na Mentality tofauti kabisa mmoja atakuwa Extra miles kuliko mwingine
_913f7fa8-c638-4b5c-b689-61a559704504.jpeg

Mifano ni Mingi sana.Lakini pamoja na yote Mifumo yote inamadhaifu yake na Faida zake.Ujamaa unaleta Upendo na Ushirikiano katika Jamii. Ubepari kila mtu anabeba msalaba wake na ndio chanzo cha misongo ya mawazo kwasababu Bepari hawezi kulala kwa amani hata siku moja kutokana na Ushindani wa Mfumo huo. Ukizembea tu unaona Jirani kaongeza mjengo mara kafungua kampuni, mara kanunua Gari kali.Hapa bepari awezi kulala kwa amani hata siku moja..kichwa chake kitawaza KUONGEZA SOURCE OF INCOME ili kuCOMPETE.

Kwenye Ujamaa ndugu/Jamaa wakiwa na Jambo watashirikiana watachanga kisha baada ya shughuli kuisha huwa kunakuwa na Shuguli nyingine.Kwanza ndugu watarundikana hapo kwa mda wa wiki mpaka Miezi. Watasimuliana Umbea mpaka midomo ikauke. Kisha majungu wao kwa wao n.k Lakini kwa Bepari shughuli ikiisha na mambo yameisha Kila mtu anatawanyika kurudi kwake.kesho asubuhi KAZI INAENDELEA kama hakuna kilichokea.

Lengo la Uzi:
Mwandishi hana Nia mbaya na mfumo wa Ujamaa.Walakini Mwandishi anajaribu kuakisi uhalisia wa Maisha ya sasa na Mifumo ya Zamani ni Asi na Chanya haziwezi kupata abadani.Miaka 62 ya uhuru ni Mingi sanaa kuendelea kutumia mfumo mmoja ni uongo.Tunajidanganya wenyewe.

Ujamaa ilikua zamani kwenye Mashamba jamaa wanalima pamoja shamba la Mzee john,Kisha wanahamia kwa Shamba la Mzee Sele.wakilima kwa kula matunba na Nyimbo za kikabila.Mwisho wa siku mnakuta mmesaidiana kulima karibia wanakijiji wote.Lakini kwasasa utalima na nani kwa ujamaa wakati plau ya mchina yenye HP kama zote inawekewa wese la kutosha inalima heka na heka 100+ na zaidi?
_63c8c2b9-1603-4840-ae1d-ea95520f2522.jpeg

Je Kiongozi gani ataja badilisha mentality zetu za Ujamaa? Jibu hupati maana hata vyama vya upinzani viongozi bado mentality ni ileile hata uwape madaraka leo wataendelea pale watawala walipoishia.Je Africa tunauita mifumo ya ubepari?Maswali na majibu ni mengi.

Je nini maoni yako mdau?

Nawasilisha
 
Ujamaa ni mfumo wa kindezi sanaaaaa, ni mfumo wa nchi nzima mnaitumikia serikali na watu wake,
Raisi na mwenyekiti wa chama wanakuwa miungu watu
 
Ndio tunatakiwa tupate Vioo-Ngozi wenye Maono tofauti kidogo
 
Weka tafsiri za

Ubepari ndio nini?

Ujamaa ndio nini?

....hayo mengine ni ya kutunga na kuunga unga tu

Hatahivyo, na ieleweke wazi kabisa, kwamba COMMUNISM sio Ujamaa.

...vilevile

Ujamaa ni Self-Reliance na sio Communism kama wajanja wanavyotaka kuaminisha.

Ujamaa ni wazo, its an Idea wa kuwa unaweza kutegemea uwezo, uamuzi(judgment) na rasilimali zako badala ya kutegemea usaidizi au mamlaka kutoka nje.

Ujamaa unakuza ubunifu na uvumbuzi.

Kwenye Ubepari hukosi ubunifu na uvumbuzi ni masuala muhimu.

Ujamaa unahimiza uwajibikaji. Uwajibikaji ni kitu muhimu kwenye Ubepari

Ujamaa unakuza uhuru, uhuru ambao unathaminiwa na juhudi za kibepari ambazo zinahitaji au zinazotaka maximum profit na ufanisi.(efficiencies).

Hivyobasi, Ujamaa is useful and compliments-Ubepari yaani, vinakamilishana.

Kudai tu Ujamaa umepitwa na wakati na blah blah blah nyingine, ni kujidanganya.
 
Zote si mode za uchumi na maendeleo
Zote si Mifumo ya maisha

Ubepari-Kila mtu apambane kwenye kujenga Taifa

Ujamaa-Tushirikiane ndugu,jamaa na marafiki kwenye kujenga Taifa
 
Naomba kutofautiana.

Ujamaa unazungumzia wewe haujawahi kuwepo Tanzania.

Again, Ujamaa sio Ukomunisti Tanzania haijawahi kuwa Nchi ya Kikomyunisti

Ujamaa wa Nyerere unaitwa Self-Reliance, ikiwa ina maana hiyo hiyo ya tafsiri uliyotoa ya Ubepari- kujipambania mwenyewe.

Sasa wewe huo Ujamaa wa tushirikiane kindugu umeutoa wapi? Una ushahidi wowote ule unavyofanya kazi? Mifano n.k?
 
Mfano 1:
Unakuta familia kuna Kabati lina vyombo vizuri vya kuvutia,Guess what?Vile vyombo vinaweza kumaliza miezi havitumiwi mpaka mende wanaweka makazi mule.kwasababu ni maalumu kwa WAGENI hii ndio mentallity ya Ujamaa.Yani apo zamani na mpaka sasa miji mingine ukitaka kuchezea kipigo tumia hivyo vyombo kwenye kabati ambavyo viko maalumu kwa WAGENI .Aisee unaweza kuchezea kipigo kama ngoma.
Pole sana kwa kupata kichapo, kipigo kama ngoma. Umedundika haswa😂😂😂

Ila wewe Kenge mmoja, huo mfano wako umeutoa wapi? Anyways, huo si mfano wa Ujamaa..
It is not a representation of Ujamaa
Sema wewe umekula kichapo mpaka umewaita wazee wako Wajamaa. Hatari sana Kenge
 
Pole sana kwa kupata kichapo, kipigo kama ngoma. Umedundika haswa

Ila wewe Kenge mmoja, huo mfano wako umeutoa wapi? Anyways, huo si mfano wa Ujamaa..
It is not a representation of Ujamaa
Sema wewe umekula kichapo mpaka umewaita wazee wako Wajamaa. Hatari sana Kenge
Mfano wa ujamaa ni upi?
 
Na bwana Kenge,

Kuna kitu kinatawala sana fikra zangu.Ubepari ni mfumo wa kiuchumi ambao mali nyingi zinamilikiwa na Sekta/watu binafsi. Katika Syllabus yoote ya Tanzania masomo yote Civics, History, Economics hakuna Kipengele utachoona wameelezea vizuri mada hii yani ni ile kupita Juujuu tu. Lakini amini kama Taifa kuijua mifumo hii itasaidia sana sana sana kujikwamua kiuchumi.
View attachment 2840559

Ubepari/Capitalism
Wazungu au Makaburu kule bondeni wanashikilia uchumi kwa Mfumo huu wa Ubepari. Kwenye Ubepari kabla ya kutajirisha Serikali. Serikali inahakikisha Mali nyingi Viwanda, n.k zinamilikiwa na Watu binafsi. Yani serikali inaweka nguvu nyingi kwenye rasilimali watu.

Leo ukianza kuchambua Matajiri wa US asilimia kubwa ni watu wa Sekta Binafsi ambao hawahusiki na Serikali kabisaa.Ila ukija huku Africa chukua any Random country kisha tafuta Matajiri wa nchi hiyo 70% utakuta waliwahi kuwa Wabunge, mawaziri e.t.c

Mimi sio mfuasi sana wa Siasa ila moja ya kitu kinachotukwamisha Africa ni huu mfumo wa maisha ya UJAMAA ambayo tumerithi kutoka kwa babu na Baba zetu.

Kwenye Ujamaa:
Hapa waamini katika mfumo wa kuishi kwa ujamaa,Mali, Mashamba, Viwanda humilikiwa na Mtaa, jamaa, kata, wilaya ambayo ndio Serikali yenyewe. Kwahiyo unakuta Serikali ndio Tajiri na inaendelea kujitajirisha kujitanua kila Leo. Ndio maana nchi nyingi zenye Ujamaa raia hupigania kwa jasho na damu ili kuingia Serikalini ambapo ndio SYSTEM yenyewe.

Kenge watakushambulia vibaya sana:
Kwa bahati mbaya kama unataka Vita na Raia wa Ujamaa.jaribu kuwachokonoa kwa kuleta Mada kama hizi za kupinga ujamaa.

Mfano 1:
Unakuta familia kuna Kabati lina vyombo vizuri vya kuvutia,Guess what?Vile vyombo vinaweza kumaliza miezi havitumiwi mpaka mende wanaweka makazi mule.kwasababu ni maalumu kwa WAGENI hii ndio mentallity ya Ujamaa.Yani apo zamani na mpaka sasa miji mingine ukitaka kuchezea kipigo tumia hivyo vyombo kwenye kabati ambavyo viko maalumu kwa WAGENI .Aisee unaweza kuchezea kipigo kama ngoma.
View attachment 2840570

Mfano 2:
Mtu mwenye Mentallity ya Ujamaa na mtu wa Ubepari wakiwa na Safari.Huyu wa ujamaa ataanza kuangalia list ya ndugu alionao kwenye Mkoa au Nchi anayoenda.Atachambua kisha atapiga simu kwa ndugu huyo kumjulisha kuwa atafikia hapo.Akifika ataweka kambi hapo haijalishi nduguye anawatoto au hana.Na huyo nduguye aliemkaribisha alivyo MJINGA kwakuwa anamentality ileile ya kuishi kwa UJAMAA atampa chumba mgeni wake pengine chumba kimoja na watoto.Unahisi kesi za Mjomba kulawiti mtoto zitaisha ??

Ila kwa mtu anaeamini "Kufa kisabuni" yani Bepari akipata safari atajianda na kutenga garama zote na yuko tayari alale Stend ila sio kufikia kwa ndugu na jamaa labda kusalimu tu kisha kwenda kutafuta Makazi ya kufikia. Mtu huyu atafungua AirBnB na kuanza kutafuta mandhari ambayo inaendana na uchumi wake ila Sio kufikia kwa Ngugu,Jamaa na Marafiki.

Watu hawa wawili watakua na Mentality tofauti kabisa mmoja atakuwa Extra miles kuliko mwingine
View attachment 2840573
Mifano ni Mingi sana.Lakini pamoja na yote Mifumo yote inamadhaifu yake na Faida zake.Ujamaa unaleta Upendo na Ushirikiano katika Jamii. Ubepari kila mtu anabeba msalaba wake na ndio chanzo cha misongo ya mawazo kwasababu Bepari hawezi kulala kwa amani hata siku moja kutokana na Ushindani wa Mfumo huo. Ukizembea tu unaona Jirani kaongeza mjengo mara kafungua kampuni, mara kanunua Gari kali.Hapa bepari awezi kulala kwa amani hata siku moja..kichwa chake kitawaza KUONGEZA SOURCE OF INCOME ili kuCOMPETE.

Kwenye Ujamaa ndugu/Jamaa wakiwa na Jambo watashirikiana watachanga kisha baada ya shughuli kuisha huwa kunakuwa na Shuguli nyingine.Kwanza ndugu watarundikana hapo kwa mda wa wiki mpaka Miezi. Watasimuliana Umbea mpaka midomo ikauke. Kisha majungu wao kwa wao n.k Lakini kwa Bepari shughuli ikiisha na mambo yameisha Kila mtu anatawanyika kurudi kwake.kesho asubuhi KAZI INAENDELEA kama hakuna kilichokea.

Lengo la Uzi:
Mwandishi hana Nia mbaya na mfumo wa Ujamaa.Walakini Mwandishi anajaribu kuakisi uhalisia wa Maisha ya sasa na Mifumo ya Zamani ni Asi na Chanya haziwezi kupata abadani.Miaka 62 ya uhuru ni Mingi sanaa kuendelea kutumia mfumo mmoja ni uongo.Tunajidanganya wenyewe.

Ujamaa ilikua zamani kwenye Mashamba jamaa wanalima pamoja shamba la Mzee john,Kisha wanahamia kwa Shamba la Mzee Sele.wakilima kwa kula matunba na Nyimbo za kikabila.Mwisho wa siku mnakuta mmesaidiana kulima karibia wanakijiji wote.Lakini kwasasa utalima na nani kwa ujamaa wakati plau ya mchina yenye HP kama zote inawekewa wese la kutosha inalima heka na heka 100+ na zaidi?
View attachment 2840565

Je Kiongozi gani ataja badilisha mentality zetu za Ujamaa? Jibu hupati maana hata vyama vya upinzani viongozi bado mentality ni ileile hata uwape madaraka leo wataendelea pale watawala walipoishia.Je Africa tunauita mifumo ya ubepari?Maswali na majibu ni mengi.

Je nini maoni yako mdau?

Nawasilisha
Anaependa ujamaa ana matatizo ya akili

Ni mtu asiependa uhuru na wajibu binafsi

Wanaopenda ujamaa ni wavivu,wajanja kujificha kwenye kundi la watu

Ujamaa ukiuongelea kijuu juu unapendwa sana ila ni lethal na most brutal way of organizing society
 
Back
Top Bottom