Je, yaliyotokea Kenya, Congo, na Uganda ni kushindwa kwa ubepari?

Dua,
Mjomba hapa nakubaliana sana na Bin Maryam kwa kutazama vielelezo vilivyotangulia..
Siku zote tunasema Amani yetu imejengwa na Ujamaa lakini mbona hata Zambia na Malawi ambao walikuwa Mabepari nao wana amani kama yetu na Ukabila sii swala kabisa linaloongelewa ndani ya nchi zao... Je, ni kipi ambacho tunafanana nao hawa watu... Utakuta ni kuwa sote tulipata Uhuru wetu kibwelele yaani jitihada za Uhuru wetu hazikuanzishwa na wananchi wenyewe kwa kuingia mwituni isipokuwa sheria za UN ndiuzo zilitupa Uhuru huo laa sivyo labda who knows tungekuwa tukitawaliwa hadi leo. Na trust me kuna tofauti kubwa sana kati yetu bara na Zanzibar na ndio maana tunawaona wao kuwa wana matatizo hali sisi Bara ndio wenye matatizo na hiyo slogan ya amani na utulivu yetu.
Sasa huo utulivu wetu wa amani mahala ambapo haki zetu zinachukuliwa na wachache ati tukiita watu wa amani ni Ujanja kweli ama ndio Ujinga wenyewe?...Mbona Tanzania, Zambia na Malawi ndizo nchi ambazo tunaliwa zaidi na viongozi kila siku kazi yao ni kubadilisha mashati tu.... (Ofisi za kazi). Na sii kwamba hatujui kuwa hawa ni Mafisadi lakini ndio kwanza tunawabeba ktk KURA na kuwaita waheshimiwa.
Sasa ukirudi ktk kuuliza mchango gani Bin Maryam kautoa, mzee wangu hapo utakuwa umechukia.... maanake hapa ni kijiweni tu sote ni Wadanganyika ambao miaka yote tumeukumbatia Ujinga huo wa amani na utulivu...Lakini kama walivyosema wahenga kuwa siku zote idea huanza na mtu mmoja kisha ikapata support na mwishowe ikatumika kuleta mabadiliko na ndio changes tunazopigania hapa. Ni kutokana na michango yenu imenisaidia sana mimi hapa kutokubali kuendelea kuwa chini ya viongozi wabovu.. leo nipo mimi kesho mtampa mtu mwingine na wimbi la msukumo wa fikra hizi utazidi kupanua wigo kati ya Wadanganyika.
Hata hiyo hoja yako ya kuuliza mchango wake nadhani pia ni msukumo wa fikra ambayo kesho itampa nguvu Bin Maryam afikirie kuchangia kivitendo fikra hizi za Mapinduzi ya fikra...
I guess hapa ndipo tulipo sasa hivi ktk Mapinduzi ya fikra na labda jambo kubwa zaidi ni jinsi ya kuzieneza hizi fikra ziwafikie Wadanganyika wengi zaidi.

Mkandara:

Mtu yoyote atakayeleta suala la amani ni lazima aangalie historia yetu. Machafuko makubwa yalikuwa wakati wa majimaji na baada ya hapo nchi imekuwa ya amani.

Tunachojua ni kuwa amani siku zote inakuja na maendeleo ya kijamii. Ukiona watu wana amani kwa muda mrefu na maendeleo hayapatikani ni lazima kutakuwa na kitu kinachowakwamisha.
 
Dua:

Sidhani Mwafrika wa Kike alipoanzisha thread alikuwa na maana ya kuenzi mchango wa mwalimu kuhusu amani. Hivyo kueleza mchango wangu kulinganisha na Nyerere nitakuwa natoka nje ya mada, lakini kwa sababu umeuliza ngoja tuelimishane kama ifuatavyo.

Kila mtu ana nafasi yake katika jamii na wote hatuwezi kuwa marais kwa kipindi kimoja. Kwa mtaji huu raia yoyote wa Tanzania ambaye ametimiza wajibu wake wa kisheria kwa nchi kama vile kufanya kazi na kulipa kodi, kutofanya uhalifu AMETOA MCHANGO MKUBWA SANA KWA TAIFA KULIKO KIONGOZI WA NGAZI YA JUU AKIWEMO MWALIMU. Ni mchango wa watanzania uliofanya viongozi walipwe mishahara, wapate vyombo vya usafiri, wapate nafasi za kukaa ofisi na kufikiri wakati wengine tunafanya kazi za kutoa jasho.

Mchango wa taifa ni sawa kwenda peponi kwa muumini wa dini. Papa na muumini asiye cheo chochote katika kanisa Katoliki wana nafasi sawa za kwenda peponi, ingawaje papa anachaguliwa na kuzikwa kwa vishindo.

Sasa huo ndio ufafanuzi wako au unaamua kupindisha kile ambacho umekiandika?

Nakuwekea hapa chini jinsi ulivyoandika:


Uhuru wa Tanzania umepatikana kwa amani. Hata Zanzibar kulikotokea mapinduzi uhuru ulipatikana kwa amani.

Zambia, Malawi, Tanzania zilikuwa za nchi za amani ata kipindi wakoloni wapo. Kaunda, Kamuzu na Kambarage walichukua nchi zenye amani cha kujiuliza ni kuwa pamoja na amani na utawala wa muda mrefu hawana vielezo kwanini walishindwa. Kusema kuwa walileta amani ni kutafuta credit kwa kile kilichokuwepo.

Swali langu

Tufafanulie ni kitu gani kilichokuwepo? Au wewe binafsi ni mchango gani umetoa kulinganisha na wa Mwalimu Nyerere (RIP)kuhusiana na amani iliyopo Tanzania.

Kwenye amani unayoiongelea labda kama unataka kusema Kiswahili kuwa lugha ya taifa ni ujamaa? Kwa sababu hiyo ndio nyenzo kubwa ambayo ilikuwa ya kwanza kuweza kuwaunganisha wabongo kabla ya jambo lingine lolote na hapo credit ni kwa Julius au tukupe wewe? Ndio nikauliza where was your contribution if any? Na hili sio jambo dogo kama unavyotaka members hapa wakubaliane na wewe, lingekuwa jambo dogo Uganda, Kenya na baadhi ya nchi zingine wasingeanza kujifunza Kiswahili kwa nguvu zote.

Tukumbuke credit hutolewa kwa wale ambao ni exceptional labda uniambie u-exceptional wako wewe katika kulipa kodi etc. ...................which I believe that's normal to the majority of the citizens.

Mshikamano ambao Julius aliufanya huwezi hata kulinganisha na nchi yoyote Afrika sasa kama hapo hutaki kutoa credit wakati wengi leo hii duniani wanatoa credit napata mashaka na kusudio lako.

Mkandara

You are missing the point, angalia swala lililozuka hapo juu, Kulinganisha Tanzania na Malawi au Zambia ni matusi kwa sababu hizi ni nchi tatu tofauti unalinganisha kitu gani? Hoja yangu ukisoma hapo juu utaelewa ni kuhusu ufafanuzi wa swali na wala sio kupindisha hoja. Kenya, Malawi, Congo former Zaire, Somalia walikuwa wanajulikana kwa kutumiwa na western countries hadi leo hii hizi ni nchi ambazo zimekuwa protrayed vizuri kuliko Tanzania kwa muda mrefu na hii sio siri. Wakati wa awamu ya kwanza hatukuwa na MAFISADI kama tulivyonao leo.
 
Sasa huo ndio ufafanuzi wako au unaamua kupindisha kile ambacho umekiandika?
Nakuwekea hapa chini jinsi ulivyoandika:

Swali langu
Kwenye amani unayoiongelea labda kama unataka kusema Kiswahili kuwa lugha ya taifa ni ujamaa? Kwa sababu hiyo ndio nyenzo kubwa ambayo ilikuwa ya kwanza kuweza kuwaunganisha wabongo kabla ya jambo lingine lolote na hapo credit ni kwa Julius au tukupe wewe? Ndio nikauliza where was your contribution if any? Na hili sio jambo dogo kama unavyotaka members hapa wakubaliane na wewe, lingekuwa jambo dogo Uganda, Kenya na baadhi ya nchi zingine wasingeanza kujifunza Kiswahili kwa nguvu zote.
Tukumbuke credit hutolewa kwa wale ambao ni exceptional labda uniambie u-exceptional wako wewe katika kulipa kodi etc. ...................which I believe that's normal to the majority of the citizens.
Mshikamano ambao Julius aliufanya huwezi hata kulinganisha na nchi yoyote Afrika sasa kama hapo hutaki kutoa credit wakati wengi leo hii duniani wanatoa credit napata mashaka na kusudio lako.



Kasome shule kwanza, bishara ya utumwa na pembe za ndovu ilisambaza sana kiswahili kuliko mipango uliyoletwa baada ya uhuru. Babu yangu alisoma shule ya mjerumani alisoma kwa kiswahili. Shule za mwingereza zilifundisha kiswahili mpaka darasa la nne.

Na historia inaonyesha kuwa uhuru ulipatikana mapema kwa sababu ya kiswahili. wakati wa harakati za uhuru lugha iliyotumika ni kiswahili.

Na mchango wa Nyerere katika kiswahili ni kufanya kitumike kuanzia darasa la tano mpaka la saba. Kitendo ambacho mwenyewe alikubali kuwa alifanya makosa ambayo yameshusha kiwango cha elimu.

Kama kuna mchango aliofanya ambao unaona ni exceptional hupo lakini sio katika amani au kiswahili. Hivi ni vitu kiongozi yoyote hatakiwi kuchukua credit yoyote (period and end of story).

Na kuhusu contribution, msimamo wangu huko palepale. Kwa umri nilionao na nafasi yangu ya kijamii, kufanya kazi, kulipa kodi na kutofanya uhalifu ni mchango mkubwa kwa taifa na najivunia kwa kile nachofanya kwa taifa langu.
 

Mshikamano ambao Julius aliufanya huwezi hata kulinganisha na nchi yoyote Afrika sasa kama hapo hutaki kutoa credit wakati wengi leo hii duniani wanatoa credit napata mashaka na kusudio lako.
QUOTE]

Kaka Dua nadhani hapa hakuna anayetaka kumdiscredit mwalimu, Hapana kabisa wangu, bali watu wanaangalia reality check! Unajua mkuu ufisadi wa kipindi cha Nyerere hata ungekuwepo tulikuwa hatujui (wengi wetu), jamii ilikuwa bado kwenye usingizi, radio ilikuwa ni moja ya RTD, Kipindi hicho akina Slaa walikuwa hawana forum ya kuongelea (unakumbuka akina Mwakitwange na Jumbe waliopinga serikali na chama waliishia wapi?), Jambo Forum haikuwepo nk. Kwa hiyo kusema kwamba wakati wa Mwalimu kulikuwa hakuna UFISADI napata shaka. Kama usingekuwepo naamini kimaendeleo tungekuwa mbali. Iweje watu walivurunda mashirika na kuhamishiwa kwingine? bila kuchukuliwa hatua? ni kwamba tulikuwa hatuna wasomi? I dont buy this idea..its too apologitic.. I agree mkuu wangu kwamba Mwalimu alijitahidi sana kuijenga Tanzania lakini as any other mwananchi napata walakini na umakini wake wa sera zake za kiuchumi.

Again, kwamba watu wa nje wanamsifia mwalimu kwa hiyo na sisi tuna wajibu wa kumsifia naamini mkuu hapo umeteleza, hata WORLD BANK na BUSH si wanampa sifa kila siku Kikwete kwamba uchumi unakuwa...and on and on...je ni kweli watanzania tuna la kujivunia na utawala wa Kikwete? with BALALIS DOING THEIR THINGS UNDER HIS WATCH?? which uchumi unaokua?

Mwalimu did what any responsible citizen should do for his country. kwa hiyo na mlipa kodi, ambaye haiibii serikali, mtu mwadilifu katika utumishi wa umma, nk ni much, much much better kuliko akina Karamagi na Mramba wanao kula kodi zetu bila kuwa accountable. Mwalimu was a great leader in his own way, but its akward that with half a century of independence we are still in the deep bondage of poverty. He cant shoulder responsibility alone, but he is equally responsible, he was our captain for almost a half of that half of the century of independence!
 
Masanja,Dua,Rev.Kishoka,FMES,Bin Maryam,

..Mimi nadhani hii amani yetu inatokana na ukweli kwamba Watanzania hatuna hamu na uchu wa maendeleo.

..Inaelekea Watanzania tumeridhika sana na hali ya umasikini uliotuzunguka.

..Vilevile Watanzania tumeshindwa kuunganisha umasikini wetu na viongozi tunaowachagua.

..Watawala wetu wamevuruga nchi na uchumi lakini hatuishi kuwaenzi na kuwatukuza.
 
Ni akili ndogo tuu ya waafrika ndio maana tumefeli kila kitu na umaskini unatuandama tangu enzi na enzi,hatuwezi kujisaidia tumekalia kusafiri kwenda kuomba misaada ndio policy ya maendeleo then tunategemea tutaenda mbele,kama sio akili ndogo ni nini? wananchi wanachagua CCM kwa kishindo huku wakijua hao ndio mwanzo wa rushwa kama sio akili ndogo ni nini? rushwa ya billion 133 kwa nchi maskini kama yetu na wanaohusika bado wako kazini kama sio akili ndogo ni nini? mimi naamini hatuna akili ndio maana ni maskini,tungekuwa timamu huko vichwani tusingekula rushwa wala kuchagua wala rushwa wanaotutengenezea mifumo mibovu kwenye jamii yetu...naamini siku tukipata viongozi wenye akili tutaendelea sana.
 
Ni akili ndogo tuu ya waafrika ndio maana tumefeli kila kitu na umaskini unatuandama tangu enzi na enzi,hatuwezi kujisaidia tumekalia kusafiri kwenda kuomba misaada ndio policy ya maendeleo then tunategemea tutaenda mbele,kama sio akili ndogo ni nini? wananchi wanachagua CCM kwa kishindo huku wakijua hao ndio mwanzo wa rushwa kama sio akili ndogo ni nini? rushwa ya billion 133 kwa nchi maskini kama yetu na wanaohusika bado wako kazini kama sio akili ndogo ni nini? mimi naamini hatuna akili ndio maana ni maskini,tungekuwa timamu huko vichwani tusingekula rushwa wala kuchagua wala rushwa wanaotutengenezea mifumo mibovu kwenye jamii yetu...naamini siku tukipata viongozi wenye akili tutaendelea sana.

Kuna Mwarabu mmoja kutoka Tunisia aliandika kitabu kabla ya karne 12. Na kuna watu wanaosoma uchumi wa jamii wanadai kuwa huyu jamaa ni kama baba wa uchumi wa duniani.

Katika kitabu chake anazungumzia masuala ya utumwa. Anasema jamii nyingi zimepitia utumwa. Kilichomshangaza ni kuwa jamii zingine zilitumia utumwa kupanga ngazi kati jamii na wangine kuwa watawala. Lakini kwa watu weusi kuridhika kwa utumwa ni kilikuwa ni kitu cha kawaida. Nikipata muda naweza kukupa reference ya kitabu chenyewe.

Amani ya Tanzania ni kuridhika. Chumvi inakosekana na bado wananchi wanaandamana kumpongeza rais. Huo ni utumwa.
 
..Inaelekea Watanzania tumeridhika sana na hali ya umasikini uliotuzunguka.

..Vilevile Watanzania tumeshindwa kuunganisha umasikini wetu na viongozi tunaowachagua.

..Watawala wetu wamevuruga nchi na uchumi lakini hatuishi kuwaenzi na kuwatukuza.

Mkuu Joka,

Heshima mbele, ni kweli kabisaa hii mkuu, very strong argument mkuu.
 
Jokakuu,
Safi sana mzee wangu nakubaliana nawe mia kwa mia.

Dua,
Jamani nimesema kitu gani hapa cha kuonyesha nimerukia na kubadilisha hoja?...
Ama siruhusiwi kuchangia mada hii?...
Nalichosema mimi kinahusu mchango wa Mwalimu JKN ktk kuleta Amani na Utulivu, na kama unakumbuka huyu ndiye kipenzi changu na hata siku moja sintamweka nyuma. Lakini ktk swala hili ati kuwa yeye ndiye sababu ya kuwepo amani nchini hapo ndipo nilipotoa mawazo yangu kulingana na reality kwani hii amani tunaizungumzia leo kwa kulinganisha na nchi nyinginezo...Laa sivyo sijui ni kipimo gani kingetumika kuonyesha kuwa Tanzania tuna amani na Utulivu hali kila nchi ina amani.
Kama unakumbuka vizuri Mwalimu alipokuwa akifanya propaganda za Uhuru alikaribishwa kila mkoa na wenyeji wake Na haikuwa kazi kubwa sana kwa chama Tanu kujipatia wanachama bila kutumia nguvu....dalili ya kuwa amani ilikuwepo kabla ya hata Uhuru wetu. Nikatoa pia mfano wa Utumwa ambapo tulikusanywa kama ndama na hakuna historia ya kuonyesha resistance ya Utumwa Tanzania nzima kama sio baadhi ya chiefdom kwa kutaka gharama kubwa zaidi. In fact watumwa tuliwakusanya sisi wenyewe kina Tip Tippu (wanyapala) ati wafanya biashara na walivaa vilemba kujifananisha kama waarabu. Na hakuna historia ya kuonyesha Tip Tippu alikuwa wanted ktk maisha yake -ndio Utulivu wetu huo ulikoanzia. Tukaja tawaliwa na Mjarumani, Tunamwona Mkwawa tu aliyejaribu kupigana nao lakini wengine woote walimpokea na mnara katuachia wa Bismini ambao hadi leo ni alama kubwa ya jiji la Dar. Muingereza yale yale tena basi alikuwa bado akiendeleza biashara ya Utumwa wakati Zenj wameisha acha na kupiga marufuku...
Ndugu yangu Amani na Utulivu ni kilema kwetu ambacho kimekuwa jadi ya Mdanganyika. Kwa hali hiyo ndio maana sikubaliani na habari za kuwa Nyerere ndiye mwanzilishi wa Amani na Utulivu kwani hii ni sifa mbaya kwangu na sidhani kama inamfaa marehemu mwalimu JK Nyerere. Uzembe wa kuabudu binadamu wengine ni kimila chetu wenyewe ambacho nafikiri kimetokana na kutokuwa na ELIMU, elimu ya kuweza kutofautisha utumwa na ubwana kwani hadi leo hii tunavyozungumza heshima hupewa mwenye kitu hata kama ni jambazi na wapo wanaokaribia kumwabudu tajiri....Hii ndiyo hali halisi ya Mdanganyika ambayo hatuwezi kuiepuka sote.
Sasa, inapofikia Ufisadi kuwa ni neema yote hii imetokana na uzembe wetu wenyewe, haya Huyo Balali amnatafutwa leo hali ni serikali ilomwacha kwenda pata matibabu US...Jeetu Patel na wengine wote waliohusika na scandal zote nchini wanafika Ikulu yetu bila hodi na mitaani hupishwa viti wao wapate kukaa kwanza....
Mjomba amni usiamini tunapozungumzia Amani haina Mjamaa wala Pebari isipokuwa uongozi wa mtu. Kama Nyerere ndiye aliyeleta amani Tanzania basi hata Kaunda na Banda ndio walileta amani nchi hizo kwani nao wapo kundi moja nasi ktk kipimo cha amani, yet tunaongoza ktk umaskini....Umaskini hauchagui Mjamaa wala Bebari kama vile Amani na utulivu haina rangi.
 
Unajua mkuu ufisadi wa kipindi cha Nyerere hata ungekuwepo tulikuwa hatujui (wengi wetu), jamii ilikuwa bado kwenye usingizi, radio ilikuwa ni moja ya RTD, Kipindi hicho akina Slaa walikuwa hawana forum ya kuongelea (unakumbuka akina Mwakitwange na Jumbe waliopinga serikali na chama waliishia wapi?), Jambo Forum haikuwepo nk. Kwa hiyo kusema kwamba wakati wa Mwalimu kulikuwa hakuna UFISADI napata shaka. Kama usingekuwepo naamini kimaendeleo tungekuwa mbali. Iweje watu walivurunda mashirika na kuhamishiwa kwingine? bila kuchukuliwa hatua? ni kwamba tulikuwa hatuna wasomi?

Masanja,

Wakati wa Mwalimu, watu walikuwa waoga kuiba na hasa kijinga kama ilivyo sasa hivi watu hawana aibu wala heshima kwa mkuu wao wa kazi.

Suala si kukosekana kwa uhuru wa maoni na habari, au kukosa pa kuongelea.

Nyerere alikuwa akipenda kuwapa watu nafasi ya pile mpaka ya nne wajifunze kutokana na makosa. kuanguka kwa mashirika mengi haukutokana na Wizi au Ufisadi, bali ni mipango mibovu ya utekelezaji na udhaifu katika ufanisi.

La zaidi, mashirika haya yaliishia kuwa "welfare" organs, kutoa ajira kwa kila mtu, kutoa huduma bure za afya, nyumba, usafiri, chakula hata uniforms!

Matumizi yalizidi mapato kutokana na msukumo wa kujenga "middle class" kutumia mishahara na si ubunifu wa uzalishaji na kuruhusu ajira binafsi, kuendeleza biashara na huduma na kukuza kilimo kutoka kilimo cha heka moja na kuwa kilimo cha kibiashara!

Mwalimu alileta plan nzuri, tulimsubiri aingie kazini na afanye kila kitu yeye mwenyewe huku tukiandamana kumtukana mkoloni na kumsifu mwenyekiti huku tukikimbia umande kukwepa kwenda kazini kuwa hodari wa kazi na wabinifu.

Kaondoka Nyerere tumepata uhuru wa kuongea, kujiajiri binafsi na hata kuwa na miradi ya pembeni, lakini hali zetu ni zile zile, goi goi, wazembe, wavivu, wabangaizaji na sasa tamaa imetugeuza mafisadi!
 
Ni akili ndogo tuu ya waafrika ndio maana tumefeli kila kitu na umaskini unatuandama tangu enzi na enzi,hatuwezi kujisaidia tumekalia kusafiri kwenda kuomba misaada ndio policy ya maendeleo then tunategemea tutaenda mbele,kama sio akili ndogo ni nini? wananchi wanachagua CCM kwa kishindo huku wakijua hao ndio mwanzo wa rushwa kama sio akili ndogo ni nini? rushwa ya billion 133 kwa nchi maskini kama yetu na wanaohusika bado wako kazini kama sio akili ndogo ni nini? mimi naamini hatuna akili ndio maana ni maskini,tungekuwa timamu huko vichwani tusingekula rushwa wala kuchagua wala rushwa wanaotutengenezea mifumo mibovu kwenye jamii yetu...naamini siku tukipata viongozi wenye akili tutaendelea sana.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu....
 
Mzalendohalisi;130189]1. Tunahitaji good and strict leadership patriotic na kuwa 'dictator' kwa miaka say 15 to 20 years! Hii haihusiani na ubepari wala ujamaa! udiktator kuweka extreme strictness ktk matumizi na makusanyo ya raslimali, na kuchukua hatua kali kwa mafisadi!

2. Udiktatoship wa kizalendo pia utarejesha uzalendo wa Taifa ambao naona kama unaanza kupotea! Pia italeta displine ya kazi na kupunguza siasa- na kuzitofautisha na kazi!

3. Then we need strong institutions kusimamia haki i.e mahakama, Bunge, free media n.k and to fairly re-distribute wealth. Mf. Mtu akiiba au haruhusiwi kugombea ubunge au to take any public office!

4. Bado hadi sasa nina wasi2 kama kweli Afrika (Tz) we were ready for Multi-party. Have many parties done good or harm? Hii stage inafaa kama 1-3 have been fullfied!

5. Pia we need to look on ways to cut off foregn AID- ila kwa humanitarian reasons! Misaada ya nje imetulemaza na inaturudisha nyuma kimaendeleo!

Angalia Kenya- wale wote waliokuwa implicated ktk Angloleasing and Golderberg multi-bilion deals -kuwaibia watu maskini wamepata promotion wote ni wabunge na mawaziri! Angalia Tz mawaziri, Makatibu wakuu wana nyumba (na nje ya nchi) na mali zisizilingana na mapato yao- na wanapeta na wanapewa nafasi zaidi! Na wananchi wa kawaida wanaona!

Pia naona kama mfumo wa sheria tuliorithi UK not ideal kwetu Afrika- we need a much stricter laws, na vyombo vya dola!

Ni kama udiktator.. flani ila watu wakishazoea na kuheshimu hizi sheria ndo Afrika we shall take off!

Otherwise I see the near future of our continent glomy![/
Mzalendohalisi:

I honestly respect every word of what you said::::Ni hitimisho la Msingi la kilakitu.....Eee Mwenyenzi Mungu Ibariki Tanzania
 
Bob Mkandara,

Ukweli utajidhihirisha pale wale wenye nia ya kweli watakapoanza kujitolea bila masharti. Katika miaka yangu 10 ya mitandao hii ya Watanzania, nimejifunza mengi na kuona kwa dhati ni jinsi gani tlivyofanana na CCM na Serikali yetu.!

Rev.

That is very important indeed!!!"kujitolea bila masharti" Basicaly uongozi wa kweli haulipwi. Kufikiria vinginevyo is the root of all problems! Kama wananchi wanjitegemeea kwa jasho lao, then viogozi wajitegemee bila kuwatumia jasho la wananchi kabisa..Hakuna njia ya kweli ya kufanya hivyo..Bila kuufanya uogozi usiwe unalipwa!!! Uogozi usiwe ni capital ya aina yeyote..I am telling you this looks upside down but ..ndio jibu!!

One day i will be able to explain this much more better.

But for now, kama pakawa na sheria inayoliwezesha hilo kutekelezeka..Ni viogozi wangapi wangebakiA kazini? Ni wabunge wangapi wangebaki kwnye nyadhifa? Huwezi kuamini hao ambao wangebaki hata ungewalipa wangekuwa honest and to the people. But beliave me one day science will come up with confrmation of waht i am saying.."UNOGOZI HAULIPIKI" hasa unavyozidi kuwa wa ngazi za juu!!!Its a free thing ni almost kitu cha kujitolea tu!!!
 
1. According to UN office on drugs and crimes -nimeona hii data ktk Mkutano unaendelea Bali hii leo!

2. Je do we need AID? Tuzibe kapu linalovuja- tunaibiwa 10 times ya misaada! Sasa eti tunajivunia Tz tumeweza kuvutia misaada na JK anajipiga kifua!

Siku tukisema misaada basi- ndo tutaanza kusonga mbele na kuendelea!

The amount of money extorted and stolen each year from developing countries is over 10 times the approximately $100bn in foreign assistance being provided by all governments and civil organizations in the world.
 
Why capitalism triumphs in the West, but failed everywhere!!!? By prof. Hernando De Soto.

"A must read"
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom