Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,641
- 46,290
Edward Lowassa limekuwa jina kubwa sana katika siasa za nchi hii kwa muda akihusishwa na kutafuta kuikalia ofisi namba bila mafanikio mpaka anaondoka duniani.
Lowassa amekuwa mjadala mkubwa kuanzia kwa Nyerere mpaka leo hii ambapo hayupo duniani. Haijawahi kuwekwa wazi hasa na yeyote wa chama chake kwa nini siku zote alionekana na vigogo wa chama chake kutofaa kwa nafasi hiyo ili hali akiwa na ushawashi mkubwa mno kwa wanachama wengine wa chama chake.
Jambo kubwa ambalo limekuwa likizungumzwa sana na watu wasio vigogo wa chama chake ni ufisadi, kukosa uadilifu au kujilimbikiza mali lakini huu nao bado ni mjadala wenye kuacha maswali mengi kuliko majibu ya kueleweka.
Sijui uadilifu wa Lowassa au kama kweli alikuwa fisadi na kwa kiwango gani cha kutisha kuliko mafisadi wengine ila naamini huenda jambo lingine kubwa kumuhusu ni kwamba labda alikuwa na mawazo ya ubepari uliopitiliza.
Nchi yetu kwa muda mrefu ilikuwa ya kijamaa na hata baada ya kufunguliwa kwa uchumi wa soko huria siasa zetu hasa za kiuchumi zimeendelea kujikita katika aina fulani ya ujamaa uchwara na mabepari sio watu waliotazamwa kwa jicho zuri sana.
Sasa Lowassa inaonekana hakuwa na muegemeo wa ujamaa kabisa. Tofauti na viongozi kama Mwinyi au Mkapa ambao ubepari wao unaonekana kusukumwa zaidi na taasisi za kimataifa na hali ya halisi za nyakati Lowassa ubepari wake unaonekana ni wa kutoka moyoni kabisa au wa imani. Huenda jambo hilo ni mojawapo ya mambo ambayo yalimletea mgogano mkubwa na wafahidhina ambao ni gate keepers wa mfumo wakihofu mabadiliko makubwa ya kimfumo endapo angekamata madaraka makubwa zaidi ya nchi.