Je, yaliyotokea Kenya, Congo, na Uganda ni kushindwa kwa ubepari?

1. Tunahitaji good and strict leadership patriotic na kuwa 'dictator' kwa miaka say 15 to 20 years! Hii haihusiani na ubepari wala ujamaa! udiktator kuweka extreme strictness ktk matumizi na makusanyo ya raslimali, na kuchukua hatua kali kwa mafisadi!

2. Udiktatoship wa kizalendo pia utarejesha uzalendo wa Taifa ambao naona kama unaanza kupotea! Pia italeta displine ya kazi na kupunguza siasa- na kuzitofautisha na kazi!

3. Then we need strong institutions kusimamia haki i.e mahakama, Bunge, free media n.k and to fairly re-distribute wealth. Mf. Mtu akiiba au haruhusiwi kugombea ubunge au to take any public office!

4. Bado hadi sasa nina wasi2 kama kweli Afrika (Tz) we were ready for Multi-party. Have many parties done good or harm? Hii stage inafaa kama 1-3 have been fullfied!

5. Pia we need to look on ways to cut off foregn AID- ila kwa humanitarian reasons! Misaada ya nje imetulemaza na inaturudisha nyuma kimaendeleo!

Angalia Kenya- wale wote waliokuwa implicated ktk Angloleasing and Golderberg multi-bilion deals -kuwaibia watu maskini wamepata promotion wote ni wabunge na mawaziri! Angalia Tz mawaziri, Makatibu wakuu wana nyumba (na nje ya nchi) na mali zisizilingana na mapato yao- na wanapeta na wanapewa nafasi zaidi! Na wananchi wa kawaida wanaona!

Pia naona kama mfumo wa sheria tuliorithi UK not ideal kwetu Afrika- we need a much stricter laws, na vyombo vya dola!

Ni kama udiktator.. flani ila watu wakishazoea na kuheshimu hizi sheria ndo Afrika we shall take off!

Otherwise I see the near future of our continent glomy!
 
1
. Ugomvi wangu katika documentary hii haukuwa sana katika nani alaumiwe kwa umasikini wa bongo. Ugomvi wangu ulikuwa katika dhani nzima ya kutengeneza documentary ya kuonyesha mabaya tu katika nchi za afrika (ukichukulia kuwa hii documentary inatengenezwa na reporters ambao asili yao ni Afrika).

Binafsi ninaona kuwa waandishi wanahitaji kuonyesha mabaya zaidi kwa sababu mazuri ni machache sana yanayoendelea huku Afrika, labda kwa kufanya hivyo watatuletea attention tunayoiihitaji kama vile yaliyotokea then Eritrea, bila ya zile videos msaada wa chakula usingekuja, ndio maana waandishi wengi siku hizi wameamua kuwa specific Dafour sasa hivi bado wanasua sua kwa sababu habari mbaya zilichelewa kuwafikia huko West, hiyo ndiyo reality ya dunai ya sasa.

2.
Kitu kimoja nimegundua kuwa kuna tatizo kubwa sana Afrika zaidi ya sera zinazoongoza nchi. Hebu angalia hali ya maisha ya South Afrika leo hii. Je unaweza kusema kuwa wananchi wa kawaida kwa asilimia ngapi wanafaidika na mafanikio ya nchi hiyo?

South Afrika, ina uchumi unaoitwa Economic Condition, ambapo serikali na kikundi cha wachache tu ndio kinakuwa the baron wa uchumi, ni nchi ambayo ni karibuni tu ndio wametoka kwenye ukoloni, binafsi niaaamini kuwa kesi yao inakuwa tofauti sana na nchi kama yetu ambayo tumekuwa huru for the last 45 years, na besides, angalao wao wanajua for a fact kuwa serikali yao ni ya kibepari, sisi hatujui serikali yetu ni aina gani au?

3.
Je ni kweli Botswana ni nchi ya kibepari iwapo serikali ya nchi hiyo inafanya biashara na huduma kwa wananchi nyingi zinatolewa na serikali bure (mambo aliyojaribu kufanya nyerere na dunia nzima ikasema huo ni ujamaa)

Botswana ni nchi ya kibepari lakini yenye mfumo mzuri wa kugawana mali za taifa, ambao pia unatokana na misingi yao imara ya siasa za kidemokrasia, na kuna big respect kwa the rule of law, sera ambayo inawahikikishia taifa kusimamia mali zao za taifa kwa umakini sana na kwa faida ya taifa, hivi karibuni kulikuwa na deal kubwa sana ya madini yao, ambapo wale wale jamaa wanaomiliki madini yetu ndio wako huko, waliamua wanataka a long term deal nao, wao bungeni wakaamua kupiga kura nchi nzima kama wakubali hiyo deal au la! Wakaikubali deal hiyo na kuweka masharti ya kwamba jamaa wa madini lazima pia wajihusishe na kuwasaidia taifa kwenye ishu ya mifugo ambayo wao kama taifa wanaithamini sana ikapita, Botswana sera zao ni very close na Switzerland ni ubepari unaoheshimu demokrasia.

4.
Kuna tatizo somewhere zaidi ya ujamaa na ubepari kwa waafrika na kwa sasa ninatafuta kulijua hili tatizo.

Ni kweli mkuu Afrika kuna matatizo mengi sana, lakini binafsi ninaamini kuwa sera yoyote ambayo haiheshimu the rule of law ni doomed kabla haijaanza na ndilo tatizo kubwa sana linalotukabili Afrika, China wana sera ambazo politically ni very unconvetional kama zetu Afrika, lakini kwa sababu wanazi-back up na sheria kali kwa kila mwananchi hata awe kiongozi wa juu mafanikio yanaonekana, ingawa na wao pia wanaanza kutumbukia mtego wa condition economy, yaani utajiri wa taifa na sio wananchi, lakini at least wana something to show as opposed na sisi Afrika, kama sio bongo. Siasa za Afrika, ni too simple kuziweka kwenye ubepari na ujamaa, maana they do not fit kwenye neither,

Ni siasa za uhuni uhuni tu, lakini ni Mungu tu ndiye anayetunusuru, I mean ninaona wanajaribu ku-break down accademically kinachoendelea Afrika, betweeeen Ubepari na Ujamaa, ukweli ni kwamba none of the two ina-apply bongo au Afrika, ndio maana waandishi wa habari wanaishia kumwagiwa acid, kwenye demokrasia ya kweli huwa hakuna hayo ya acid.

Anyways ni maoni yangu tu mkuu!
 
Amani ya Tanzania imetokana na sera za awamu ya kwanza ya uongozi. Kenya walikuwa na tofauti ambazo zilikuwa zimejificha hadi wakati huu ambapo zimefumuka, ukiangalia kwa undani wamekuwa wakitumiwa sana na nchi za magharibi kuwa kama mfano lakini hakuna mfano bora hapo ulikuwa ni ukandamizaji na uporaji wa mali ya Kenya kwa mgongo wa chupa; hivi sasa hata Tanzania wanachota kama wanavyotaka baada ya kushindwa kufanya hivyo wakati wa awamu ya kwanza.

Wakati utafika hawa MAFISADI watawafikisha wananchi kuchukua sheria mikononi mwao, ni jukumu letu hasa hiki kizazi kuona Uvundo unaoendelezwa na hii awamu unakatwa tena kwa upanga ambao umeshikwa na mtu ambaye haonekani kama Invisible. Msione kimya majirani zetu hawapendi amani yetu.
 
Mkuu hayo maneno ni mazito mno. Usipoheshimu utawala wa sheria hata siku moja huweza songa mbele. Hata USA au Europe usifikiri kwamba wenzetu ni miungu watu, lakini mfumo uliopo unawafanya wawe makini na discipline na ndiyo maana wamesonga mbele. wakati kwenye banana republic za kwetu wakati machinga anayeuza sambusa mjini anaweza kukaa keko miezi sita bila dhamana, mtoto wa Kingunge au boss kama Dito anaweza kuua na kuachiwa bila hoja. kwa mwendo huo maendeleo ni the real sense of the word, tutayasikia tuu. Pre requisite yoyote ile ya maendeleo ni utawala unaoheshimu maamuzi ya wengi wakati matakwa ya wachache (minorities) yakipewa kipaumbele pia.

Waandishi hatuwatendei haki. Hivi katika yote wanayoyaliport iwe CNN, BBC au kwingineko kwani ni UONGO????? hayapo? kama hayapo hapo tunaweza kuweka mjadala mwingine! But for me, Now I have no problem with their reporting. Its the truth, ingawa inauma! Period, kama hutaki, jirekebishe! Otherwise tuache kuwalaumu. SASA HIVI KENYA WAMEIBIANA KURA, RAISI KAWA MBOGO HATA MEDIA KAZUIA, WATU WANACHINJANA, WAKIMBIZI WAMEJAA UGANDA... CNN NA BBC wakionyesha huu upuuzi, tunajifanya kuwaka eti media coverage YA WEST iko biased!! Are we real? WE ARE SO APOLOGETIC!!!!
 
Bin Maryam,
Katika nchi za Afrika mashariki: Kenya, Uganda na Tanzania. Kenya ilikuwa ni nchi ya makazi. Tanzania na Uganda zilikuwa wazalishaji tu. Faida ya makazi ni kwamba wakoloni walijenga miundo mbinu lakini wazawa walinyang'anywa ardhi. Faida ya nchi za uzalishaji, wazawa walibakia na vipande vyao vya ardhi.

katika nchi za Afrika ya kati (Rhodesia): Zambia na Malawi walikuwa wazalishaji wakati Zimbabwe yalikuwa ni wazawa walinyang'anywa vipande vya ardhi.

Mkuu wangu ktk hili mimi nina mtazamo tofauti kidogo...Upande wa pili wa shillingi hiyo hiyo ya uchumi ktk Ukoloni.
Je, huoni kama nchi ambazo umezitajja kama ni nchi za makazi ya wakoloni ni zile ambazo waingereza walikuwa wakizitawala moja kwa moja (Kenya, Zimbabwe na South Africa) kabla hata ya vita kuu ya pili hali nchi ambazo umezitaja kuwa ni za uzalishaji ni zile ambazo were under Protectorate ya Muingereza hivyo hapakuwa na ulazima wa Muingereza kuziendeleza nchi hizo kwani ktk masharti ya uwekaji sahihi za kinga hiyo ilikuwa KUTOA UHURU kwa wananchi pindi wakatakapo kuwa tayari...
Sasa Muingereza hakuwa mjinga kujenga nyumba isiyokuwa yake ndio maana inaonekana leo kuwa tulitumiwa tu kuzalisha tofauti na Kenya hali sisi sote tulitumiwa kama sehemu za Uzalishaji. Kenya ilitumika kuzalisha kwa manufaa ya Malkia yaani utawala wa Muingereza, kidogo walichopata kinatokana na umuhimu wa kuwepo vitu hivyo ktk uzalishaji. Huwezi kuwa na mashamba ya Kahawa na chai Kenya nzima bila kuwa na Usafiri mzuri, maghala na pengine kiwanda cha kutengeza mazao hayo yapate soko kwao Ulaya... Lakini je mapato ya mauzo ya kahawa na chai hiyo yalirudishwa Kenya?.. sidhani. Mimi nadhani Mjerumani hakupata muda huo wa kujenga infrastrure ya uzalishaji Tanzania na Uganda kwa sababu walikuwa na malengo ya kupanua zaidi koloni lao hali Muingereza na Mreno tayari waliisha tulia na kutazama Uchumi...
Na ukitazama Uhuru wa nchi hizi Kenya na Zimbabwe utakuta kwamba walipigana vita kumwondoa Muingereza tofauti na sisi tuliokuwa chini ya Protection...Nafikiri sio Muingereza tu tazama hata Angola na Msumbiji hizi nchi sasa hivi wanatisha ktk maendeleo kwa sababu hizohizo za Kenya na Zimbabwe yaani infrastructure (ya Kibepari) imejengwa kabla hata ya Uhuru. Kilichowachelewesha ni kuwepo kwa vita ya ndani miaka kibao laa sivyo sidhani kama wangekuwa fungu moja nasi.
 
Kuongezea tu comment zangu ktk mjadala huu nafikiri kuna kitu ambacho wengi tumekiacha kukitazama...
Kwanza nikubali kuwa hoja zilizotolewa humu ni nzito sana na zina ukweli wa hali ya juu isipokuwa kitu kimoja tumekiacha nje - SIASA.

Huwa nashindwa kabisa kuona ndani tunapozungumzia capitalism na maendeleo yake ya kiuchumi kisha tukasahau kuwa ktk maazimio yake kuna Ujenzi wa Ujamaa wao.. sawa kabisa na madai ya Ukommunist ambao wao wanaamini ujezi huo hauwezi kupatikana ikiwa mali zote zitakuwa mikononi mwa watu binafsi.
Kwa hiyo Malengo yao wote yalikuwa sawa isipokuwa njia za kupata maendeleo hayo kiuchumi yalitofautiana.. Mmoja akiamini kuwa serikali ndiyo inatakiwa ku control njia zote za uchumi wa nchi na mwingine akisema hapana.... serikali ni mweka sheria tu, serikali haiwezi ku control njia za uchumi kifanisi isipokuwa watu binafsi...mmoja akihofia hawa mabepari na hataki kuwasikia yaani haramu, hali mwingine akisema bepari sii wa kumwogopa ila kumpa kibano kisheria kumwendeleza mtu mwingine.

Nikirudi ktk kitu ambacho wengi wetu tumeshindwa kukitazama..
Jamani hamuoni kwamba nchi zote zilizowahi kupigana vita ktk kuutafuta Uhuru wao ama kumwondoa kiongozi fulani ndizo nchi zilizoendelea? imekuwaje nchi ambazo tumeupata UHURU kiulaini hadi leo pamoja na kuwepo Utandawazi na soko huria ndio kwanza tunajikokota ktk maendeleo.
Je, vita nayo ni fundisho fulani maanake nasikia hata Rwanda leo hii wamepiga hatua kubwa baada ya Genocide, Uganda nao baada ya mavita kibao leo hii wametulia wanaangalia maendeleo na viongozi wao wako makini sana kuonyesha Utawala bora...Msumbiji, Angola hali kadhalika. Nchi kama Kenya, Zambia na Malawi baada ya kumwondoa Mkoloni kizazi hiki kimesahau kabisa athari za vita yaani wame relax na sasa hivi wamekuwa wagumu kuelewa nini Utawala bora baada ya kuwepo amani nchini mwao kwa miaka mingi.
Tanzania ndio ussiseme kabisa hatuna historia hiyo, hivyo kuwafanya viongozi wasifahamu sababu ya kuwa na good governance...waogope kitu gani hasa?..

Ni ktk kujiuliza kwangu... Mhhhhhnnnn!
 
Ufanisi, Umakini, Ufuatiliaji, Uhakiki!

Azimio la Arusha lilisema kuwania ni kujenga Taifa huru lenye kujitegemea na kuishi kijamaa. Ujamaa unaozungumzwa ni wa rangi mbili. Rangi moja ni U-Karl Marx na wa pili ni African Socialism.

Azimio lilisema, pamoja na kwamba ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, pia lilisema kuwa kuboresha Juhudi na Marifa kwatika shughuli za uzalishaji mali.

Aidha, Azimio lazungumzia miiko ya uongozi na kufuata sheria katika Uzalishaji na kuzuia Unyonyaji na Dhuluma!

Sisi waafrika,tumebahatika kwa warithi wa miundo ya uzalishaji mali za kilimo,viwanda, biashara na huduma kutoka kwa Wakoloni. Jamii zetu za miaka 300-1000 iliyopita zilikuwa na mfumo tofauti kabisa wa uzalishaji mali na hata vitendea kazi pamoja na juhudi na maarifa zilikuwa tofauti sana na hali tuliyonayo leo hii.

Kilichotokea Afrika kuendelea kuwa kiwanda cha mali ghafi na hivyo kubobea kuwa Masikini si Ukoloni au kupotoka kwa kushindwa kuamua ni mfumo gani wa kiuchumi (kwa tasfiri za kimagharibi) unatufaa Ujamaa au Ubepari, bali ni Uvivu. Uvivu wa kufikiri, uvivu wa ubunifu, uvivu wa kufanya kazi, uvivu kuwa na ufanisi bora, uvivu wa kuwa makini, uvivu wa kuwa wafuatiliaji na uhakiki.
Ama tumejaliwa na Uzembe wa kubuni, kufikiri, kuhamasisha, kufuatilia, umakini na uhakiki. Zaidi tumeshiba Unyonge, wa kushindwa kusimama kidete, wa kugoma kuburuzwa, kunyanyaswa, kudhulumiwa na kudhihakiwa.

Wiki mbili niliongea na rafiki yangu ambaye yuko jikoni, nikaleta suala la Azimio. Yeye akanihoji kama naamini Mfumo Huru wa Uzalishaji mali. Nikamwambia ndio naaamini kuwepo kwa ushindani na uruhusu wa Mfumo huru wa Uzalishaji na Masoko. Lakini nikamwambia, Kuwepo huku, lazika kuwe na uratibu mkali wa kisheria utakaohakikisha haki kwa wote wanaohusika iwe ni mwekezaji, wafanyakazi wake hata watumiaji wa bidhaa.

Umasikini wa Waafrika kwa sasa hivi ni wa kujitakia na si kuendelea kulaumu Ukoloni na nchi za Kibepari au Ujamaa.

Nitachukua nchi moja kama mfano, Tanzania. Ni vipi Tanzania nchi yenye utajiri mkubwa wa Asili ambao kila leo twafukua hazina mpya yaendelea kuwa mtegemezi mkubwa wa misaada na mikopo na tunashindwa kujiendesha kwa kuboresha shughuli za uzalishaji mali?

Kwanza,tumelea Uzembe, Uvivu, Uzururaji na Unyonge. Pili uzembe huu umesababisha tukimbilie kuwa na Tamaa, Ulafi, Uroho na kukosa Uadilifu. Tatu, tuna Tukuza kila mgeni na kumuona ndio suluhisho la udhaifu wetu.

Ni ugumu gani uliopo ukiondoa yale tusiyonauwezo nayo kufanya Tanzania ilishe Afrika Mashariki na Kati? Tuna maziwa, mito na ardhi yenye rutuba. Tuna watu wa kutosha kwenye sekta ya kilimo hata kama wao ni wakulima wadogo wadogo.

Tusiendelee kusingizia ujamaa ndio umetupumbaza maana Ujamaa ulilenga kutoa nafasi sawa na haki kwa kila mmoja wetu kutumia juhudi zake na maarifa kujiendeleza.

Kilichotokea ni utekelezaji mbovu wa sera, ufanisi mdogo na umakini dhaifu wa uongozi na uzalishaji mali, kukosekana kwa ufuatiliaji na kujisahihisha pale tulipokosea na hivyo kukimbilia kuzaa Tamaa ambazo zimeleta na kustawisha Rushwa, Wizi, Uhujumu, Dhuluma na Ufisadi.

Ni sisi Wananchi wenyewe tulio na nguvu ya kusahihisha hili.

Kitila atawaambia jiungeni CHADEMA. Mwanakijiji atasema fuatilieni hizi habari KLH news, Mimi napiga kampeni ya kufufua Utaifa kwa kurekebisha Katiba na kulirudia Azimio la Arusha. Bubu, Lunyungu, MwK, Game na Mtanzania wanaanika skandali za Ufisadi, Mkandara anatoa busara.

Sasa hii ni dalili tosha kuwa Uwezo tunao, Nia tunayo na Sababu tunazo kujirekebisha na kuwa taifa lenye kujitegemea na kutumia rasilimali zake kwa uadilifu na kwa manufaa ya Wananchi kama Botswana au Sweden.

Mwafrika wa Kike, naelewa dhumuni lako kuhoji hiyo filamu na kuhusu mada kuu kuonyesha udhaifu na si mazuri ya Serengeti na Mr. Nice. Lakini uelewekuwa jamii yetu ipo njia panda. Njia moja ni kuamka na kujirekebisha na nja ya pili ni kuzubaa na kuendelea kuangamia.

Madhali nguvu zetu hapa JF ni kulijenga Taifa letu na kulinda rasilimali zake, hivyo basi tusiishe kuwa wahubiri, bali tuanze kuwa wafanisi na makini katika mahubiri yetu na kuyaainisha kwa Wananchi wa Tanzania ili waone kuwa si ngonjera tuu, bali kila linalosemwa lawezekana, mtaji mkuu ni utashi binafsi kwa kutumia juhudi na maarifa kujiletea maendeleo binafsi na ya kitaifa.

We need to increase efficiency, we need to be competent, we have to desire to be accountable and above all, we need to have morals that are self motivated and also guided by fair laws governed by workable constitution for Watanzania!

Demokrasia ya kweli haitakaa itokee tukiendelea kuwa masikini. Utajiri na maendeleo hayawezi kuja kama tutaendelea kukosa uadilifu na msukumo wa kufanya kazi, kulegalega katika kuwa wabubunifu au kudumisha uzalishaji mdogo mdogo wa kilimo, mifugo, uvuvi, biashara, viwanda na huduma.
 
Rev.

Rule of Law kwanza na watu kuheshimu sheria awe mtawala au mtawaliwa! Strong Institituons of Law and Order- watu waogope serikali! Pia waheshimu kazi na kuwa waadilifu!

Huwezi ongelea uzalendo wakati watu wanaiba mabilioni na wanapenta na ndo wanaongezewa vyeo!
 
Rev. Kishoka,
Ulosema yote kweli tupu na nadhani ndicho alichokuwa akisisitiza sana Taasisi. Mimi nilikuwa msitari wambele toka miaka hiyo ya 2000 lakini imeniuwia vigumu sana kuamini kwamba tupo wengi wenye kuhitaji mabadiliko na nadhani mamluki hapa JF ni wengi zaidi ya wale wanaotaka kuona mabadiliko.
Na kutokana na hofu hiyo ya Kibongo kuwa utaachwa peke yako kwenye mataa nimekuwa napingana sana na imani yangu ktk mabadiliko na hata kuna baadhi ya hoja zangu zimemkatisha nguvu kabisa Taasisi.
Biashara ya siasa tanzania ni sawa kabisa na vitendo vyetu yaani watu tupo radhi kuchangia harusi kwa mamillioni ya fedha lakini sio Elimu ya watoto wetu. Na tukirudi ktk kutoa hoja utaona Wadanganyika wengi wanashangaa tabia hii hali ni wao wachangiaji wakubwa hali watoto wao hawana elimu...
Kazi kubwa kufahamu nini Mdanganyika anafikiria...
 
Rev.
Rule of Law kwanza na watu kuheshimu sheria awe mtawala au mtawaliwa! Strong Institituons of Law and Order- watu waogope serikali! Pia waheshimu kazi na kuwa waadilifu!
Huwezi ongelea uzalendo wakati watu wanaiba mabilioni na wanapenta na ndo wanaongezewa vyeo!

Mzalendo,

Namba nirudie nilichosema hapo juu
We need to increase efficiency, we need to be competent, we have to desire to be accountable and above all, we need to have morals that are self motivated and also guided by fair laws governed by workable constitution for Watanzania!

Sasa kama hivi si vigezo vya uzalendo, basi sijui ni mfumo gani au ni jisnsi ganitutapata maendeleo ya kizalendo!
 
Rev. Kishoka,
Mimi nilikuwa msitari wambele toka miaka hiyo ya 2000 lakini imeniuwia vigumu sana kuamini kwamba tupo wengi wenye kuhitaji mabadiliko na nadhani mamluki hapa JF ni wengi zaidi ya wale wanaotaka kuona mabadiliko...Kazi kubwa kufahamu nini Mdanganyika anafikiria...

Bob Mkandara,

Ukweli utajidhihirisha pale wale wenye nia ya kweli watakapoanza kujitolea bila masharti. Katika miaka yangu 10 ya mitandao hii ya Watanzania, nimejifunza mengi na kuona kwa dhati ni jinsi gani tlivyofanana na CCM na Serikali yetu.

Tumegawanyika kati ya wale wanaotaka maendeleo ya kweli kwa ajili ya Taifa na wale wanaotangaza maendeleo na vita vya uhujumu huku wao wakiwa wameridhika na hali halisi(kelele nyingi, bila tija kutatua matatizo).

Na hii ndio taswira ya Taifa letu na Bara letu la Afrika.

Kina Ngouabi, Lumumba, Cabral, Sekou Toure, Kaunda, Tafaa Balewa, Ben Bela, Nkrumah, Nyerere, Kenyatta, Nasser na Mandela walikuwa ni waasisi waliokuwana mawazo na maono ya mbali. Haikuwa lazima kwa wao kuwa ndio Watendaji na Wafuatiliaji wa kila kitu na kila siku.

Tunahitaji kuanza kuzalisha Taifa la visionaries kama kina Nyerere. Tunahitaji kuzalisha Taifa la Wabunifu kama Bwana Mianzi wa Iringa, tunahitaji kulea taifa la uadilifu na ufanisi kama Mzee Ben Mulokozi aliyekuwa Utumishi. Tunataka tuwe na wachapakazi kama Sokoine.

We need to quadruple our efforts to obtain these caliber of individuals to make progress!
 
Bin Maryam,

Mkuu wangu ktk hili mimi nina mtazamo tofauti kidogo...Upande wa pili wa shillingi hiyo hiyo ya uchumi ktk Ukoloni.
Je, huoni kama nchi ambazo umezitajja kama ni nchi za makazi ya wakoloni ni zile ambazo waingereza walikuwa wakizitawala moja kwa moja (Kenya, Zimbabwe na South Africa) kabla hata ya vita kuu ya pili hali nchi ambazo umezitaja kuwa ni za uzalishaji ni zile ambazo were under Protectorate ya Muingereza hivyo hapakuwa na ulazima wa Muingereza kuziendeleza nchi hizo kwani ktk masharti ya uwekaji sahihi za kinga hiyo ilikuwa KUTOA UHURU kwa wananchi pindi wakatakapo kuwa tayari...
Sasa Muingereza hakuwa mjinga kujenga nyumba isiyokuwa yake ndio maana inaonekana leo kuwa tulitumiwa tu kuzalisha tofauti na Kenya hali sisi sote tulitumiwa kama sehemu za Uzalishaji. Kenya ilitumika kuzalisha kwa manufaa ya Malkia yaani utawala wa Muingereza, kidogo walichopata kinatokana na umuhimu wa kuwepo vitu hivyo ktk uzalishaji. Huwezi kuwa na mashamba ya Kahawa na chai Kenya nzima bila kuwa na Usafiri mzuri, maghala na pengine kiwanda cha kutengeza mazao hayo yapate soko kwao Ulaya... Lakini je mapato ya mauzo ya kahawa na chai hiyo yalirudishwa Kenya?.. sidhani. Mimi nadhani Mjerumani hakupata muda huo wa kujenga infrastrure ya uzalishaji Tanzania na Uganda kwa sababu walikuwa na malengo ya kupanua zaidi koloni lao hali Muingereza na Mreno tayari waliisha tulia na kutazama Uchumi...
Na ukitazama Uhuru wa nchi hizi Kenya na Zimbabwe utakuta kwamba walipigana vita kumwondoa Muingereza tofauti na sisi tuliokuwa chini ya Protection...Nafikiri sio Muingereza tu tazama hata Angola na Msumbiji hizi nchi sasa hivi wanatisha ktk maendeleo kwa sababu hizohizo za Kenya na Zimbabwe yaani infrastructure (ya Kibepari) imejengwa kabla hata ya Uhuru. Kilichowachelewesha ni kuwepo kwa vita ya ndani miaka kibao laa sivyo sidhani kama wangekuwa fungu moja nasi.

Komredi Mkandara:

Nakubaliana na mawazo yako kwa asilimia 100. Lakini posti yangu ilikuwa inamjibu utangulizi wa Thread hii iliyotolewa na mwafrika wa kike

Katika utangulizi waandishi wanaonyesha kuwa moja ya matatizo ya nchi za kiafrika zilizofuata ubepari kama Kenya ni Slum na watoto wazururaji walio wengi ukilinganisha na nchi zilizofuata ujamaa kama Tanzania.

Analysis yangu inaonyesha kuwa nchi zilizokuwa kama makazi zilipata faida ya kuendelezwa katika miundo mbinu. Na hii inasaidiwa na mchango wa posti yako. Lakini wazawa wa nchi hizo walinyang'anywa ardhi zao. Na kunyang'anywa kwa ardhi kulisababisha wazawa kutokuwa na makazi na kuwa chanzo cha slums.

Matatizo ya slums Kenya, Zimbwabwe au South Afrika chanzo chake sio ubepari au ujamaa baada ya uhuru. Tatizo kubwa ni kuwa yalikuwa makoloni ya makazi na sheria za ardhi ziliwabana wazawa.

Wakati Tanzania inapata uhuru zaidi ya 75% ilikuwa bado haitumiki. Na Ujamaa haukufanya lolote katika mambo ya kupunguza Slums kwa sababu hatukuwa koloni la makazi.

Hivyo kutumia kigezo cha slums na watoto wazururaji kuonyesha mafanikio na mapungufu ya ujamaa na ubepari kunaonyesha ni jinsi gani waandishi wetu wanavyochambua mambo juujuu tu bila kuangalia kiini cha matatizo yenyewe.

Angola ni moja ya nchi yenye watoto wengi wazururaji na slums. Chanzo kikubwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe na sio ubepari au ujamaa.
 
Amani ya Tanzania imetokana na sera za awamu ya kwanza ya uongozi. Kenya walikuwa na tofauti ambazo zilikuwa zimejificha hadi wakati huu ambapo zimefumuka, ukiangalia kwa undani wamekuwa wakitumiwa sana na nchi za magharibi kuwa kama mfano lakini hakuna mfano bora hapo ulikuwa ni ukandamizaji na uporaji wa mali ya Kenya kwa mgongo wa chupa; hivi sasa hata Tanzania wanachota kama wanavyotaka baada ya kushindwa kufanya hivyo wakati wa awamu ya kwanza.

Wakati utafika hawa MAFISADI watawafikisha wananchi kuchukua sheria mikononi mwao, ni jukumu letu hasa hiki kizazi kuona Uvundo unaoendelezwa na hii awamu unakatwa tena kwa upanga ambao umeshikwa na mtu ambaye haonekani kama Invisible. Msione kimya majirani zetu hawapendi amani yetu.

Dua:

Uhuru wa Tanzania umepatikana kwa amani. Hata Zanzibar kulikotokea mapinduzi uhuru ulipatikana kwa amani.

Zambia, Malawi, Tanzania zilikuwa za nchi za amani ata kipindi wakoloni wapo. Kaunda, Kamuzu na Kambarage walichukua nchi zenye amani cha kujiuliza ni kuwa pamoja na amani na utawala wa muda mrefu hawana vielezo kwanini walishindwa. Kusema kuwa walileta amani ni kutafuta credit kwa kile kilichokuwepo.
 
1

Binafsi ninaona kuwa waandishi wanahitaji kuonyesha mabaya zaidi kwa sababu mazuri ni machache sana yanayoendelea huku Afrika, labda kwa kufanya hivyo watatuletea attention tunayoiihitaji kama vile yaliyotokea then Eritrea, bila ya zile videos msaada wa chakula usingekuja, ndio maana waandishi wengi siku hizi wameamua kuwa specific Dafour sasa hivi bado wanasua sua kwa sababu habari mbaya zilichelewa kuwafikia huko West, hiyo ndiyo reality ya dunai ya sasa.

2. South Afrika, ina uchumi unaoitwa Economic Condition, ambapo serikali na kikundi cha wachache tu ndio kinakuwa the baron wa uchumi, ni nchi ambayo ni karibuni tu ndio wametoka kwenye ukoloni, binafsi niaaamini kuwa kesi yao inakuwa tofauti sana na nchi kama yetu ambayo tumekuwa huru for the last 45 years, na besides, angalao wao wanajua for a fact kuwa serikali yao ni ya kibepari, sisi hatujui serikali yetu ni aina gani au?

3. Botswana ni nchi ya kibepari lakini yenye mfumo mzuri wa kugawana mali za taifa, ambao pia unatokana na misingi yao imara ya siasa za kidemokrasia, na kuna big respect kwa the rule of law, sera ambayo inawahikikishia taifa kusimamia mali zao za taifa kwa umakini sana na kwa faida ya taifa, hivi karibuni kulikuwa na deal kubwa sana ya madini yao, ambapo wale wale jamaa wanaomiliki madini yetu ndio wako huko, waliamua wanataka a long term deal nao, wao bungeni wakaamua kupiga kura nchi nzima kama wakubali hiyo deal au la! Wakaikubali deal hiyo na kuweka masharti ya kwamba jamaa wa madini lazima pia wajihusishe na kuwasaidia taifa kwenye ishu ya mifugo ambayo wao kama taifa wanaithamini sana ikapita, Botswana sera zao ni very close na Switzerland ni ubepari unaoheshimu demokrasia.

4.

Ni kweli mkuu Afrika kuna matatizo mengi sana, lakini binafsi ninaamini kuwa sera yoyote ambayo haiheshimu the rule of law ni doomed kabla haijaanza na ndilo tatizo kubwa sana linalotukabili Afrika, China wana sera ambazo politically ni very unconvetional kama zetu Afrika, lakini kwa sababu wanazi-back up na sheria kali kwa kila mwananchi hata awe kiongozi wa juu mafanikio yanaonekana, ingawa na wao pia wanaanza kutumbukia mtego wa condition economy, yaani utajiri wa taifa na sio wananchi, lakini at least wana something to show as opposed na sisi Afrika, kama sio bongo. Siasa za Afrika, ni too simple kuziweka kwenye ubepari na ujamaa, maana they do not fit kwenye neither,

Ni siasa za uhuni uhuni tu, lakini ni Mungu tu ndiye anayetunusuru, I mean ninaona wanajaribu ku-break down accademically kinachoendelea Afrika, betweeeen Ubepari na Ujamaa, ukweli ni kwamba none of the two ina-apply bongo au Afrika, ndio maana waandishi wa habari wanaishia kumwagiwa acid, kwenye demokrasia ya kweli huwa hakuna hayo ya acid.

Anyways ni maoni yangu tu mkuu!

FM:

Napata faraja kubwa kuona sipo peke yangu. Ni lazima tukubali kuwa tunachemsha. Na hii tabia ya kupata credit kwa vitu vidogo vidogo sioni kama kuna umuhimu wake.

Bottom Line: Kuna common denominator katika nchi za kiafrika ambavyo vinasababisha umasikini. Na common denominator hiyo sio ubepari au ujamaa.

Kenya ambayo ilikuwa ni nchi ya kibepari kwa mawazo ya wengi bado ilikuwa na mashirika ya umma ambayo uendeshaji wake ulikuwa wa kijomba-jomba sawa na yale ya Tanzania.

Na Tanzania ambayo ilikuwa ni nchi ya kijamaa bado ilikuwa na sekta binafsi ambayo waendeshaji wake walipata matatizo na serikali zao kama wafanyabiashara wengine katika nchi za kiafrika zisizo za kijamaa.

Kitendawili kiwe ni nini hiyo Common Denominator (CD) yetu au zetu? Katika mijadala yetu kisingizio mbona Kenya wako nyuma, mbona Ghana wako nyuma. Je insparation ni lazima itoke Afrika na sio Malaysia au Vietnam?

CD ninayoiona mimi ni naivette katika mambo ya finance. Tumekuwa kama mfano ya Bwana Yesu. Wenzetu wakipata pesa wanataka kuziongeza na sisi tunazifukia udongoni.
 
Mzee ES napenda ujue kuwa Afrika kusini ilipata uhuru mwaka 1910 kutoka kwa Uingereza, na baada ya hapo kulikiwa na utawala wa wachache mpaka mandela alipoingia madarakani!
I know others can question this!
 
Tanzania ubepari na ujamaa vytoe haviwezi kuwa na mafanikio. Kwa sasa inaonekana kuwa ufisadi ndio unafanikiwa zaidi. Tungeweza kusema kama Tanzania imefanikiwa au haijafanikiwa, kama kusingekuwa na ufisadi na mismanagement ya uchumi!
 
Mzee ES napenda ujue kuwa Afrika kusini ilipata uhuru mwaka 1910 kutoka kwa Uingereza, na baada ya hapo kulikiwa na utawala wa wachache mpaka mandela alipoingia madarakani!
I know others can question this!

Mkuu nimekusikia, lakini ninaaamini kuwa you got the my point, tuendelee kumkoma nyani mkuu!
 
Dua:

Uhuru wa Tanzania umepatikana kwa amani. Hata Zanzibar kulikotokea mapinduzi uhuru ulipatikana kwa amani.

Zambia, Malawi, Tanzania zilikuwa za nchi za amani ata kipindi wakoloni wapo. Kaunda, Kamuzu na Kambarage walichukua nchi zenye amani cha kujiuliza ni kuwa pamoja na amani na utawala wa muda mrefu hawana vielezo kwanini walishindwa. Kusema kuwa walileta amani ni kutafuta credit kwa kile kilichokuwepo.

Tufafanulie ni kitu gani kilichokuwepo? Au wewe binafsi ni mchango gani umetoa kulinganisha na wa Mwalimu Nyerere (RIP)kuhusiana na amani iliyopo Tanzania.
 
Dua,
Mjomba hapa nakubaliana sana na Bin Maryam kwa kutazama vielelezo vilivyotangulia..
Siku zote tunasema Amani yetu imejengwa na Ujamaa lakini mbona hata Zambia na Malawi ambao walikuwa Mabepari nao wana amani kama yetu na Ukabila sii swala kabisa linaloongelewa ndani ya nchi zao... Je, ni kipi ambacho tunafanana nao hawa watu... Utakuta ni kuwa sote tulipata Uhuru wetu kibwelele yaani jitihada za Uhuru wetu hazikuanzishwa na wananchi wenyewe kwa kuingia mwituni isipokuwa sheria za UN ndiuzo zilitupa Uhuru huo laa sivyo labda who knows tungekuwa tukitawaliwa hadi leo. Na trust me kuna tofauti kubwa sana kati yetu bara na Zanzibar na ndio maana tunawaona wao kuwa wana matatizo hali sisi Bara ndio wenye matatizo na hiyo slogan ya amani na utulivu yetu.
Sasa huo utulivu wetu wa amani mahala ambapo haki zetu zinachukuliwa na wachache ati tukiita watu wa amani ni Ujanja kweli ama ndio Ujinga wenyewe?...Mbona Tanzania, Zambia na Malawi ndizo nchi ambazo tunaliwa zaidi na viongozi kila siku kazi yao ni kubadilisha mashati tu.... (Ofisi za kazi). Na sii kwamba hatujui kuwa hawa ni Mafisadi lakini ndio kwanza tunawabeba ktk KURA na kuwaita waheshimiwa.
Sasa ukirudi ktk kuuliza mchango gani Bin Maryam kautoa, mzee wangu hapo utakuwa umechukia.... maanake hapa ni kijiweni tu sote ni Wadanganyika ambao miaka yote tumeukumbatia Ujinga huo wa amani na utulivu...Lakini kama walivyosema wahenga kuwa siku zote idea huanza na mtu mmoja kisha ikapata support na mwishowe ikatumika kuleta mabadiliko na ndio changes tunazopigania hapa. Ni kutokana na michango yenu imenisaidia sana mimi hapa kutokubali kuendelea kuwa chini ya viongozi wabovu.. leo nipo mimi kesho mtampa mtu mwingine na wimbi la msukumo wa fikra hizi utazidi kupanua wigo kati ya Wadanganyika.
Hata hiyo hoja yako ya kuuliza mchango wake nadhani pia ni msukumo wa fikra ambayo kesho itampa nguvu Bin Maryam afikirie kuchangia kivitendo fikra hizi za Mapinduzi ya fikra...
I guess hapa ndipo tulipo sasa hivi ktk Mapinduzi ya fikra na labda jambo kubwa zaidi ni jinsi ya kuzieneza hizi fikra ziwafikie Wadanganyika wengi zaidi.
 
Tufafanulie ni kitu gani kilichokuwepo? Au wewe binafsi ni mchango gani umetoa kulinganisha na wa Mwalimu Nyerere (RIP)kuhusiana na amani iliyopo Tanzania.

Dua:

Sidhani Mwafrika wa Kike alipoanzisha thread alikuwa na maana ya kuenzi mchango wa mwalimu kuhusu amani. Hivyo kueleza mchango wangu kulinganisha na Nyerere nitakuwa natoka nje ya mada, lakini kwa sababu umeuliza ngoja tuelimishane kama ifuatavyo.

Kila mtu ana nafasi yake katika jamii na wote hatuwezi kuwa marais kwa kipindi kimoja. Kwa mtaji huu raia yoyote wa Tanzania ambaye ametimiza wajibu wake wa kisheria kwa nchi kama vile kufanya kazi na kulipa kodi, kutofanya uhalifu AMETOA MCHANGO MKUBWA SANA KWA TAIFA KULIKO KIONGOZI WA NGAZI YA JUU AKIWEMO MWALIMU. Ni mchango wa watanzania uliofanya viongozi walipwe mishahara, wapate vyombo vya usafiri, wapate nafasi za kukaa ofisi na kufikiri wakati wengine tunafanya kazi za kutoa jasho.

Mchango wa taifa ni sawa kwenda peponi kwa muumini wa dini. Papa na muumini asiye cheo chochote katika kanisa Katoliki wana nafasi sawa za kwenda peponi, ingawaje papa anachaguliwa na kuzikwa kwa vishindo.
 
Back
Top Bottom