Je, Walimu wa Tanzania hawajitambui?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,159
Habari!

Walimu ndio wenye number kubwa katika utumishi wa umma wakifuatiwa na wanajeshi, polisi na kada zingine.
Zamani nikipohoji kwanini maslahi ya Walimu ni kidogo nikaambiwa kwakuwa idadi yao ni kubwa hivyo kama ukiwalipa pesa nyingi serikali itakuwa na mzigo mkubwa zaidi.

Hili jibu kumbe halina ukweli. Jibu la ukweli ni kwamba serikali inakulipa kulingana na utashi (ufahamu wako).
Serikali imeona kuwa hili kundi halina utashi kichwani ndio maana huwalipa pesa kidogo. Kama walishindwa kudai haki zao za msingi kipindi cha nyuma ambapo mtaani hapakuwa na walimu wasio na ajira sasa kipindi hichi ambacho wakitaka kuinua kinywa tu wataambiwa tutaajiri wengine ku-replace nafasi zenu wataufyata na kulia wenyewe vyumbani mwao.

Unaendeaje likizo ya malipo bila kulipwa? Huu sio utahira? Wengine mpaka wanahamishwa na kuhamia kituo B pesa wanaisubiria wakiwa wanapiga kazi. Serikali Ina pesa nyingi tu, kucheleweshewa maslahi yao ni kwasababu ya uzwazwa uliomo kichwani mwao. Mbona wàbunge wakistaafu mamilioni yao wanayapata ndani ya siku chache?

Leo hii Walimu hutumiwa na wanasiasa kujiimarisha huku maticha wenyewe wakipiga makofi . Kada zingine wakiwa na semina malipo hufuata miongozo ya kiutumishi. Mwalimu anaweza kufanyiwa semina siku 5 akaambulia laki 2.5 huku watumishi wengine hizo siku tano wanaweza kulipwa mara 2 au mara 4 ya malipo ambayo amelipwa mwalimu.

Walimu wanaweza kufanyishwa semina leo wakalipwa miezi 3 mbele huku kada zingine wañalipwa ndani mara tu wakimaliza semina.
 
Sekta ya elimu haiingizi Pato serikalini yenyewe inatumia tu, ulitaka wafanane na madini, TRA, Bandari au Maliasili
Sawa. Haya niambie NEC wanaingiza pato kwa taifa?

Diploma holder wa NEC mwenye mkataba wa permanent anamzidi mshahara mwalimu wa TGTS E na ana posho ambazo anaweza kuwalipa posho wakuu wa shule zaidi ya 3 maana posho za wakuu wa shule hazizidi 250k.
Tafuta la kujitetea, that's why tunawaita nyie wapumbavu.

Serikali ina taasisi takribani 450 hebu fanya utafiti wa maslahi ya wenzenu akili zenu zifunguke.
PCCB wanazalisha?

Nikutajie taasisi zingine zenye mishahara minono ingawa shughuli zao hazihusiani na uzalishaji?
 
We dogo ni kima.
 
Wewe mshahara wako ni sh ngapi? Tuanzie hapa kwanza.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Heading umeuliza Swali, Chini umejijibu mwenyewe. Atakayekinzana na wewe unamshambulia.

Umeamka na hasira hasira tu, najua mambo mengi kuhusu walimu, wewe ualimu kuna namna unakuhusu, na kuna namna umekula za uso, unataka kujitenga na wenzako.

aliyeko nje hawezi poteza mda wote huo kufuatilia hayo, na kua na povu lote hilo, kwa asilimia kubwa utakua ni mwalimu, kama sivyo unapambana na Ajira za ualimu.

Utabisha hapa ila ukweli unaujua, ni hivi, njia pekee ya kupata unachokipanda ni kupambana na mwenyewe sio ajira, nguvu, akili na muda wako ndio viamue kipato chako, sio Mwajiri.
 
Back
Top Bottom