kibakulism
New Member
- Aug 13, 2023
- 1
- 2
Walimu wa ajira ya 2019 May, katika halmashauri ya wilaya Ruangwa -lindi, hatujalipya pesa ya kujikimu tangu kuajiriwa kwetu.
Kilichotokea ni kwamba, tulivyoajiriwa na serkali mwezi mei 2019, serkali ilituma pesa za kujikimu ili tulipwe, lakini pesa hivyo, ikatokea sintofahamu na hazikulipwa.
Baada ya kufuatilia tukaambiwa ni kweli pesa zililetwa ila hazikuwa na kifungu, kwahiyo kwakuwa ilikuwa mwishoni mwa mwaka wa serkali (yaani mwezi wa sita mwishoni), kwahiyo serkali ilizirudisha pesa hizo hazina.
Tukaulizia halmashauri zingine zikiwemo na za mkoa lindi, ajira mpya wote wamepata. Tukawauliza mbona wengine wamelipwa sehemu zingine, wakasema ngoja tunaziomba tena hazina mtapewa.
Tukawaomba watuandikie barua hayo majibu, lakini mpaka leo barua hatujapewa.
Hatukuishia hapo, kulikuwa na usahihishaji wa mtihani wa mkoa Nachingwea, baada ya kumaliza kazi hiyo, Afisa elimu taaluma mkoa akatoa neno na kuuliza kama kuna mtu ana changamoto zozote. Mmoja wetu akasema hatujalipwa pesa ya kujikimu, akashangaa akasema mbona taarifa nilizonazo hakuna ambaye hajalipwa wote mkoa wa Lindi wamelipya. Akatoa agizo tulipwe lakini mpaka sasa hatujalipwa.
Inavyoonekana hizo pesa zilibadilishiwa matumizi, kwasababu baada ya kuwasumbua sana, wakasema tutawalipa kwa mapato ya ndani. Wanaongea hivyo ili tutulie kwasababu hawajawahi kuiweka hata kwenye bajeti, sasa unalipaje bajeti yake hauna.
Kiufupi wanatumia uwepo wa Waziri Mkuu, kama sehemu ya kuwakandamiza watumishi katika halmashauri hii, Mh. Waziri Mkuu anajitahidi sana kuboresha elimu huku kwake, anapambana apate walimu, lakini hawa viongozi wa halmashauri wanakwamisha mipango hiyo kwa maslahi yao binafsi, kiasi kwamba watumishi wengi wanatamani kuhama.
Mazingira sio rafiki kwa watumishi kubaki hapa. Kwahiyo pesa zetu za kujikimu mpaka sasa ni hazijatolewa.
Tunaomba serikali yetu iliyo makini iliangalie swala hili, kwasababu ni haki yetu kupata.
Asante!
Pia soma - Ajira mpya Afya Halmashauri ya Rombo hatujalipwa fedha za kujikimu