Dumuzi aendelea kukitafuna Chama cha Walimu Tanzania

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Chama cha walimu Tanzania ndio chama kikubwa kuliko vyote vya Wafanyakazi hapa nchini japo leo hii kina sura tofauti mbele ya jamii. Yanayojitokeza hivi sasa ni muendelezo tu wa vurugu zilizoanza baada ya kifo cha aliyekuwa katibu mkuu Alhaj Yahya Msulwa 2017. Hiki ndicho kipindi ambacho yaliibuka mafisadi ndani ya chama. Huduma kwa wanachama zilianza kupungua. Ikiwemo fedha zinazotumwa matawini, wilayani na mikoani. Mkono wa kwa heri (Golden Shakehand) ya kutoa mabati 20 kwa kila mwalimu anayestaafu ulifutwa na utitiri wa vikao vya kamati ya utendaji ya taifa visivyo na tija viliibuka. Mafisadi wale wamekuwa wakijiimarisha na nguvu zao kuongezeka kiasi cha kuweza hata kunyamazisha sauti za mabadiliko ndani ya chama. Rais wa chama Bi. Leah Ulaya alipokuwa akikemea ufisadi uliokuwa unafanywa na Deus Seif aliyekuwa katibu mkuu na Abubakari Alawi aliyekuwa mwekahazina wa taifa.

Leah alitengenezewa zengwe na kang’olewa madarakani kabla ya watajwa hapo juu kutiwa hatiani na mahakama ya kisutu na kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela. Cha ajabu ni kwamba Leah huyo huyo baada ta kurejeshwa madarakani na mkutano mkuu baada ya kipindi alishindwa kuendelea na msimamo wake. Baada ya kutoka jela viongozi hao waliendelea kufungua utitiri wa kesi dhidi ya chama na viongozi wake huku fedha za chama zikitumika. Hapa kuna la kujiuliza, jeuri hii wanaipata wapi.

Zimekuwepo taarifa mbalimbali na ushahidi kuwa yupo mwanasiasa mmoja mwandamizi ambaye amekuwa akilifadhili genge hilo kiasi cha kudiriki hata kuhujumu juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kushindwa kukutana na walimu kwa wingi wao kama karata yake ya pekee kuuaminisha mfumo kwamba yeye ndiye njia pekee na muhimu kuwafikia walimu, huku akitumia nafasi hiyo kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya malengo yake na genge lake. Mwanasiasa huyu mwandamizi amewahi kuwa mwenyekiti wa CWT wa moja ya mikoa ya kanda ya ziwa.

Utata wa uhalali wa Japhet Maganga ulitengenezwa na kiongozi huyo na genge lake baada ya kuona kuwa Mwalimu Maganga hakuwa anaingilika kirahisi. Itakumbukwa kwamba suala la kibali cha Maganga kwisha barua yake ilionekana kwenye tovuti na mitandao ya kijamii ya Tamisemi. Hata barua ya mkurugenzi wa Temeke ya kuonesha kuwa Maganga si mtumishi tena ilitumwa kwenye mitandao hiyo hiyo jambo lilioibua maswali kwa watu kwamba suala binafsi la mtumishi linawekwaje kwenye mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya wizara? hii ilikua nguvu ile ile ya mwanasiasa huyo.

Disemba 16, 2023, CWT ilipanga kufanya sherehe za kutimiza miaka 30 tangu kiundwe sanjari na maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani. Hafla hii ilipangwa kufanyika Mwanza, wajumbe wote walikua wameshafika Mwanza wakiwemo wageni kutoka vyma rafiki vya nchi za nje, wajumbe wa shirikisho la walimu Afrika mashariki, na wajumbe wa shirikisho la vyama vya walimu Duniani. Kwa mshangao wa kila mtu siku moja kabla ya sherehe hizo Bi. Leah Ulaya ambaye alikua ameghilibiwa na genge hilihili alitangaza kwenye vyombo vya habari kwamba sherehe zimefutwa eti kwa sababu mgeni rasmi ambaye alipaswa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa na udhuru. Tangazo hili alilitoa akiwa Dodoma katika mazingira ambayo si ya ofisini. Huku taarifa za ndani zikibainisha kuwa alitishiwa kudhalilishwa kwa kuwa genge hili lilikuwa na taarifa zake nyeti. Alitoa tangazo hilo wakati viongozi wote wa chama wakiwa Mwanza. Nyuma ya Pazia, ni mwanasiasa huyu huyu ambaye alitoa maelekezo walimu wanyimwe uwanja wa CCM Kirumba.

Walimu walikuwa na shauku ya kukutana na Rais wa JMT, pengine walitaka kuitumia fursa hii kubainisha changamoto walizo nazo na kutoa mawazo yao juu ya mustakabali wa elimu ya nchi hii. Walimu walivunjika moyo sana pengine hata yakaanza kujipenyeza mawazo kwamba huenda Rais hapendi kuwasikiliza. Katika hali ya kushangaza kiongozi huyu huyu wa serikali aliyefanikisha hujuma hizi amekuwa akikutana na walimu kisirisiri na hata waziwazi. Akiwa jimboni kwake alipokutana na walimu, Waziri mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alimuambia waziwazi hadharani kwamba amalize matatizo yanayokitafuna chama cha walimu.

Hizi zilikua ni busara za Waziri Mkuu mstaafu kwa kuwa pasi na shaka alimtambua Dumuzi anayekitafuna chama cha walimu na alitaka asikie kutoka kwenye kinywa chake mwenyewe. Katika kuendeleza juhudi zake za kujiimarisha kwa walimu kupitia chama chao, kwa maelekezo yake Chama kimeamua kupanga kufanya kongamano chini ya mwamvuli wa ujirani mwema litakalofanyika tarehe 26 Machi 2024 huko mjini Tabora anayelisimamia hilo ni rais wa chama Bi. Leah Ulaya ambaye kwa asili yeye na mwanasiasa huyu kwao ni kumoja na zimekuwepo taarifa mbalimbali kuwa kipindi mwanasiasa huyo akiwa rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha St. Augustine (SAUT) kwenye kampeni yake kwa nafasi hiyo alipata ufadhili kutoka moja ya nchi jirani ambako ndiko asili yake. Cha kushangaza mgeni rasmi wa kongamano la Tabora amepangwa kuwa mwanasiasa huyo huyo labda aahirishe baada ya kuiona taarifa hii na kwamba walimu wamepangiwa kufanya maandamano ya kumpokea ili kutuma ujumbe kwa watanzqnia kuwa yeye walimu wanamkubali na anaweza kuwa mkombozi wao.

Huku taarifa nyingine zikibainisha kuwa iwapo kwa namna yoyote hatakuwepo atamtuma mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako. Mikoa itakayohusika ni 8 ya kanda ya ziwa ikiwa na wajumbe kutoka Wilaya zote za kanda hiyo na pia Wenyeviti, Makatibu na Waweka Hazina wa mikoa yote nchini watahudhuria. Fulana na Kofia 45,000 zilizokuwa zimepangwa kutumiwa kwenye sherehe za Mwanza ndizo zitavaliwa na walimu siku ya maandamano. Cha kujiuliza, inakuaje chama kimeingia hasara ya kufutwa kwa sherehe za Mwanza kihuni, na hivi sasa chama hicho hicho kinaingia tena gharama ili kumpaisha mwanasiasa huyohuyo anayekihujumu?

Ni vyema ifahamike kuwa mwanasiasa huyu si rafiki wa walimu bali ni adui. Japokuwa mamlaka kwa umakini wake zimeshabaini sarakasi zake, bado watu wachache wanaumizwa kwa kufuata maagizo yake wengi wakiingia kwenye mkumbo kuwa anafanya hayo kwa maelekezo kutoka juu jambo ambalo halina ukweli wowote.

Uthibitisho wa mwanasiasa huyu kuingilia mambo ya chama cha walimu uliendelea kujidhihirisha kwenye mkutano wa Baraza la Taifa wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma Tarehe 15 Februari 2024 aliyekuwa RPC wa Dodoma Martin Otieno alielekezwa kutuma askari wawakamate baadhi ya viongozi wa chama cha walimu ambao walikuwa hawaungi mkono kuondolewa kwa Japhet Maganga kwenye nafasi ya ukatibu mkuu eti kwa kutokuwa na Kibali, na awekwe madarakani Joseph Misalaba ambaye hata yeye hana kibali cha kufanya kazi Chama cha Walimu kwani kibali chake kiliisha tarehe 14 Disemba 2023 ambapo ilibidi akaripoti kwa Mwajiri wake Mkurugenzi Halmashauri ya Kasulu pamoja na kwamba alikwisha kuondoshwa kwenye nafasi ya unaibu katibu mkuu na baraza la taifa tarehe 18 Juni 2023 na kufutiw uanachama.

Swali la kujiuliza, kwa nini mmoja asiye na kibali anaondolewa na mwingine asiye na kibali anawekwa madarakani. Martin Otieno hakutii maelekezo yake, tarehe 16 Februari mwanasiasa huyu kwa kutumia njia nyingine askari walimwagwa kwenye ukumbi na mmoja wa wajumbe Issa Bashasha ndiye alikuwa akiwaelekeza askari hao wajumbe wa kuwakamata ambapo walianza na Japhet Maganga mlengwa mkuu ambaye alikamatwa na Askari watatu wenye bunduki eti alikua akifanya fujo huku kwa uhalisia uliokuwepo ukumbini, fujo zilizoongozwa na Bi. Leah Ulaya ambaye alivua koti ili apigane na pia aliwarushia baadhi ya wajumbe chupa za maji. Viongozi waliokamatwa ni :

  1. Maganga Japhet Katibu Mkuu wa CWT
  2. Mahanya Kiyora mtumishi makao makuu
  3. Philemon Leo mwenyekiti wa Kyerwa
  4. Hamis Chinahova katibu wa Mwanza
  5. Hamis Ntundua Mwenyekiti wa Singida
  6. Alen Shuli katibu wa Shinyanga
  7. Daudi Mafwiri katibu wa Kilimanjaro
  8. Costa Paul mwenyekiti wa Kagera
  9. Aristides Ishengoma mwekahazina wa Mwanza
  10. Alphonce Mbasa Katibu wa Morogoro

Wakati wajumbe wanakamatwa na askari ukumbini, ilikuwa ni mbele ya viongozi wa Federation of East African Teachers Union na wajumbe wa shirikisho la vyama vya walimu Duniani (EI) lenye makao makuu yake Brussels nchini Ubelgiji lenye vyama 438 kote duniani na shirikisho hili lilitoa waraka kulaani kitendo cha serikali kuingilia uhuru wa vyama vya wafanyakazi na waraka huo umenakilishwa kwenye shirika la kazi la Umoja wa Mataifa(ILO). Hii inatokea kwenye kipindi ambacho serikali inaimarisha mahusiano yake kimataifa. Ulafi wa mwanasiasa huyu unaharibu sura ya nchi.

Viongozi hawa waliwekwa mahabusu ya kituo cha kati cha Polisi Dodoma tarehe 16 hadi 19 Februari 2024 na wakaendela kuripoti kituoni hapo kwa siku 8 baadae, hadi sasa hawajafunguliwa mashitaka na hatufahamu waajiri wao waliwaambia nini kwa kuwa hawakuwepo kazini kwa kipindi chote hicho bila ruhusa.

Ni vyema ieleweke kwamba, Dumuzi huyu anayekitafuna chama cha walimu ana mikakati yake ya kuhakikisha kwamba.
  1. Anamuaminisha mkuu wa nchi kwamba yeye ndiye anayependwa na kusikilizwa na walimu kwa kuwa alishawahi kuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama cha walimu na kwamba ili kuwapata walimu kwenye mustakabali wa kisiasa yeye ndiye mlango wa kuingilia.
  2. Anataka kuwaaminisha walimu kwamba yeye ndiye mkombozi wao huku akiamini kwamba walimu hawafahamu kuwa yeye ndiye amekuwa mfadhili wa genge lile lile la viongozi wa zamani wa chama waliokiibia chama hadi kufungwa gerezani 2022 tarehe 28 Juni. Na pia kwamba Kaimu Katibu Mkuu aliyepo ndiye aliyemuunga mkono kwa hali na mali alipochaguliwa kwenye mkutano mkuu uliofanyika Tanga 2023.
  3. Dhamira ya mwanasiasa huyu kwa kumtumia Kaimu katibu mkuu na rais wa chama ni kujinufaisha kwa fedha za chama zinazotokana na ada zinazolipwa na walimu kila mwezi kujinufaisha kisiasa. Aidha ni kuwatumia walimu hususani wa kanda ya ziwa kama mtaji wake wa kisiasa.
Inashauriwa kwamba ni vyema Serikali na mamlaka zake liangalie kwa jicho la pekee kiini cha changamoto zisizokwisha zinazochochewa na kufadhiliwa na dumuzi huyu na kuona kwamba utulivu unapatikana ndani ya chama cha walimu na walimu wanahudumiwa ipasavyo kwa kuwa chama ni chao na kinaendeshwa kwa rasilimali zao ndani ya nchi yenye utawala wa sheria.
 
Nchi ingekuwa chini ya Magufuli msingefanya huu upuuzi wenu wa kugombania madaraka kana kwamba mtaishi milele hapa duniani.

Mnateuliwa mpaka ukuu wa wilaya alafu mnakataa kwenda ili muendelee kukivuruga CWT.
 
Porojo nyingi na umeandika pumba Dumuzi Dumuzi si umtaje tu kama unaona huwezi acha kusumbua watu kenge maji ww
 
Mtaka nyingi na Saba hupata mwingi msiba,huyo Maganga angeenda kwenye UDC sahizi angekuwa anatumikia wananchi,Kama kakutuma atulie tu wakati umeshampita.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tunakushukuru umeandika vizuri sana na lazima utakuwa Mwalimu wa kiswahili maana ulivyozipanga hoja inatakiwa aje mwalimu mwingine kuzipangua. Lakini kwa sisi ambao sio waalimu lazima tuguseguse baadhi ya maeneo tu. Nimekuwa na maswali kadhaa kama ifuatavyo.
1.Waalimu ndio mnaotufundisha kila tukijuacho je tunajifunza nini toka kwenu?
2.Kama mnajua kidudu mtu kinachowakwamisha maendeleo yenu kinachokwamisha kukishughulikia ni nini?
3. Chama kimejaa Maofisa wa serikali (Tiss) na mnawafahamu kwanini mko kimya?
4. Mna posho za kila kikao ni nini hiyo? (kikao si ndo sehemu ya kazi yako kwa nini ulipwe kwa kuhudhulia kikao?)
5. Punguzeni ubinafsi Beba mataztizo ya mwenzio yawe ya kwako.
Nina maswali mengi nimechoka kuandika.
 
Kuandika Kwa code si vizuri weka wazi watu wajadili, kutaja dumuzi dumuzi ni sawa na lamuli chonganishi kiongozi
 
Back
Top Bottom