Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,628
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya Leo 23/01/2022
Leo ni mwendelezo wa mada ya wiki iliyopita kuhusu Spika Bora na Bora Spika, Kujiuzulu kwa Ndugai ni Mpango wa Mungu kwa Tanzania ili Tupate Spika Bora. Je CCM Ituteulia Spika Bora, au Bora Spika Kama Kawa?. Isipo...Karma Ita..
ambapo niliwaomba CCM ituteulie Spika Bora, kwasababu mteule wa CCM akiisha teuliwa na chama cha Mapinduzi, CCM, huyo ndie Spika, japo kwa sasa jina lililopendekezwa na CCM ni jina moja la Naibu Spika, Dr. Tulia Akson, kikao cha Wabunge wa CCM ambacho ndicho kilipaswa kiwe ni kikao cha uchaguzi wa jina moja kati ya majina matatu, kufuatia Dr. Tulia kuwa ni mwepesi sana kulinganisha na yale majina matatu, hivyo CC ya CCM, imeamua kukamilisha kazi ya jina moja, hivyo kikao cha wabunge wa CCM sio kikao tena cha uchaguzi, ni kikao cha kukamilisha tuu taratibu, na hata uchaguzi wa Spika utakaofanywa na Bunge la JMT, japo utakuwa ni uchaguzi kwasababu kutakuwa na wagombea wengine kutoka vyama vingine, lakini ukweli ni uchaguzi tuu wa kumthibitisha Dr. Tulia ili ni kukamilisha tuu taratibu, swali linabaki ni jee chaguo hili la Dr. Tulia ndiye Spika Bora?, au CCM imetuteulia tena Bora Spika?.
Wiki iliyopita nilisema Spika aliyetangulia hakuwa Spika Bora, bali alikuwa ni Bora Spika, hivyo ikitegemewa Naibu wake Dr. Tulia Akson pia atakuwa ni Bora Spika kwa kufuatia ile kanuni ya uwajibikaji wa pamoja ( a collective responsibilities), kwa makosa yote ya Bunge la JYN na naibu Spika Tulia, hivyo kati ya watu 70 waliogombea uspika kupitia CCM, miongoni mwao kuna watu mule wangetupatia Spika Bora kuliko Dr. Tulia, ila kwa vile aliyepitishwa na CCM ni Dr. Tulia, hivyo sasa Dr. Tulia Akson ndie Spika wetu.
Hii maana yake, ile sauti niliyoisikia hapa, Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... ilikuwa ni sauti ya Mungu
Dr. Tulia Akson ndiye mpango wa Mungu kuwa Spika mpya wa Bunge la JMT.
Moja ya maeneo magumu sana ambayo sisi media yetu ya Tanzania haina, ni eneo la kitu kinachoitwa "analysis" yaani uchambuzi yakinifu. Mimi ni miongoni mwa waandishi wachache wa Tanzania, tunaofanya uchambuzi yakinifu, na mimi hufanya uchambuzi huu kupita humu jf, na kwenye makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazotoka kwenye gazeti la Nipashe, kila siku za Jumapili. Hivyo nilifanya uchambuzi yakinifu, ya majina hayo 70 waliojitokeza CCM, katika uchambuzi huo, jina la Dr. Tulia halikuingia hata kwenye 10 bora!, za mtu wa kuwa Spika Bora. Wajue the Top 10 wa CCM watakaotoa, the top 5, top 3 na the best Spika. Angalizo, si lazima the best ndiye awe Spika, bali the chosen one!, kwenye uzi huu, niliweka jina la mtu ambaye angekuwa the best kutupatia Spika Bora, ili pia nikaweka angalizo kuwa Spika wetu, atakayepitishwa, sii lazima awe the best, but the chosen one, hivyo aliyechagulia ni Dr. Tulia.
Mambo mawili kwake.
Kwanza kwa vile she was tainted na madhaifu ya Bunge lililopita, hivyo kuonekana Dr. Tulia kama ni another Bora Spika, let's give her the benefits of doubt, kwamba japo alikuwa Naibu Spika chini ya Bora Spika, akitegemewa na yeye atakuwa ni Bora Spika, kosa kubwa la mtangulizi wake ni kukurupuka, ni kukurupuka huko, kukafanya taarifa ya kamati teule ya Bunge, kukurupushiwa kukabidhiwa kwa rais, bila kujadiliwa na Bunge, hivyo Bunge kuonekana kana kwamba linajipendekeza kwa serikali, Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?.
Ni kukurupuka huku kulipelekea Bunge letu tukufu kupitisha azimio batili, Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? tena Bunge lilipaswa kunishukuru sasa mimi, ndiye niliyewatonya azimio hilo lao ni batili, na kuwatonya nini kinakwenda kulikumba Bunge letu kama azimio hilo lingetekelezwa Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba, ndipo alizimio hilo batili, likafichwa chini ya uvungu kimya kimya as if halipo!, na ripoti ile ikapokelewa, hivyo kulinusuru Bunge!.
Ni kukurupuka huko ndiko kulimfanya JYN kutamka maneno yale kwenye ule mkutano wake na Wagogo, na baada ya video kusambaa, akakurupuka tena kuomba msamaha batili, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! akina sisi, tukampa ushauri wa busara, achutame kwa kujiuzulu, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? lakini mwenzetu akakomaa na hadi baada ya kusoma bandiko hili Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away? ndipo akakubali kunyoosha mikono juu kwa kukurupuka Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!
Kwa vile ukurupuka huo umefanyika huku Dr. Tulia, akiwepo, na Dr. Tulia nae kuonekana kama mkurupukuja kwa kutaka "to eat her cake and have it", kwa kuutaka Uspika, huku ameukumbatia Unaibu Spika na kuuatamia!. Lakini kama ilivyo kwa JPM na Samia, JPM was JPM na Samia ame prove She is Samia, hivyo lets give her a benefit of doubt kuwa Tulia akitulia, kama lilivyo jina lake, ana fursa na anaweza kabisa kuwa Spika Bora.
Pili tuahidi kumpatia kila aina ya Ushirikiano Spika Mpya Dr. Tulia Akson ili aweze kuwa Spika Bora.
Hongera sana, Spika wetu mpya, Dr. Tulia Akson Mwansasu
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.