Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

vazi la taifa halibuniwi bali hutokea lenyewe.huu ni upigaji tu.vazi la taifa la kenya lipi?marekani?uingereza?
Mavazi hutokana na mazingira tu.km wamasai,wamang'ati,wagogo.its natural.
Taifa utambuliwa kwa tabia za watu wake,vazi huja lenyewe.
Wizi tumechoka jamani.
 
hawa watatumia muda mwingi kwenye 'upuuzi' huu na baada ya hapo watabuni wazo lingine la CAKULA CHA TAIFA!
Ndio maana katika wizara ambazo wadau wa siasa wanasema zisiwepo ni hii ya Michezo na Utamaduni, kingekuwa kitengo/idara tu kwenye wizara nyingine.
Kuonyesha hawa jamaa wasivyo serious, wangelijiuliza maswali haya kabla ya kuamia huu mchakato:
  • 1. hivi ukienda Nigeria/Ghana ambao tunadai wana vazi la taifa kuna anayeweza kuleta ushahidi kuwa walikaa lini kubuni mavazi hayo!?
  • 2. Au kuna ushahidi kuwa kiliwahi kuwepo kikao cha kufanya Mbege iwe kinywaji cha Wachaga!?
tatizo ni aliyeasisi system na kuwaaminisha watu kuwa 'Kamati Kuu' ndio think tank ya nchi
Linchi lisiliokuwa na dira , limekufa. Tanzania ina priorities nyingi za msingi laikini kama watoto wadogo vile. Wanakimbilia mambo yasiyo ya msingi. Wanatufuta ulaji tuuuuu. Wanatangaza maredio yote na matv kuhusu vazi la Taifa as if we have nothing else to do. Halafu wasivyokuwa na akili hata kidogo wameshasema kitambaa cha rangi ya bendera ya TZ kitu ambacho kila mtu anajua. Sasa watanatufuta dizaini huku wanasema ni vazi. Ushenzi mtupu. Nawashauri wamtafute disigner proffessional na sio kutupigia mikelele isiyoisha wakati tuna njaa.
 
hi na wimbo wa taifa ulibuniwa na nani, kwa staili ipi!? ....ni kweli ulitumia mchakato huu?
 
hawa watatumia muda mwingi kwenye 'upuuzi' huu na baada ya hapo watabuni wazo lingine la CAKULA CHA TAIFA!
Ndio maana katika wizara ambazo wadau wa siasa wanasema zisiwepo ni hii ya Michezo na Utamaduni, kingekuwa kitengo/idara tu kwenye wizara nyingine.
Kuonyesha hawa jamaa wasivyo serious, wangelijiuliza maswali haya kabla ya kuamia huu mchakato:
  • 1. hivi ukienda Nigeria/Ghana ambao tunadai wana vazi la taifa kuna anayeweza kuleta ushahidi kuwa walikaa lini kubuni mavazi hayo!?
  • 2. Au kuna ushahidi kuwa kiliwahi kuwepo kikao cha kufanya Mbege iwe kinywaji cha Wachaga!?
tatizo ni aliyeasisi system na kuwaaminisha watu kuwa 'Kamati Kuu' ndio think tank ya nchi

Kweli mkuu.
 
hi na wimbo wa taifa ulibuniwa na nani, kwa staili ipi!? ....ni kweli ulitumia mchakato huu?

Watanzania bana nahisi kuna vikao vinakaa na posho zinalipwa kwa kuchakachua vazi la taifa.
 
kama mchakato ulianza 2004 kipi kili tusibu ukazimika gafla,nini kimeibua tena mchakato huu,je utazimika tena? Vipi ukizimika utaibuka tena ?
 
Kama mtanzania ukienda sehemu yoyote duniani na ukamuona mtu kajifunika/kavaa kanga lazima utamfutata huyo mtu kwa sababu Kanga ni vazi la Kiswahili.Tanzania ndio home of Kiswahili culture na ukimuuliza huyo mvaaji kanga lazima atatoa maelezo ambayo yatagusa Tanzania. ama alikuja yeye, au mtu aliyetembelea Tanzania alimnunilia.

Hapa naweza kusema kabisa kuwa Tanzania tunayo bahati kubwa ya kuwa na kitu kama kanga kwa sababu kanga sio tu maua bali pia kwa kawaida kanga inakuwa na 'msemo au ujumbe' ambao lazima mtu awe anafahamu Kiswahili ili aweze kuelewa nini kimeandikwa. Tukienda kwenye vitenge, karibu Afrika nzima inatumia vitenge, huwezi kudai hata kwa chembe kwamba kitenge ni asili ya Tanzania tofauti na ilivyo kwenye kanga. Kanga hata kama imetengezewa China lazima itengenezwe kwa kizingatia utamaduni wa Kiswahili.

Na kwa upande wa wanaume kaunda suti (zenye kola) ziko Tanzania na pengine India. Wachina wao hawana cola. Ukimuona mtu mwafrika kavaa kaunda suti (nadhani wote tunajua kaunda suti mshono wa Rais Kikwete, Mnyika etc) lazima huyo mtu ana connection fulani na Tanzania. Sasa mimi nilidhani kama ni vazi la taifa ni vizuri tuzingatie 'identities' ambazo zipo tayari.
Sioni kwa nini watu wanataka ku-reinvent the wheel wakati solutions zipo? If ain't broke don't fix it!


Pili, nimeona kwenye tv matangazo kuhusu ubunifu wa vazi la taifa kwa maana ya rangi (nadhani hapa wanaongelea rangi za kitambaa). Na kwenye matangazo hayo wanasisitiza uwepo wa rangi za bendera ya Taifa au/pia nembo ya kitaifa! Kwa sheria zilizopo sasa hivi ni kosa (kisheria) kuvaa bendera ya taifa au nembo ya taifa kinyume na sheria inavyoeleza. Wanasheria na hasa Tundu Lissu anaweza kutusaidia kwenye hili maana hata bungeni yuko mbunge mmoja wa CCM aliambiwa avue 'scarf' aliyokuwa amefunga shingoni. Sina hakika kama wajumbe wa hii kamati ya vazi la taifa wanalifahamu hili na sikukumbuki kama Dr Nchimbi akipeleka muswada bungeni ili kuruhusu nembo/rangi za bendera ya taifa kuvaliwa.

Ziko nchi nyingi watu wanavaa nguo, kofia hata tai zenye rangi ya bendera ya nchi zao. Sheria zao zinaruhusu, sasa kama sisi tunataka kufanya hivyo ni vema turekebishe kwanza sheria. Niliwahi kuuliza huko nyuma inakuwaje alama za bendera ya nchi zimetumika kwenye ZULIA la ukumbi wa bunge? Kipindi cha Mwl. Nyerere bendera ilikuwa na heshma mno pengine kwa sababu serikali ilijitahidi kuwaeleza wananchi matumizi ya bendera/rangi/nembo za kitaifa.

Mwisho, kati wa wajumbe wa hii kamati ya vazi nani ni mwanasheria?
 
hivi ni vazi la taifa au kitambaa cha taifa? Nani kaweka vipengele visivyo guswa kama kitambaa lazima kiwe na rangi za bendera ya taifa?
 
Kuwa na vazi la taifa as such sio jambo baya wala geni. Lakini litakuwa la aina gani is the issue especialy sasa wakati tumepoteza national identity. Ukiwa nje utaweza kuwa identify waganda, wanyaruanda na wakongo wanawake kwa mavazi yao na to an extent hata wanaume. Lakini dame wakiTZ ana kimini, kitaight pants au some times anablend utadhani kinyonga.
 
You can not pre- aarange vazi la taifa as it is part f your evolution. Tusipoteze wakati
 
wameteua waandishi wa habari ili kupunguza manunguniko, si magazeti hayataandika! Ila kwa maoni yangu hilo vazi litakuja automatic, halafu sio kweli vazi la taifa lina kuwa na rangi ya bendera, km ni hivyo si watu wanavaa wakati Serengeti boys inapocheza kuna watu walikaa wakabuni? Picha za mwanzo za uhuru Nyerere na Kawawa walikuwa wanavaa vazi la kiasili hatujaambiwa kwanini waliacha. Tufanye mambo ya msingi kama kufufua riadhaa na michezo mingine kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia badala ya kungangania vazi. Watu hawavaa timu ikiwa inafungwa bao 6 wataona aibu, imarisha michezo watu watakuwa proud na taifa na kuwa tayari kuvaa utambulisho wao mahali popote
 
Back
Top Bottom