Je, Somo la Civics (Uraia) linawasaidia wanafunzi kuijua nchi yao na kuwaandaa na siasa ya kesho?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam ndugu zangu,

Matokeo ya Kidato cha nne yametoka leo. Kama ilivyo kawaida kila mwaka, pia takwimu za masomo ya Mwaka huu zinaonesha ufaulu unaongezeka.

Kwa upande wangu nimetazama nilikuwa interested na somo la Civics ambapo pia nimeona ufaulu umeongezeka kwa mwaka huu 2023 ukilinganisha na mwaka 2022. Tazama hapa chini:

1706222402615.png

Jedwali linaloonesha kupanda kwa ufaulu wa masomo ya Sayansi Jamii ikiwamo Civics
Swali na hoja yangu hapa, Je Somo hili linatosheleza kuwafanya wanafunzi waelewe misingi ya Uraia wa Nchi yetu? Somo hili linawaandaa kuwa viongozi au Wanasiasa baadaye?

Kwa mtazamo wangu naona hili ni somo la muhimu sana kuanza kuwaandaa madogo toka chini.

Bila kujenga misingi bora ya somo hili, ni ngumu kujenga future ya Wanasiasa wazuri. Matokeo yake kila siku tutapata viongozi wa kurithishana madaraka na Chawa wao kupewa vitengo.
 

Attachments

  • PRESS CSEE 2023 Final 25 Jan 2024.pdf
    352.5 KB · Views: 1
Kuna waziri alipata F hilo somo na mnaona alivyo kilaza kabisa kwenye mambo madogo madogo.
 
Ndio hili somo linawaita waha ni watutsi, wahaya ni waganda na wamakonde ni wa Msumbiji

Lakini kwa kuwa wamasai ni fahari ya wazungu wanaonekana ni watanzania asili
 
Ndio hili somo linawaita waha ni watutsi, wahaya ni waganda na wamakonde ni wa Msumbiji

Lakini kwa kuwa wamasai ni fahari ya wazungu wanaonekana ni watanzania asili
Naona Muha unatapika ya rohoni.

Ukweli waburundi (wahutu) wengi wanajiita waha, hao ndiyo huwasababishia waha halisi kuwa na wakati mgumu wanapihitaji huduma za rahia halali wa kitanzania.

Waburundi wamejaa Dar, Geita Mara, Katavi, Tabora, Pwani, Mwanza, n.k. wanajiita waha wanamiliki ardhi na nafasi kibao serikali I, wengine wananufaika na miradi ya kumsaidia Kaya masikini Kama vile TASAF.
 
Wanasoma tu kutimiza wajibu. Mathalani, mimi nakumbuka tulifundishws mihimili 3 enzi hizo kuwa inajitegemea, lakini ukija mtaani Rais ni kila kitu.
 
Back
Top Bottom