Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Wakati wengi wanazungumzia ufaulu wa hesabu, jambo la kushangaza ni kwamba, waliopata A kwenye somo la hisabati ni wengi zaidi kuliko waliopata A kwenye somo la Civics. Hapa nimetumia masomo saba ambayo wanafunzi wote wanasoma na kuangalia ufaulu wa masomo hayo. Nimewaza zaidi inakuwaje watoto wanashidnwa kufaulu somo hili ambalo ni msingi wa wao kujua haki na wajibu wao ambao ndio msingi wa utawala bora na uwajibikaji.
Nikaenda kuangalia waliopata F yaani waliofeli somo hili, ama kwa hakika bado Civics haiko vizuri. Uraia (Civics) ni somo la kati kwa waliofeli kwa kuwa watu wamefeli zaidi hisabati, historia na Jiografia kisha wanafuatiwa na Uraia. Kiswahili ndio kimeonekana kuwa na watu wachache waliofeli wakifuatiwa na biologykisha kiingereza. Yaani watoto wa kidato cha nne, ni maridadi wa biolojia kuliko uraia, very strange.
Hata hivyo nimeona shida kwenye uwekezaji wa elimu ya Uraia, yaani Civics lina vitabu vichache zaidi kwa kulinganisha na masomo mengine. Hii ni kwa shule za serikali na binafsi kwa mujibu wa takwimu za TAMISEMI(BAEST). Somo lenye vitabu vingi ni hisabati.
Vitabu vya uraia ni 9% ya vitabu vyote vya masomo yanayosomwa na wanafunzi wote wa shule ya upili. Je, jambo hili ni la makusudi ili watu wasiwe na ufahamu wa kutosha kuhusu haki na wajibu wao katika taifa?