Je, Serikali "imevilazimisha" vyombo vya habari viripoti habari nzuri pekee za watawala wa CCM?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kwa nchi yoyote yenye utawala Bora, inavitumia vyombo vya habari kama mhimili wao wa 4, usio rasmi, baada ya mihimili rasmi ya Serikali, Mahakama na Bunge, katika kuendesha nchi.

Huwa wanavitumia vyombo vya habari kama "watchdogs" vyao Kwa kuwa huwa wanakosoa, Ili serikali Ione mapungufu yake Ili ijirekebishe, katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hali ni tofauti Sana hapa nchini kwetu, Kwa kuwa mihimili yote 3, yaani Serikali, Mahakama na Bunge, yote ni kama "imemezwa" na Mhimili wa Serikali, ambao ndiyo unaoelekea kuwa "umejichimbia" zaidi chini, hivyo kufanya mihimili mingine ya Bunge na Mahakama kutoweza kufurukuta!

Hata hivyo pamoja na mihimili hiyo 2 "kumezwa" na Mhimili mmoja, ambao ni Serikali, Bado hufanya Mhimili mwingine, usio rasmi, wa vyombo vya habari, kufanya kazi yake ya kukosoa Kwa weledi mkubwa, hivyo kuufanya Mhimili wa Serikali, kufanya kazi yake ikijirekebisha pale ilipokosolewa.

Hapa nchini kwetu, Mhimili wa Serikali, unachukua nafasi ya u-mungu-mtu, ambao hautaki kabisa kukosolewa na hivyo kufanya utawala Bora, kuwa kama hadithi tuuu ya alifu lela ulela!

Serikali inaweza kusema inatoa uhuru Kwa vyombo vya habari, pamoja na vile vya binafsi, kuwa huru, lakini "indirectly" uhuru huo wanauminya!

Kwa kuwa vyombo vya habari, hususani magazeti, hujiendesha Kwa kutumia matangazo ya biashara, na Serikali ikiwa ndiyo mtoaji mkubwa wa matangazo hayo, huweza "kuvipendelea" vyombo vya habari vinavyosifu sifu utawala huu wa CCM, Kwa kutumia lugha yao kuwa "Rais Samia anaupiga mwingi"na hivyo kutotoa matangazo hayo Kwa vyombo vya habari, ambavyo vinatekeleza wajibu wao kikamilifu wa kukosoa na hivyo kuvinyima matangazo hayo na hivyo kuvifanya vyombo hivyo vya habari binafsi, kutoweza ku-survive katika soko hilo.

Kwa Serikali kujifanya Iko 100 percent perfect, ndiko kunakoifanya ifanye figisu figisu hizo za kuvinyima fursa hiyo ya matangazo vyombo hivyo vya habari ambavyo viko "serious"

Hivi katika nchi kama yetu, ambayo imeweka mfumo wa kumfanya Rais wetu, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chake, kuwa kama mungu- mtu, ambaye ni binadamu, kutotoa nafasi ya kukosolewa, kunadhoofisha Sana mfumo wa utawala Bora.

Kwani vitabu vyote vya dini vinaamini kuwa ni Mungu pekee, ambaye yuko 💯 percent perfect, ambaye hapaswi kukosolewa.

Lakini sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na hivyo kutufanya kutumia njia ya kukosolewa kama njia ya kujirekebisha na hivyo kurudi kwenye msitari.

Ukiviacha vyombo vya habari vya mtandaoni kama Jamii forum, ambavyo uhuru wao wa kukosoa uko juu, vyombo vingine vya habari, kama vile magazeti, Televisheni na Radio, uhuru wao wa kutoa habari unathibitiwa na Serikali na upo chini Sana hapa nchini kwetu.

Dawa pekee na ya kudumu ni kupata Katiba mpya, ambayo itaweka mifumo imara ya kiuongozi wa nchi
 
Kwa kuwa vyombo vya habari, hususani magazeti, hujiendesha Kwa kutumia matangazo ya biashara, na Serikali ikiwa ndiyo mtoaji mkubwa wa matangazo hayo, huweza "kuvipendelea" vyombo vya habari vinavyosifu sifu utawala huu wa CCM, Kwa kutumia lugha yao kuwa "Rais Samia anaupiga mwingi"na hivyo kutotoa matangazo hayo Kwa vyombo vya habari, ambavyo vinatekeleza wajibu wao kikamilifu wa kukosoa na hivyo kuvinyima matangazo hayo na hivyo kuvifanya vyombo hivyo vya habari binafsi, kutoweza ku-survive katika soko hilo.
hii kinaitwa factors that shaping the news!, he who pays the piper, may call the tune!.
Kwa Serikali kujifanya Iko 100 percent perfect, ndiko kunakoifanya ifanye figisu figisu hizo za kuvinyima fursa hiyo ya matangazo vyombo hivyo vya habari ambavyo viko "serious"
Sii kweli, serious media haitakiwi kuitegemea serikali!, Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?
Hivi katika nchi kama yetu, ambayo imeweka mfumo wa kumfanya Rais wetu, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chake, kuwa kama mungu- mtu, ambaye ni binadamu, kutotoa nafasi ya kukosolewa, kunadhoofisha Sana mfumo wa utawala Bora.
Mbona tunasifu na kukosoa?. Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!
Kwani vitabu vyote vya dini vinaamini kuwa ni Mungu pekee, ambaye yuko 💯 percent perfect, ambaye hapaswi kukosolewa.
Naunga mkono hoja, Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!
Lakini sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na hivyo kutufanya kutumia njia ya kukosolewa kama njia ya kujirekebisha na hivyo kurudi kwenye msitari.
Hata Samia sio malaika Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Ukiviacha vyombo vya habari vya mtandaoni kama Jamii forum, ambavyo uhuru wao wa kukosoa uko juu, vyombo vingine vya habari, kama vile magazeti, Televiisheni na Radio, uhuru wao wa kutoa habari upo chini Sana hapa nchini kwetu.
Ni kweli

Not necessarily!, katiba mpya is not a panacea ya matatizo yote nchini kwetu!.
P
 
Wewe Kama una habari mbaya na ndio zikufurahisha si uripoti hata kutokea if kwani Kuna tatizo?

Kwenye haya magazeti hapa chini Kuna habari nzuri tuu? 👇
20221229_053546.jpg
20221229_053530.jpg
20221229_053420.jpg
20221229_053637.jpg
20221229_053617.jpg
20221229_053723.jpg
20221229_053747.jpg
 
Wewe Kama una habari mbaya na ndio zikufurahisha si uripoti hata kutokea if kwani Kuna tatizo?

Kwenye haya magazeti hapa chini Kuna habari nzuri tuu? 👇View attachment 2461643View attachment 2461644View attachment 2461645View attachment 2461646View attachment 2461647View attachment 2461648View attachment 2461649
Vipo vyombo vya habari vichache, ambavyo vina uthubutu wa kukosoa Ili watawala wetu, wajirekebishe na warudi kwenye msitari na watuongoze Kwa haki.

Katika vyombo hivyo vya habari vya binafsi, pamoja na kufanyiwa figisu figisu za "kubaniwa" kupewa matangazo na Serikali, Sina budi kutoa kongole Kwa gazeti la Raia Mwema🤝
 
Vipo vyombo vya habari vichache, ambavyo vina uthubutu wa kukosoa Ili watawala wetu, warudi kwenye msitari na watuongoze Kwa haki.

Katika vyombo hivyo vya habari vya binafsi, pamoja na kufanyiwa figisu figisu za "kubaniwa" kupewa matangazo na Serikali, Sina budi kutoa kongole Kwa gazeti la Raia Mwema🤝
Kwani vilianzishwa ili kutegemea matangazo ya serikali unayoikosoa? Huko Ni kukosea njia sasa
 
Huo ndiyo ukweli mchungu ambao watawala wetu wa CCM hawataki kuusukia.

Hebu jaribu ku-imagine, inawezekanaje vijarida vinavyotoa habari, mothili ya udaku viweze ku-survive, wakati magazeti "serious" ya Tanzania Daima na MwanaHalisi yaachwee yafe?

Jibu ni Moja tu, vijarida hivyo vyenye kazi Moja tu ya kuwasifu na kuwaabudu watawala wetu wa CCM vinapewa upendeleo maalum wa kupewa matangazo na Serikali yetu isiyopenda kukosolewa!🤬
 
Hebu jaribu ku-imagine, inawezekanaje watu ambao wanatajwa kuiba mabilioni ya shilingi, Kila mwaka, katika ripoti zake CAG, hawachukuliwi hatua, wakati magereza yetu yamejaza wafungwa, ambao ni wezi wa kuku?

Jibu ni kuwa vyombo vya habari havisaidii kupiga kelele, Ili kukomesha uonevu huu wa haki za binadamu hapa nchini
 
hii kinaitwa factors that shaping the news!, he who pays the piper, may call the tune!.

Sii kweli, serious media haitakiwi kuitegemea serikali!, Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Mbona tunasifu na kukosoa?. Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Naunga mkono hoja, Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!

Hata Samia sio malaika Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Ni kweli

Not necessarily!, katiba mpya is not a panacea ya matatizo yote nchini kwetu!.
P
Nambie sekta yeyote ambayo nchi yetu imefanikiwa kwa kiwango cha kimataifa. Uchumi, elimu, michezo, afya, siasa nk. Kifupi sekta ya habari haiwezi kuwa kisiwa katika bahari. Wanahabari wetu wengi wanapitia mfumo wa elimu ulio dhaifu. Watu wanashindana kununua Phd madukani.

Kifupi nchi yetu ni kama imelaaniwa. Siku hizi hata hapa jf ukuiikosoa serikali uzi unaondolewa haraka. Uhuru pekee wa habari tuliobaki nao ni wa kuongelea kwenye mabaa na migahawa kwa tahadhari
 
Unataka kuniambia kuwa hata hapa JF uhuru wa kutoa habari haupo?🤐
 
Not necessarily!, katiba mpya is not a panacea ya matatizo yote nchini kwetu!.
P
Katiba mpya na iliyo bora bila shaka ndiyo suluhu ya matatizo ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini. Kwasabb itatoa uhuru wenye mipaka kwa mkosoaji na mkosolewa. Itamdhibiti kwa kumpa mamlaka yenye ukomo huyu ambaye Sasa tunamuita mungu-mtu.

Mamlaka za utoaji haki zitakuwa huru na kuondoa kabisa tabia iliyopo Sasa ya kuziendesha kwa nguvu kutoka juu.

Bunge litatimiza wajibu wake ipasavyo na kufuta kabisa hali ya sasa ambapo halina tofauti na kwaya kuu pale parokiani.
 
Vipo vyombo vya habari vichache, ambavyo vina uthubutu wa kukosoa Ili watawala wetu, wajirekebishe na warudi kwenye msitari na watuongoze Kwa haki.

Katika vyombo hivyo vya habari vya binafsi, pamoja na kufanyiwa figisu figisu za "kubaniwa" kupewa matangazo na Serikali, Sina budi kutoa kongole Kwa gazeti la Raia Mwema🤝
Mkuu Mystery , hakuna kitu kizuri kama appreciation ya kizuri kidogo kilichopo na mimi najisikia fahari kuwa sehemu ya Raia Mwema
RM.jpg
WhatsApp Image 2018-04-12 at 11.39.14.jpeg
WhatsApp Image 2018-04-12 at 11.39.15.jpeg
 
hii kinaitwa factors that shaping the news!, he who pays the piper, may call the tune!.

Sii kweli, serious media haitakiwi kuitegemea serikali!, Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Mbona tunasifu na kukosoa?. Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Naunga mkono hoja, Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!

Hata Samia sio malaika Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Ni kweli

Not necessarily!, katiba mpya is not a panacea ya matatizo yote nchini kwetu!.
P
Bwana Mayala tangu wakati ule Magufuli alipokupiga na kitu kizito haujawahi kurudi kwenye mstari.
 
.Kifupi nchi yetu ni kama imelaaniwa. Siku hizi hata hapa jf ukuiikosoa serikali uzi unaondolewa haraka. Uhuru pekee wa habari tuliobaki nao ni wa kuongelea kwenye mabaa na migahawa kwa tahadhari
Naomba utofautishe uhuru wa kuikosoa serikali na uhuru wa kutokana serikali na viongozi wake. Kama ni ukosoaji with facts, if bado tunaongoza sana kuisaidia serikali kwa ukosoaji na nyuzi hazifutwi!. Ila kuna wenzetu humu ambao sio wazima, badala ya kuikosoa serikali wao ni kutokana na kuwatukana viongozi, if modes ni wazima wako macho na halali.
P
 
.Hii fortification ilianza tokea awamu ya nne mwishoni,awamu ya tano ikamultiply maradufu mpaka sasa.. kiufupi hawa jamaa they have given up on reasoning to win the consensus to govern,SASA hivi ni propaganda + nguvu tu
 
Back
Top Bottom